Zitto na ushahidi wake Bungeni (Mawaziri kushawishiwa kutoa maamuzi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto na ushahidi wake Bungeni (Mawaziri kushawishiwa kutoa maamuzi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Jul 4, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  HATMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliyelituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa kubadili msimamo wa kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge itajulikana leo.

  Hatua hiyo inatokana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumwagiza Zitto kuwasilisha utetezi wake hadi kufikia leo baada ya agizo lake la mara ya kwanza alilolitoa Juni 23 kumtaka mbunge huyo kuwasilisha utetezi huo hadi kufikia Juni 29 kugonga mwamba.

  Hata hivyo, ulishindwa kutolewa uamuzi siku hiyo (Juni 29) baada ya siku ya kwanza ambayo Zitto alitakiwa kuthibitisha kauli yake kuwasilisha barua kwa Spika akiomba amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha zinazohusu mjadala wa CHC ambazo zitamsaidia katika utetezi wake, jambo ambalo Spika alisema alishindwa kumsaidia kwa kile alichoeleza kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri.

  Baada ya tamko hilo la Spika bungeni kumtaka Zitto kuwasilisha utetezi wake, mbunge huyo alimzunguka na kuamua kuwasilisha utetezi wake na vielelezo Alasiri ya siku hiyo (Juni 29).

  JE ATANUSURIKA NA HUO USHAHIDI WAKE LEO BUNGENI ATAKAPOKUWA ANAUSOMA MBELE YA BUNGE?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli aliwasilisha ushahidi huo (kwa maana ya nyaraka za baraza la Mawaziri), na hata kama ushahidi wake utashindwa kuthibitisha wazi wazi tuhuma/shutuma alizotoa, jambo moja litabaki kwenye historia ya Nchi yetu kwamba "hakujapata kutokea Serikali ya kijiweni kama hii".

  Nyaraka za Baraza la Mawaziri ni Siri na Mhe. Zitto anaelewa hilo, kwa kuziweka hadharani atasaidia kuanzisha mjadala kuhusu uadilifu wa baadhi ya Mawaziri na Maafisa wanaohusika na Baraza la Mawaziri, mwisho wa Siku (bila hata kujali kama tuhuma/shutuma za Mhe. Zitto zimethibitishwa au la) tutawaomba JK na Baraza lake wajiuzulu kupisha Uchaguzi Mpya.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Zitto ni jembe lenye makali, sina wasiwasi na ushaidi wake. Namwonea huruma spika!
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  hivi LEMA si aliwasilisha ushahidi wa uongo unaomhusu PM? mbona huyu mama kaukalia? au unamnogea?
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ushahidi upo. Hata mimi ninao. Tatizo litakuwa ni ushabiki wa Spika Makinda.
   
 6. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  za lema zinamiez4 lakin mpaka leo hawajampa nafas ya kuiwasilisha
   
 7. n

  niweze JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwleli ubongo wako na akili zinazotoka ndani ya wanachama wa ccm defects tupu. Hivi Zitto analozungumzia huoni ni kwa manufaa ya kwako na familia yako? You guys need to be thrown in a den of fire
   
 8. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Hii kitu itaishia hivi hivi tu kimya kimya, kwani Lema, Kafulila na Mwesiga si waliombwa walete ushahidi na walishapeleka lakini hatusikii chochote? Hii tabia ya kukalia vitu muhimu (kuanzia kwa Amiri Jeshi Mkuu, Waziri Mkuu, Spika mpaka viongozi wa ngazi za chini) inakipotezea chama mwelekeo kwa spidi kubwa.
   
 9. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata PM alitaka utajiwe kama kweli kuna mawaziri wanaishi hotelini wakati nyumba zao zilishajengwa alipotajiwa Shamsi Vuai Nahodha yeye alijbu nimekusikia ... kwisha. Hivyo hizi thibitisho wanazoomba nikuua mjadala unaondelea watu wa-"concentrate" kama uthibitisho upo au la na hoja inakua teyari imepotezewa kiaina ...
   
 10. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cdm wasikubali ushahidi wa Zito utolewe kabla ya ule wa Lema. kwa nini ule ushahidi wa Lema spika ameukalia, atoe kwanza wa halafu ndo ufuate wa Zito
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hapa kunakamchezo sisiem wanafanya!
   
 12. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ndugu unataka ushaidi wa lema usomwe bungeni huku pinda akiwepo?unajua madhara yake?moja,bunge halitakuwa na imani na serikali tena kwani jamaa amethibitisha kuwa pinda ni muongo.pili pinda itambidi ajiuzuru sababu kalidanganya bunge na taifa zima. Tatu pinda atazaraulika mbele ya jamii na kuonekana mtu asiye makini.utetezi wa lema ulikuwa unanguvu sana na wauhakika.
   
 13. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ni njia iliyobuniwa na ccm kujaribu kukandamiza demokrasia bungeni,wanataka siku mtu akishindwa kuthibitisha tu wambane na aonekane ni mzushi but kwa cdm hawawezi.
   
 14. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tusubiri Mamaa Makinda atuwekee ushahidi wa jembe mh. Zitto
   
 15. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Unamuonea huruma spika kwa lipi, niko kwenye TV mda huu nataka nishuhudie kama Zitto atapewa nafasi na kuvuka huu mtego..
   
 16. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Mbona Godbless Lema hajapewa nafasi kudhibitisha uongo wa Pinda..
   
 17. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mambo ni yale yale tulitegemea SPIKA angemuhitaji ZITTO kuthibitisha kauli yake lakini naona muda wa maswali umepita na ZITTO hajaitwa kuthibitisha,
   
 18. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Zitto yumo Bungeni?
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  hA HA HAAAA!
  Yaleyale ya Gdbless Lema na MKPP!
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyo mama bunge limemshinda!
   
Loading...