Zitto ndani ya kumekucha ITV

Kutoka kipindi cha mahojiano asubuhi hii ITV Zitto Kabwe ametangaza kumuunga mkono Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana kwa uamuzi wake wa kukataa na kukataza wanaccm kuitana waheshimiwa. Anasema tulipoacha kuitana Ndugu ndipo matabaka na kasi ya kujilimbikizia Mali na madaraja katika utoaji huduma ilipoanza. Je, Ndugu ni physchological factor katika kujenga nchi moja. Tuendelee na mjadala.
 
Anasema wenzetu Senegal wameweza ku-trace fedha zao zilizo kuwa zimefichwa Uswis kupitia bank ya dunia na wameweza kurejesha fedha zao, sisi tukiamua kufanya kama wao tunaweza, serikali inaonekana haiko tayari.

Azimio la bunge nila aina yake kwa kuwa hakuna nchi yoyote imekuwa na azimio kama hili. Cha msingi ni kuwa na nia ya dhati kwa wabunge wengine ili kuoko fedha hizo.
 
Mimi binafsi sioni uhusiano wa karibu kati ya watu kuitwa waheshimiwa na suala la ufisadi.[This means coefficient of correlation is equal to zero].
 
hiki kichwa ni hazina kwa taifa.
lazima tukiunge mkono lakini tukikishauri kipunguze wenge saa nyingine.

mkuchika ashughulikiwe na bunge kwa kukiuka azimio la bunge.
 
AMUOMBE PIA BW JANGILI AWE KAMPENI MENEJA WAKE KT HARAKATI ZA KUGOMBEA URAISI KUPITIA CHADEMA KWAN KINANA NI MENEJA MZUR WA KAMPENi
 
"Wasiwasi wangu ni watu wa serikali kukata tamaa"

"Hatuwezi kuwataja tu maana tumeshawataja hata mafisadi kwa majina lakini hakuna kilicho fanyika"

"Lazima tubadili mbinu, ambayo itawafanya wahusika kuwajibika na si kutaja tu halafu hakauna kinacho fanyika"
 
"Tanesco ni kweli kuna ubadhirifu mkubwa sana na hii ni ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, kuna zadi ya dola milioni mia nne na hamsini na nne zimeibwa"

"Kuna raketi ya watu ambao wao kazi yao ni kupiga deal kwa umeme wa dharua"

"Mpango wa umeme wa dharura umekwisha kwa nini unaendelea huku wakiendelea kulipwa"
 
"Fedha zimetoka hazina kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mitambo na watu wamechikichia, mafuta hayaja nunuliwa na hakuna hatua zilizo chukuliwa"
 
Zitto!! Ulijibu maswali 100 kwa ufasaha,ila hoja hii moja umechemsha!!eti nini?ukiitwa mheshimiwa unakuwa fisadi/mwizi? Hapana,yeye kinana ambaye si mheshimiwa(mwizi a k a fisadi)arudishe basi uhai wa tembo wetu alioshiriki kuwaangamiza na hatimaye kubainika akisafirisha mzigo huko asia!! Eti huyu ndiye mtu safi kabisa ccm!!ptuuuu
 
"Waziri wa fedha nataka atoe taarifa ni kiwango gani cha fedha kimetoka kwa ajili ya kununua fedha, sasa hivi kwa sasa tunatumia zaidi ya bilioni 172 kwa ajili ya kununulia mafuta mazito ya umeme wa dharura" duhh halafu kuna wajinga wanasema elimu bure haiwezekani! Kina chama na Ritz aibi yenu.
 
Last edited by a moderator:
"Fedha zimetoka hazina kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mitambo na watu wamechikichia, mafuta hayaja nunuliwa na hakuna hatua zilizo chukuliwa"

Anasema kila mwezi tanesesco wanatumia zaidi ya dola milion 70,wasiwasi wake ni je pesa hizo ni kweli zinatumika ama zinaliwa?
 
Nampata hapa Zitto ngoja tuone strategy zake za kuwa introduce kwa sirikali wale waliompa taarifa ambao ni mswizz na muingereza!!
 
Last edited by a moderator:
Haaaaa Zitto amependekeza waandishi wa habari wawe wanawahoji kama walivyofanya JF wamemuhoji masaa nane na wamemuuliza maswali magumu na mengine ya kuuzi...
 
Last edited by a moderator:
Kwa style hii kuna dalili za Baba Mwanaasha kuikimbia magogoni kabla ya mda wake au Zitto watammwakyembe
 
"Watanzania wamekosa matumaini, ni lazima tuanze upya kujenga matumaini kwa wananchi wetu"

"Bunge limeingia kwenye mtego wa kuanza kupoteza matumaini kwa wananchi"

"Vyombo vya habari zina nafasi kubwa sana ya kujenga imani kwa wananchi"

"Jamiiforums nimefanya mahojiano nao kwa masaa 8 wananchi wameuliza mengi, vyombo vya habari vina nafasi kubwa kwenye kurejesha imani kwa wananchi"

"Ripoti ya ngwilizi inatakiwa iwekwe wazi ili wabunge waijadili"
 
Kamanda Zitto yuko hewani kwenye kipindi cha kumekucha cha ITV akiongelea walioficha fedha Uswis.
kaka naomba uendelee kutujuza
nipo mbali kidogo na JF imeshaniathiri nipo darasani but naendelea kufuatilia kinachojiri
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom