Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 1,743
- 4,270
Kwa dhati kabisa naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama changu kuipongeza Serikali kwa hatua hii ya kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa wa Sakata la Escrow kama ilivyoazimiwa na Bunge Septemba, 2014.
Hii ni hatua muhimu sana katika mapambano dhidi ya Ufisadi nchini.
Nasikitika ndugu yangu Deo Fulikunjombe hayuko hapa kushuhudia matokeo haya ya kazi kubwa aliyoifanya kwaajili ya Taifa.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Mikumi- Morogoro Juni 19, 2017