Zitto,
Utaandikaje sera kama hujui mikataba mliyo nayo ina kasoro gani? Katika tume ya Bomani kwa nini hamkupendekeza mikataba ibadilishwe? Kuna uoga gani Tanzania kubadilisha mikataba wakati hii imeshafanyika Australia na hata Congo baada ya Mobutu kupinduliwa? Unasema anachotaka kufanya profesa Muhongo kimewahi kufanywa huko nyuma lakini haujaona manufaa, na hii ni kwa sababu hamkutoa mapendekezo yeyote ya mabadiliko yafanyike kwenye mikataba. Muache profesa apitie mikataba yake huenda akaja na mapendekezo mapya wakati ninyi mlishindwa kubadilisha mikataba ya madini katika tume ya Bomani. Hata kama mikataba itawekwa wazi, then what? Lakini inaonekana unataka kumkatisha tamaa hata kabla ya zoezi lake kuanza. Give him time, and the benefit of the doubt.
Nadhani mnapata tabu sana kumuelewa Zitto juu ya mapitio ya mikataba. Anasema jambo hilo lishafanyika zaidi ya mara moja na hakuna kilichofanyika kwa hiyo agizo hilo ni marudio ya kilichowahi kufanyika hapo au kwingineko.
Kama kweli lishawahi kufanyika hakuna haja ya kurudia hilo isipokuwa kupitia records na hivyo lile lililokusudiwa kufanyika kutokana na findings hizo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mikataba hiyo inaacha kuwa labelled siri nzito.