Zitto na January, Hongera kuhusu Posho ila nina Ushauri... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto na January, Hongera kuhusu Posho ila nina Ushauri...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Jun 16, 2011.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  What enticed me kuja na topic hii ni kwamba kimsingi nakubaliana na hoja iliyoibulia na Mheshimiwa Zitto na baadae kuungwa mkono na Mheshimiwa January juu ya posho kuwa mzigo kwa taifa, mlipa kodi in particular.

  Nampongeza Zitto kwa kuleta hoja hii na pia nampongeza January kwa kuiunga mkono na kuielezea vizuri katika context ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano ijayo. Kimsingi nakubaliana na hoja hii kwani inalenga kutujengea fiscal discipline. Lakini nina some reservations on how mjadala unavyoendelea pamoja na mikakati inayoelekea kufuatwa.

  Sitazungumzia posho za wabunge na viongozi wa vyama vya siasa bali zile za watumishi wa serikali. Kufuta posho za watumishi wa serikali kiholela holela inaweza kutupelekea hasara zaidi ya faida. The way I see how suala zima linavyo unfold, I don't see it being sustainable na mjadala unapoteza mwelekeo. Pia kama hatutakuwa waangalifu, tunaweza face a collapse ya public sector management system.

  Kwanza lilianza suala la posho za wabunge, baadae likaongezeka la watumishi wa umma na sasa hata vikao vya vyama vya siasa vimeingiliwa. Kimsingi nina wasiwasi na mjadala juu ya posho za watumishi wa serikali, especially baada ya mjadala kuchukua mkondo mpya ambapo posho za watumishi wa serikali, wabunge na wa vyama vya siasa zinachukuliwa kama ni tatizo moja. Hapa kuna tatizo kwani mfumo wa posho hizi haufanani kwahivyo solution zake haziwezi kuwa treated in a ‘one size fits all' fashion.

  Suala la posho za wabunge na za vikao vyama vyama vya siasa ni rahisi kusema hata ukiwa usingizini kwamba zifutwe lakini sio suala la posho za watumishi wa serikali kwani unlike za wabunge (kwa hali yao ya kiuchumi leo hii) na vyama kwa sasa kuwa more of a political issue, suala juu ya posho za watumishi wa serikali is a political, economic and social issue Kwahiyo ufumbuzi wake uzingatie these spheres (political, social, economical) otherwise madhara yake yatakuwa si ya kisiasa tu bali kijamii na kiuchumi. Nitafafanua baadae.

  Tukianza na posho za watumishi wa serikali, hizi zilishika kasi kutokana public sector reform programme in the early 1990s, a very expensive reform ambayo ililenga kutatua tatizo la a ‘near – collapse' of the public service management system. Structural Adjustment Policies (SAPs) zilipelekea wages kwenye civil service kuwa very uncompetitive kiasi cha kuanza kuleta madhara kiufanisi na kiutendaji – in the context of public service delivery. Changes took into account of the political, social and economic dimensions. Ntafafanua baadae.

  Tukija kwenye posho za wabunge – hizi ni waheshimiwa wenyewe wamekuwa wakizipigania ili ziwawezeshe kuwa na ufanisi zaidi katika mazingira yao ya kazi.Uamuzi wa nyongeza haukuhitaji reforms zaidi ya maamuzi ya vikao vya watendaji wachache kupitia ofisi ya chief secretary. Mchakato wake ni tofauti kabisa na ule wa watumishi wa serikali na umekaa kisiasa zaidi.

  Tukija kwenye posho vikao vya vyama vya siasa, hili ni suala la kichama zaidi na maamuzi juu ya posho hizi hayatokani na reforms zozote bali uamuzi wa watendaji wachache wa vyama husika na pia limekaa kisiasa zaidi.

  Lakini inawia vigumu kuelewa kwanini makundi haya matatu ya posho yanachukuliwa kama yapo sawa, is it because the common denominator ni mlipa kodi? Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu, ni makosa kuweka posho zote hizi katika kikapu kimoja kwani logic has it kwamba aina hizi tatu za posho zimepitia michakato tofauti, na tukichanganya maamuzi juu ya hatima zake, tunaweza jikuta katika madhara yasiyotarajiwa – as we might be in a brink of the collapse of the public service management system. Nitafafanua baadae.

  Pengine nianze kwa kujadili theory of employee motivation and then bring the issue into practical experience. There is a general consensus kwamba performance of employees (PUBLIC OR PRIVATE) to a large extent depends on how they are compensated. Kuna counter arguments ambazo zinasema monetary rewards alone sio enough/can't act as a sole motivator for enticing public servants to maintain and improve their performance.

  Such arguments attribute effectiveness of job performance as a function of other factors such as job satisfaction which stems from realization by an employee kwamba he/she is having other needs such as personal fulfillment i.e. self – actualization in ones work that can be fulfilled kupitia ajira. Kuna wengine wana argue pia kwamba mbali ya pay, work environment and supervision also influence performance ya mfanyakazi. Yote haya ni muhimu lakini the bottom line ni kwamba ‘pay' remains an essential element in satisfying basic needs for most employees. And this is particularly important kwa watumishi wa serikali in societies kama Tanzania where poverty is endemic and few people ever reach self-actualization zone.

  I will pay less attention on whether posho is a motivator to productivity ya mtumishi wa serikali or not kwani nadhani it is more useful to address the consequences of low pay on behavior za watumishi wetu and how that might impact utendaji wa kazi pamoja ikiwa ni pamoja na huduma wanazozitoa kwa jamii.

  Reforms za public sector in early 1990s zilitokana kutambua umuhimu wa theory on employee motivation. Given the precipitous decline ya ubora wa huduma za jamii in Tanzania, iligundulika haraka sana kwamba good-pay strongly determines performance, productivity and quality of public services offered, provided that supervision and work environment is right. Structural Adjustment Policies zilipelekea sekta ya utumishi kuwa uncompetitive compared to the private and NGO sectors in terms of recruiting and retaining talent needed to manage public sector.

  Kipindi cha 1975 – 1985 kilishuhudia a sharp decline in real wages za watumishi wa serikali. By 1994, the year that marked the beginning of the reforms in civil service, real average pay in civil service was only slightly more than half of level ya mwaka 1969 (real – meaning wage adjusted to inflation). This level was among the lowest in Sub Saharan Africa (because of mfumo wa awali wa Ujamaa ambapo mishahara iliwekwa chini sana ili kutojenga matabaka katika jamii). It is only after 1994 when we saw substantial improvements on real average pay of civil servants. However, this improvement was misleading.

  In Tanzania, basic salary ya mtumishi wa serikali kwa miaka yote imekuwa behind in terms of uhalisia wa gharama za maisha. Ndio maana hata argument kwamba posho zifutwe na mishahara iongezwe will hardly solve the problem. The rise in civil pay leo hii is partially explained by posho, sio the actual salary; otherwise salaries za watumishi wa serikali bado largely remain at a competitive disadvantage compared to private and NGO sector in terms of attracting, retaining and adequately motivating qualified professional and technical personnel. Ndio maana huduma za jamii bado duni.

  Madhara ya kufuta posho za watumishi wa serikali ambao mishahara yao kwa sasa ni midogo ni nini?
  • Reduced commitment ya watumishi to public service – their commitment is key to poverty alleviation. We faced this problem in early 1990s.
  • Kupungua kwa uwezo wa government to attract, recruit and retain qualified, managerial, professional and technical personnel.
  • Brains drain of current personnel - to self employment, private sector and NGO sector.
  • Reduced efforts (by employees) leading to decline levels of performance & deterioration of services offered by watumishi wa serikali.
  • Undermining of accountability & control mechanism.
  Hizi ndizo sababu kuu kwanini tulijikuta public service management system ina collapse in the late 80s-early 90s. During this period, nilikuwa na umri mdogo lakini nilikuwa na uwezo wa kuelewa matatizo yaliyokuwa yanajitokeza kwani ndugu zangu wengi walikuwa ni watumishi wa umma. Kutokana na ugumu wa maisha, watumishi wa serikali walianza kujiingiza into counter-productive behaviors that did not support production, service delivery and good fiscal management. Pia they engaged into defiant behavior such as time-theft and corruption. Yote ilikuwa ni livelihood strategy kupigana na hali ngumu ya maisha iliyotokana na real wage kuporomoka. Kwa kifupi, haya yalijitokeza na kwa hali ya mjadala wa sasa, yanaweza kujitokeza tena:
  • Work sharing - Prior to civil service reforms, ilikuwa jadi kwa watumishi wa serikali to engage into work-sharing whereby walikuwa wanakubaliana kuachiana kazi kwa zamu, kutoroka au kutofika kabisa kazini ili kwenda kujitafutia riziki;tatizo hili bado lipo ila limepungua sana due to reforms;
  • Cost – Sharing – Rushwa ilizidi kwani ili mwananchi apate huduma, ilikuwa ni muhimu atoe chochote thus pay for service that was already being paid for kupitia kodi yake. Tatizo hili pia bado lipo ila sio kubwa kama miaka ile;
  • Resource sharing – public resources, supplies and equipments were used for personal gain;
  • Revenue sharing – mapato ya serikali mengi yalipotea kwani watumishi wengi walikuwa wanachota mapato. Hili pia bado lipo ila limepungua sana.
  Maswali ya msingi yanabaki, je:
  • How can we remove posho za public officials whose salaries are way below accepted levels and are irregularly paid?
  • How can we get rid of posho hizi without disrupting the already under performing public management system?
  In my view, in most cases than not, posho kwa watumishi wa serikali ni necessary and justified. Tatizo linakuja pale when the allowances are loosely connected to costs incurred & relatively high in relation to basic salary. Posho is meant to be a reimbursement, not an incentive, otherwise it becomes hard to manage. Mfano rahisi, a middle level official wa serikali akienda kwenye semina ya siku tatu tu nje ya Dar-es-salaam anapata kiasi cha posho which is almost one third ya mshahara wake wa mwezi mzima.
  Faida ya kuendelea kuwalipa posho watumishi wa serikali ni nini?
  Nitazitaja chache:
  • The bottom-line remains kwamba civil servants wanahitaji kuhudhuria seminar mbali mbali za kuwaongezea ufanisi e.g. zile za capacity building zinazo develop skills and expertise, ili mradi ziwe na tija; watumishi hawa ambao wengi wao tayari wapo under-paid cannot reasonably be expected kujilipia out of their pockets usafiri, chakula, malazi. Posho zao ni justified and it is part of any fair compensation system that empowers them to fulfill the requirements of their jobs. So given the importance of such seminars, they should be motivated to continue attend such seminars ila zipunguzwe, na ziwe na tija, sio kuzifuta.
  • Public sector has underpaid but qualified staff (especially experience wise); na tusisahau kwamba posho nyingi zinapitia Donor Funded Projects ambazo zinaingia katika bajeti zetu kila mwaka; donors wanatusaidia sana to bring civil servants a considerable amount of income, develop their careers and provide them with further incentives to stay in public service where we urgently need them.
  • Isitoshe, posho hizi zina multiplier effect katika uchumi kwani ndizo zinatufanya tujidai kwamba tuna watumishi wachapa kazi hata kama basic salary zao ni za chini; pia zinachangia ongezeko la pato la Taifa (GDP) kwani personal income adds up to the GDP; pia zinasaidia kupunguza idadi ya watu living under the national poverty line na kwa kiasi kikubwa sana zina circulate humu humu nchini and lots of it is remitted vijijini kusaidia ndugu zao kukabili maisha – most of it hazitoki nje ya nchi.
  Loopholes za kuziba katika posho za watumishi wa serikali
  • Figures za posho kwenye bajeti zinatutisha kwa sababu kiasi kikubwa cha hizi posho ni hewa; tatizo la posho hewa lisitufanye tuje na uamuzi wa kuzifuta kirahisi rahisi. Mzigo wa posho kuwa kubwa unachangiwa sana na presence of fake seminars/workshops, falsified attendance list, inflated entitlements and payments below what is reported and budgeted. Ni muhimu zaidi kuziba mianya hii kuliko kufuta posho hizi. Inakadiriwa kwamba posho katika bajeti yetu ni karibia nusu ya total wage-bill. Ukiangalia haraka haraka inatisha lakini tukiziba mianya ya leakages, gharama itakuwa ndogo na tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kubaki na posho zenye tija kwa mlipa kodi in terms of watumishi kujituma kutoa huduma za kijamii.
  • High ranking officials wa serikali should stop hijacking opportunities za seminars makazini. Mara nyingi wao ndio huchukua nafasi hizo, wanalipwa na mara nyingine they don't even attend, na kwa sababu ni wakubwa, hakuna wa kuwauliza attendance; hizi seminar ni muhimu zaidi kwa lower level civil servants kwani inawapa nafasi to develop their skills, improve their performance thereby improve public service delivery. Na since ni watumishi wa ngazi za chini, ni rahisi kuwafuatilia in terms of attendance.
  Ushauri kwa waheshimiwa wabunge
  Suluhu juu ya tatizo la ubadhirifu wa fedha za umma ipo mikononi mwenu. Ni wazi kwamba moja ya mikakati wa kila mwanasiasa wa leo ni kutafuta sympathy ya mlipa kodi, mwananchi mlalahoi. Lakini tusisahau kwamba suala la posho sio la kisiasa pekee bali kiuchumi na kijamii. Kutoliangalia suala la posho kwa watumishi wa serikali kwa uangalifu by mixing it na posho za wabunge na za vikao vya chama au kulijadili nje ya reforms zilizopelekea uwepo wake inaweza kutuletea madhara kuliko faida nchini.

  Ebu tumweke huyo mwananchi mlipa kodi/maskini in the centre – tumjadili katika mazingira ya posho za watumishi wa serikali.

  Takwimu zinatueleza ya kwamba asilimia 89 ya watanzania karibia milioni 45 wanaishi chini ya dollar 1 kwa siku – sawa na kuishi chini ya shillingi 1,500 kwa siku. Idadi hii inakaribia watanzania milioni 40 kati ya milioni 45 na ushee. Hawa ni watanzania ambao utafiti wa hivi karibuni wa REPOA umeonyesha kwamba hawaoni kama ni tatizo kulipa kodi na ikiwezekana kodi iongezeke ili mradi waone thamani ya kodi yao kupitia huduma bora za kijamii kama vile maji, elimu, umeme, afya na barabara.

  Kwa maana hii, mtanzania hatakuwa na tatizo lolote kama posho za watumishi wa serikali zitaendelea kuwepo huku huduma za kijamii zikizidi kuboreshwa. Hivyo ndivyo jamii za wenzetu waliotutangulia kimaendeleo wanazidi kupaa. Njia kuu ya serikali ya kumhudumia mwananchi huyu na kumpunguzia maumivu ya maisha ni kwa kupitia utekelezaji wa ilani, sera na mikakati ya iliyopo ya maendeleo. Utekelezaji wa miradi yote hii unatokana na kodi anayolipa huyu mwananchi. Ndio maana kila mwaka katika bajeti, ni jukumu la serikali kumhakikishia mwananchi kwamba kodi yake inapangiwa matumizi yatakayomnufaisha.

  Katika miaka ya hivi karibuni utekelezaji huu umekuwa ukipitia Mkakati wa Kutokomeza Umaskini na Kukuza Uchumi Tanzania yani – MKUKUTA, kupitia clusters zake kuu tatu. Kama sikosei, in the previous financial year, MKUKUTA ilitengewa around 5.8 trillion shillings. Zilizopatikana zilikuwa 3.6 trillioni, na kuacha deficit ya kama shillingi trillion 2.3. Sasa kama shortage hii ya trilioni 2.3 ndio inafanya mikakati ya kupunguza umaskini wa walipa kodi kulega lega, posho za watumishi wa serikali zikiondolewa kiholela zitasaidia au zitazidi kuleta matatizo? We suffer from income poverty kuliko chochote, now why make it worse?

  Kwa mtazamo wangu, kuziondoa kama nilivyokwisha ainisha zitatuletea hasara zaidi ya faida katika kumaliza umaskini. Isitoshe, kama tulivyokwisha ona, mwananchi hana tatizo na kulipa kodi au kodi yake kutumika kulipia posho kama watendaji wa serikali watafanya kazi zao kwa ufanisi na kuwaletea maendeleo yanayofanania na thamani ya kodi yao. Tukiweza tatua tatizo la posho hewa na pia kupunguza idadi ya seminars ili zibakie zile zenye tija tu, nina uhakika kabisa gharama za posho katika bajeti zitapungua kwa kiasi kikubwa sana. Tunaweza kabisa kupunguza kiwango hiki kifikie around 25% of the total wage-bill and this level is very reasonable. Kiwango hiki kitaongeza ufanisi wa kazi za watumishi serikalini thereby kuchangia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

  Waheshimiwa wabunge, kuna upotevu mkubwa sana wa fedha kila mwaka, kiwango kikubwa sana kuliko posho za watumishi wa serikali. Tukiweza kuziba hizi revenue leakages ambazo nitazielezea punde, tuna uwezo wa kupelekea nchi yetu kuwa ya kiwango cha kati kiuchumi na kimaendeleo ndani ya miaka miaka 15 tu, bila hata ya kuwanyima watumishi wa serikali haki yao ya posho, as long as kiwango cha posho kisizidi 25% of the total wage-bill. Nchi kama India na wengine wengi wanajali sana posho za watumishi wao na hawathubutu kuzifuta bali ziongeza in manageable size kwa sababu wanaelewa umuhimu wake katika public sector management system. Tatizo letu watanzania ni kwamba, kila kitu tunaingiza siasa. Suala la posho kwa watumishi wa serikali is not only a political issue but also economic and social and any interventions have to take into account of these three spheres – social, economical and political.

  Kama tunakubaliana kwamba MKUKUTA ni muhimu katika kutatua umaskini, tukiweza kuminimize posho to about 25% of the total wage bill kuna tatizo gani? Kama tulivyokwisha ona, in the MKUKUTA tupo behind by about shilingi 2.3 trilion. Kwanini wabunge wetu msielekeze nguvu zenu katika the obvious problem – revenue leakeages zilizopo? Kila mwaka we lose trillions of shillings za mapato kupitia a combination of tax exemptions, tax avoidance, low mining loyalties, illicit means and trade mispricing.

  Based on available data, the government is forgoing over 2 trillion shillings a year in tax revenue exemptions and illicit trade means with foreign countries. Hii ina maana tukiamua kuziba revenue leakages kama hizi kwa mwaka mmoja tu, tunaweza kupata fedha za kutosha to fund deficit ya MKUKUTA ya 2.3 trillion shillings. Hii itapunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa mwananchi kuzidi kulipia MKUKUTA kwani mtanzania is already over taxed, na kwa sasa hakuna further room ya kuongeza mapato kwa kumtoza kodi zaidi bila kumwongezea umaskini zaidi. Serikali inahitaji ubunifu mwingine wa mapato lakini tusiende mbali, solution ipo wazi – lets block this revenue leakage, sio kufuta posho za watumishi wetu wa serikali wenye hali duni.
  • According to TRA, ndani ya miezi tisa tu (July 2008 to April 2009), serikali ilipoteza billion 587 shillings just from tax exemptions. In 2008 alone, the government lost 1.8 trillion shillings just from exemptions. Hii ni zaidi ya mara tatu ya bajeti yetu mwaka huu ya elimu au afya.
  • More is lost to mining companies; Tume ya Bomani ilitueleza kwamba in 2006-2007 alone, tulipoteza 40 billion shillings; in 2007-2008 tulipoteza 59 billion shillings as a result of fuel exemptions granted to six major mining companies in Tanzania.
  • Independent auditors also reported tax evasion by mining companies that undervalued their profits whereby we lost 171 billion shillings between 1998 – 2003 only; na cha kusikitisha, suala la kodi sekta ya madini bado limeachwa katika bajeti yetu ya 2011-2011. Mheshimiwa Zitto alilivalia sana njuga ila hatujui tumefikia wapi leo.
  • According to international trade statistics, we lost approximately 54 billion shillings just between 2005 – 2007 due to illicit means and trade mispricing of Tanzania products sold to foreign countries; the figures are just for EU, UK and USA; nchi kubwa kibiashara na Tanzania za China, India na South Africa hapa hazijahesabiwa and we lose trillions huko because of loopholes;
  • We lose billions of shillings kila mwaka from bad contracts in mining, fishing, forestry and tourism.
  • Waheshimiwa wabunge, tujikite less katika kufuta posho za watumishi wa serikali, badala yake tusaidieni kuzijengea mazingira ziwe na tija kwa mlipa kodi. Tusaidieni to strengthen the link between tax payment and public service delivery bila kuvuruga posho za watumishi wa serikali ambao they are already underpaid. Kwani kama tulivyokwisha ona according to a recent study by REPOA, majority of Tanzanians hawana tatizo na kulipa kodi na wapo tayari hata ziongezwe kama wataona faida yake in terms of huduma za kijamii. Tax revenues and services benefits should reciprocate or be connected so as to build trust among tax payers; building trust kupitia kufuta posho za watumishi wa serikali will build trust but not in a sustainable fashion;
  • Wabunge mngetusaidia to enact a legislation that curbs mispricing done by wafanyabiashara wakubwa na pia Multinationals; We should demand transparency and accountability on part of Multinational Companies doing business in Tanzania; companies law ziboreshwe ili ziwabane vizuri juu ya reporting of their finances;
  • Pia tusaidieni to enact laws ambazo hapo baadae zitatusaidia nchi iwe refunded from mispricing and bad contracts zinazofanywa na Multinationals;
  • Vile vile tusadieni kuzibana nchi tajiri ziruhusu mfumo wa automatic flow of information za banking operations of individuals and companies toka nchi tajiri operating in Tanzania. Mfano all interest paid au malipo yote yanayofanywa kwenye bank accounts za individuals and companies zilizopo nje ya Tanzania kutokana na business operations registered kwenye ardhi yetu ya Tanzania ziwekwe wazi kwa serikali yetu na mataifa ya nje ili tujue chetu ni ngapi. Marekani wana mikataba na nchi kadhaa kuripoti haya, kwanini sisi tushindwe? Leo hii ukipata nafasi ya kuziona fedha zinazohamishwa toka Tanzania na matawi ya benki kama citigroup kwenda nje utashangaa. Jiulize, citigroup ina matawi mangapi Tanzania? Hayazidi mawili. Kwanini? Walikuja kukuza banking sector Tanzania au wana lao jambo?
  Tuamke.
   
 2. T

  The Jicho Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mchambuzi,

  Hoja ya kufuta posho za wabunge, watumishi wa serikali na watumishi wengine kama wale wa vyama vya wafanyakazi ni sawa na wala haina madhara kama unavyojaribu kuonesha. Ni kweli mishahara ya watumishi wa serikali ni midogo lakini hii ni strategy ambayo imebuniwa na CCM ili malipo makubwe kwa watumishi wachache yafanywe kwa jina la POSHO na yasilipiwe kodi.

  Tunachotaka sasa ni kufutwa posho na budget hiyo ya posho ihamishiwe kwenye nyongeza ya mishahara. Uzuri wa kufanya malipo yote kwenye mshahara ni kwamba yatakatwa kodi hivyo kuinua mapato ya serikali, pensheni za watumishi husika zitaboreka kitu ambacho ni cha msaada sana kwao wanapostaafu kazi.

  Mwisho, kufutwa kwa posho kutaondoa dysfunctional management set up ndani ya serikali na idara zake kwa kushabikia vikao ili wapate nafasi ya kulipwa posho.
   
 3. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Natumai hamjambo hapa jamvini.

  Nimejaribu kufuatilia kauli nyingi zitolewazo kuhusu hoja ya kufuta posho za sitting allowance.

  Nimeshangazwa na kauli za watoto wa viongoz wawili NAPE NNAUYE na W.J MALECELA ambao wanataka kutuaminisha ya kwamba kufuta posho za vikao ni kuturudisha katika siasa za ujamaa ambazo kimsingi kwa maoni yao ndizo zilizotufanya tuwe maskini na kukimbiwa na wasomi wazawa. Ni J. Makamba na H. Bashe ndio walionikosha kwa kutamka wazi kuwa wanaunga mkono hoja hiyo kwa maslahi ya wananchi
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uchambuzi wako naweza kuulinganisha na maji yanayochemka na kutikisa kijiti kikijigongagonga kwenye kuta tokana na msongo wa maji. Umejigongagonga tu kwa maelezo marefu bila kutoa taswira ya hali halisi ilivyo. Hujachambua kwa nini viongozi wa juu serikalini, bunge wanajipendelea kupata posho hizo na kuwaweka kando watumishi wengine wa ngazi za wachini wanaovuja jasho zaidi kama walimu, wauguzi, idara za ujenzi k.

  Suluhisho futa posho hizo kwa wote na wote waonje chungu ya ugumu wa maisha hapo kiwango kinapofikiriwa kama ni kupandisha mishahara au kuongezewa posho za kujikimu zifikiriwa kwa watumishi wote bila ubaguzi wa kujibangia ziada ya malipo kwa viongozi wa juu tu na hivyo kujenga matabaka ya wazi.
   
 5. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi habari za leo,
  Naona nawe umejikita kwenye kutetea posho kama ilivyo ada.
  Swala hapa CDM wameleta hoja ya kutolewa posho sio tu kwa wabunge bali kwa kila mwajiriwa wa serikali na taasisi zake, Wabunge 300+ posho zao hazifiki 900billioni, kwa hiyo kama uliisoma ile bajeti ya CDM ni kwa wote sio wabunge tu.

  Hoja zako sioni kama zina mashiko, zaidi ya kutetea kambi yako. Kwanini Magamba mnaogopa watu kulipwa mishahara kwa kazi wanazofanya? Hii posho ndio nini? Kila kitu kina historia ila kuna vilivyofanikiwa na vilivyoshindwa. Hakuna kitu posho imeleta zaidi ya uzembe, wizi, na ufujaji wa fedha za umma.

  Rushwa imeongezeka kwa kiwango cha ajabu, na ufisadi umekuwa 2005-2010 kuliko kipindi chochote cha Nchi yetu. Nikiwa ninamatumaini makubwa na wasomi nikijua wewe umesoma tena nchi ambazo hazina posho za kijinga, sijui ni kampuni gani ulikuwa ukaiongoze kwenye zile nchi halafu uanzishe posho za vikao vya kila siku.

  Kama swala ni mshahara tujadili mshahara.

  Kwenye hayo maswali yako nitajie ni ofisi ipi ya serikali haina rushwa kuliko miaka kumi iliyopita,
  Nionyeshe ni ofisi ipi ya serikali leo watu hawatumii mali za umma kwa kujinufaisha. wacha mzaha kijana. Turekebishe uchumi wetu kwa kukubali kula vidonge vichungu.

  Posho zenyewe hazina usawa, kwa nini daktari asipewe posho anapofanya operation? kwanini mwalimu asipewe posho anapofundisha? Mbona balali aliweza kutoa posho za BOT, mara alipoona sio utaratibu wa kazi. Bot kulikuwa na vikao kila siku asubuhi na kila kikao watu walikuwa wanavuta posho wakati wapo kazini come on now.

  Hizi safari za arusha, dodoma kwenye semina za ajabu zitakwisha. Mishahara ipangwe kutokana ujuzi na uzoefu. Hakuna serikali inaendeshwa kama hii ya kwetu, ila sasa simshangai Nape wanamshauri ndio wasomi wa CCM. Nchi imekwisha.
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,802
  Likes Received: 6,312
  Trophy Points: 280
  Hivi hoja ya Zitto/Chadema ni kutaka kufutwa kwa posho za vikao (sitting allowances) pekee au posho zooote kwa ujumla wake - including DSAs kwa mtumishi wa serikali anayekwenda safari ''kikazi'' nje ya eneo lake la kazi au Mbunge anapokuwa Dodoma na Dar es Salaam?

  Tusichanganye mambo.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kwamba suala la posho limetamkwa kwamba ni suala la kitaifa na katika mazingira ya siasa za sasa nchini Tanzania, God knows how this debate will unfold kwani sympathy ya mpiga kura/maskini ndio inatafutwa hapa na wanasiasa, nothing else. Kufuta posho za watumishi wa serikali per se will be the biggest blunder na hao hao walipa kodi wata feel the pinch with the salt, sio wanasiasa. From experience tuliyoona, real wages watumishi wa serikali (meaning adjusted to inflation) have never catched up with uhalisia wa hali ya maisha ya Mtanzania. Sasa suala la kwamba posho zifutwe ila mishahara ipandishwe lina ulakini kiutekelezaji, tena mkubwa sana.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sio kila kitu ni sympathy ya mpiga kura mazee... wher is patriotism in any of CCM members these days??
   
 9. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Can u demonstrate patriotism inayoonyeshwa na opposition ambayo ni tofauti na inayoonyeshwa na baadhi ya wana CCM ambao wana uchungu na nchi hii?
   
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Consultant, ulichokisema hapo juu ni nilichokisema mimi in a over 100 lines. This debate is getting out of hand na itatugharimu sana. Tunachanganya mambo. Posho limekuwa suala la kitaifa, uamuzi juu ya posho za vikao vya ccm, bunge, na watumishi wa serikali sasa ni kikapu kimoja in the name of seeking symphathy from mlipa kodi/mpiga kura.
   
 11. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi,

  Naona umejaa theory nyingi lakini kwa bahati mbaya practical zero. Umeandika vitu vingi ambavyo havina chembe ya ukweli, hivi unaweza kufananisha rushwa inayofanyika leo na ya miaka ya 80? Hizi posho ni mzigo kwa taifa , na kusema ukweli hatuwezi kuendelea kukopa hela kufinance posho! Na huu ujinga wa kumsifia Januari Makamba ambaye amelidanganya bunge, sijui audacity unapata wapi? Viongozi wote wa CCM wamesema posho haziwezi kuguswa na haipo katika mpango wao wa maendeleo.

  Ni kweli serikali inapoteza mabilioni if not trilioni ya shilingi kutokana na serambovu za chama chenu cha CCM. Tatizo ni kuwa kodi ni kubwa sana and that is the reason many people are looking for loopholes to avert from paying taxes. Ni jambo la kushangaza kuona vijana na akili zao timamu wanakunywa kool-aid ya CCM.
   
 12. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Suala hapa sio kutetea bali kupinga au kutopinga. Ulichokisema ni sawa sawa na nilichokieleza katika post yangu kwani if i read you correctly, watumishi wa serikaliw wanastahili good pay ili wawe na ufanisi katika kutoa huduma za kijamii, sasa kama itatokana na posho au kuongezeka kwa viwango vya mishahara, haujafafanua kwa ufasaha how this can be sustainable.
   
 13. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Rufiji, mimi nimsifie January kwa msingi upi, i dont even know the guy, yeye ni mbunge huko, mimi ni mwana ccm mtaani nisie na tofauti na mwananchi anaepigana kuishi over 1 dollar a day. labda tunafanana uanachama wa CCM tu. January, halima mdee, Mnyika, Lissu, kafulila na Zitto ni wabunge ambao wananivutia kihoja. Mbunge wa Mbozi (Chadema) pia katulia.
  Kuhusu suala la theory na practice, tafadhali fanya uchambuzi unieleze wapi unapingana na hoja yangu ili tuweze kuwa na interesting debate kwani unaweza kuwa na hoja nzuri lakini hauzifikishi kileleni. Suala la CCM kuwa na sera mbovu haijibu hoja zangu juu ya kwanini posho za watumishi wa serikali zisifutwe bali zirekebishwe ili ziwe na tija. Isitoshe, inaonekana haujanisoma vizuri kwani mjadala juu ya posho za wabunge na za vikao vya ccm mimi nilitupa huko. Tuzungumzie posho za watumishi wa serikali tafadhali.
   
 14. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,748
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  if you have eyes then you must be there to see... i woudlnt count too many coz there are a few few opposition members, but awareness raised about our natural resources, accountability commitment to deliver (e.g. budgets mbadala) in very limited resources without too much support from the government as patriotic

  being bold in their stand is another example rather than most of your party members saying things in the pubs and zip up whenever they see green color

  i would cite a few more examples but January to me has been positive and i dont how much storm he'd weather

  .... CDM members for examples used peanut to get elected, and CCM members used an average of 100M to win primaries, how nice

  Just take it from me, the disease your party is suffering has nothing to do with you.... Its like AIDS patients dying of cryptoccocal meningitis, we cant blame crypto
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  what a question mkuu, wewe huoni?? just give me time to go through your post (i saved it bro - seven pages in word document)... will chat
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi.

  (1) Unakosea kuwachanganya Januari na Zitto. Wanazungumzia kutokea anga mbili tofauti.

  (2) Mchango wako ni mzuri sana kwa jumla, ila ninadhani tatizo liko kwenye remuneration system yetu. Mtu analipwa kidogo kwa kazi nzuri anayofanya ila eti mapatro yake yajazilwe kwa posho. Hilo ni tatizo ambalo ni lazima tulitatue; kuwe ni mishahara inayotosheleza halafu tuondoe posho zote. Posho pekee za kubakia ziwe ni zile za per diem kwa mtu kufanya kazi nje ya mazingira ya kazi aliyoajiliwa. Mbunge hastahili hata per diem kwa sababu mazingira yake ya kazi ni huko jimboni na bungeni, kwa hiyo perdiem itatokea tu iwapo labda amekwenda nje ya nchi.

  (3) Posho anayoongelea Zitto, ni ile apewayo mtu kwa kufanya kazi aliyoajiliwa kufanya na anapata mshahar. Mbunge kulipwa posho kwa sababu ya kuhudhuria mikutano ya bunge ambayo ndiyo kazi yake ni kosa. Ni kama kumlipa mwalimu posho ya kufundisha darasani wakati hiyo ndiyo kazi aaliyoajiliwa kufanya. Mawaziri kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri ni semehu ya kazi zao na hawatakiwe kulipwa kwa kufanya hivyo.

  kich.
   
 17. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi,

  Unajua unapoandika kitu kaa ukijua ya kuwa watu wengine nao watakisoma na kufanya uchambuzi wao. Januari akusapoti hoja ya Zitto bali alidai ya kuwa hii hoja ni part and parcel ya mpango wa CCM wa miaka mitano wa maendeleo. Kitu cha kushangaza, what he stipulated was contrary to viongozi wake wakina Pinda, Makinda na Lukuvi waliotetea posho za wabunge kwa nguvu zote. Sasa kama suala la posho liko kwenye mpango wa maendeleo wa CCM then kwa nini kunakuwa na mixed messages? Nadhani Januari alikuwa anataka sifa na kukikosha chama chake kinachopoteza mvuto kwa wananchi kila kukicha.

  Forget about other poshos for a minute, nataka nikuulize swali kuhusu posho za wabunge, what is your stand? Do you support them?
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Posho za wabunge ni mzigo, hilo halina ubishi.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Posho za wabunge ni mzigo. Tayari wana mshahara mzuri sana, over 2 million a month, wana tax exemptions nzuri tu, wanapewa fedha kwa ajili ya mfuko wa majimbo, wana diplomatic immunity etc. Nakumbuka miaka ya nyuma in the 1980s wabunge wengi walikuwa wa kweli kwani walikuwa wanaacha kazi zao nyingi za maana ili waende kuwatumikia wananchi. Wabunge wa sasa wengi wao wanafuata maslahi tu. Kwani ni ajabu kuona madaktari wa meno na ugonjwa wa moyo, mabalozi, retired civl servants wakikimbilia ubunge, kulikoni? kwanini miaka ya nyuma hili halikuwepo?
  Kufuta posho wa wabunge ni sahihi in my view, posho zao ni mzigo kwa taifa and Zitto is right. Mimi nilichokuwa nakielezea ni kwamba mjadala alioanzisha zitto is getting out of hand kwani watumishi wa serikali nao posho zao zimengiliwa in a way thats not systematic.
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, nakubaliana na wewe. ila tujiulize, kwanini wehenever tunasikia mishahara ya watumishi wa serikali inapanda, at the end of the day their real wage doesnt reflect uhalisia wa gharama za maisha? kuna nini hapa, ni kwamba fedha hazitoshi? ndio maana until we get the right answer, i support posho as long as zinakuwa na tija.
   
Loading...