Zitto: Naipongeza Serikali kwa Kuchukua Hatua Juu ya Sakata la Escrow

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,740
4,230


Kwa dhati kabisa naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama changu kuipongeza Serikali kwa hatua hii ya kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa wa Sakata la Escrow kama ilivyoazimiwa na Bunge Septemba, 2014.

Hii ni hatua muhimu sana katika mapambano dhidi ya Ufisadi nchini.

Nasikitika ndugu yangu Deo Fulikunjombe hayuko hapa kushuhudia matokeo haya ya kazi kubwa aliyoifanya kwaajili ya Taifa.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Mikumi- Morogoro Juni 19, 2017
 
Tatizo ni JK habebeki bora tu turuhusiwe kumjadili kwa maovu aliyotufanyia watanzania...chonde chonde JPM Huyu Kikwete afilisiwe ndio ROHO za watanzania zitatulia na kukuunga mkono kwa dhati ya mioyo yetu
 
Bado waliolamba hela za Barrick aka ACACIA kwa kisingizio cha miradi ya maendeleo.
 
Bado na ile mikataba inavyosemekana ilikuwa ya gesi , maana nakumbuka wakati inapitishwa kule bungeni wabunge wa upinzani walifanyiwa hila/hiyana ili wasuse/wazire ili wabunge wa chama cha makinikia wapitishe ile mikataba kwa hila! Arobaini Yake itafika nayo nazani muda si mrefu! Vipi kuhusu mkataba wa ticks kule Bandarini
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom