Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Makinda anajua gharama ya Zitto kuusoma ushahidi bungeni leo. Hawezi kumruhusu
Mbona Godbless Lema hajapewa nafasi kudhibitisha uongo wa Pinda..
Akishindwa watamvictimise kama kawaida ya bunge la magamba. Nasi tuwe tayari kudai kwa nguvu zote uthibitisho wa waziri mkuu kulidanganya bunge kuhusu mauaji ya Arusha wa Lema. Bi Kiroboto upo kwenye kona BE CAREFUL afadhali uiweke kabatini kama ya Lema LA SIVYO!!!!HATMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliyelituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa kubadili msimamo wa kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge itajulikana leo.
Hatua hiyo inatokana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumwagiza Zitto kuwasilisha utetezi wake hadi kufikia leo baada ya agizo lake la mara ya kwanza alilolitoa Juni 23 kumtaka mbunge huyo kuwasilisha utetezi huo hadi kufikia Juni 29 kugonga mwamba.
Hata hivyo, ulishindwa kutolewa uamuzi siku hiyo (Juni 29) baada ya siku ya kwanza ambayo Zitto alitakiwa kuthibitisha kauli yake kuwasilisha barua kwa Spika akiomba amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha zinazohusu mjadala wa CHC ambazo zitamsaidia katika utetezi wake, jambo ambalo Spika alisema alishindwa kumsaidia kwa kile alichoeleza kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri.
Baada ya tamko hilo la Spika bungeni kumtaka Zitto kuwasilisha utetezi wake, mbunge huyo alimzunguka na kuamua kuwasilisha utetezi wake na vielelezo Alasiri ya siku hiyo (Juni 29).
JE ATANUSURIKA NA HUO USHAHIDI WAKE LEO BUNGENI ATAKAPOKUWA ANAUSOMA MBELE YA BUNGE?
Watu wa Kigoma wachawi sana, nina uhakika atanusurika tu mara hii tena.
Hakuna siri ya kufanya kitu haramu.Inasemekana kuna ka sheria kanakokataza kuwa na 'siri' za serikali. Vpi kama kweli kapo kakitumiwa kumnanihii Zitto?! iwapo tu ni kweli kaanika nini Baraza la Mawaziri liliazimia!
Hee bado upo tu,si ulisema unaenda fb?kunani tena.Sasa uchawi umeingiaje hapa?Watu wa Kigoma wachawi sana, nina uhakika atanusurika tu mara hii tena.
Sure, we beg him to exposeZito atuletee huo ushahidi hapa jamvini