Zitto na pesa za sensa ya watu

Neema William

Senior Member
Jan 3, 2012
171
76
Neema Kishebuka, Dsm

Kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) iumewataka wabunge wa chama hicho kurudisha pesa zilizowekwa katika account za wabunge kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la kuhesabu watu linalotarajiwa kufanyika nchini kote Agost 25 mwaka huu.

Kamati hiyo iliyokutana jijini hapa imetoa maagizo hayo na kuwataka wabunge wake kuzirudisha fedha hizo kwa katibu wabunge wake baada ya kuzipitia akount zao na kubaini kuwepo kwa pesa hizo kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mbunge zilizowekwa katika akaunti zao.

Kamati hiyo imesema kuwa si halali wabunge hao kupokea pesa hizo kwa kuwa ni wajibu wao kuhamasisha zooezi la sensa katika maeneo hayo.

Imeelezwa kuwa ni wajibu wa wabunge kushughulikia masuala ya kiserikali kama ya sensa ya watu na makazi hivyo kupokea pesa Hizo ni sawa na rushwa kwani ni wajibu wao.

Hata hivyo wabunge hao wamekanusha kupata taarifa ya kuingiziwa pesa Hizo na ofisi ya Bunge na kuahidi kuzinagalia akaunti hizo na endapo watakuta pesa zimeingizwa watazirudisha kama kamati kuu ilivyoagiza.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, aliwaasa wabunge wa CHADEMA kuwa makini na pesa zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ambayo tayari ni wajibu wa wabunge wa Bunge hilo lililo chini ya Ana Makinda.

"Hii ni rushwa ya wazi ndugu zangu, mimi nimeambuwa na katibu wa Bunge kuwa amewaingizia milioni moja kila mbunge sasa ni wajibu wetu kurudisha pesa hizo kwakuwa ni wajibu wetu kufanya kazi za kijamii'' alisema Zitto.
 
Kashilila weeweeee na Makinda jamani hamna haata huruma na walalahoi???kwa nini msitumie media kuhamasisha??rushwa wazi kabisa na kipindi hiki cha kura ya kutokuwa na imani na JK/Pinda
 
Kwahiyo mil kama 300 hivi ndio hivyo tena! Mwambieni huyo Malkia wa bunge mdogo wangu anasoma udsm hana mkopo na hali kifamilia haielezeki! USHAURI¤¤ Ili wasiwe wanaaibika ovyo, wawe wana-consult kamati kuu ya cdm kabla ya kuamua chochote kwenye hii serikali. Na mimi naona jk akizidiwa kidogo tu zaidi ya hapa atakabidhi hii nchi ya kusadikika kwa jeshi.
 
Hivi kwa wabunge wote 300 na kitu hivi ni jumla ya TSH 300Mil!!!!!!!!!!! CCM na Serikali yake wana pesa za mchezo sana, Si wakalipe malimbikizo ya waalimu na madaktari au wakawachangie wanafunzi wa elimu ya Juu.
 
kama ni kweli hizo pesa walipewa na bunge na chadema wamewaamuru wabunge wao kurudisha hizo pesa basi nitaamini kua cdm si mchezo wana uchungu na hela ya walalahoi kama vile ni hela za kwao wenyewe...daah hawa jamaa ni noma... mbona ccm wamekaa kimya wabunge wa ccm hawaoni hata aibu??
 
Huu ulikuwa ni mtego kama ule wa posho mara mbili ili baada ya kuzitumia itumike kama propaganda ya kuimaliza CDM kuwa inatumia kodi ya watanzania kwa kazi ambazo ni wajibu wao, hongera tena Zitto.
 
430005_368355079849768_100000258363304_1344855_900140523_n.jpg
 
Wanafunzi wanakaa chini, wengi wako nyumbani kwa kukosa ada kuanzia sekondari hadi vyuoni alafu wanagawa mil mona kila mmona! Kwani hawawajibiki kwenye majimbo hadi walipwe? Assnte sana Mh Zitto kwa kutufungua macho na hilo. Ubsrikiwe.
 
kazi ipo!
wabunge sijui miatatu na ngapi mara milioni moja!! vijichenji ambavyo vingeliweza alau kutosha kujenga kijizahanati na kijishule cha chekechea watoto wetu wakapata chanjo za polio na kuchangamsha akili zinatapanywa!
ama kweli kufa kwa mdomo mate kutawanyika!
nchi imeoza imebakiza kunuka tu
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom