Zitto: Mwaka 2015 pato letu lilikuwa USD 1,060, kuingia pato la kati la chini ni 1,090 lengo la nchi ni kufika USD 3,000. Sasa sherehe za nini?

Miaka mitano mishahara imewashinda kuongeza,madeni ya watumishi hawalipi, alafu wanafikiri hii habari ndio eti itawasaidia!

Watu maji hawana, alafu unaenda kuwaambia eti uchumi umekuwa, hivi si wanaweza kukushushia kichapo kama sio kukuzomea?

Ukuaji wa uchumi usio-reflect maisha halisi ya watu ni kupigiana kelele tu.

CCM hawapendi data, wanapenda propaganda.
 
Wacha washereheke, maana kila mtu/ kama una familia ya ya watu 7, inatakiwa kwa siku mlale na sh.6,900/ kila mtu, mala 7, huo ndiyo tafsili ya tulipo kwa sasa.
 
Mimi bhana, sijui lakini kwa kutumia takwimu zile zile za World Bank, narudia narudia tena hapa kwamba kwa takwimu hizo za WB, ni ushahidi tosha kwamba JPM amevuruga uchumi, na hata corrupt JK Government, was far better compared to JPM.

Taarifa hiyo ya Benki ya Dunia inasema kwamba:-
For the current 2021 fiscal year, low-income economies are defined as those with a GNI per capita, calculated using the World Bank Atlas method, of $1,035 or less in 2019; lower middle-income economies are those with a GNI per capita between $1,036 and $4,045;
Kwa maana nyingine, hatimae ndo tumefika kwenye $1036+!!'

Ukiangalia WB Secondary Data, unakutana na hii kitu (GNI per capita by Atlas Method).

per capita.png


Kumbe, 2015 GNI Per Capita by Atlas Method ilikuwa $980. Kwa maana nyingine, kwa miaka 5 mzima, JPM alikuwa anahangaika kuivusha GNI per capita from $980 to $1036... a difference of ONLY $54.

Kinyume chake, GNI Per capita in 2010 ilikuwa kama ifuatavyo:-

per capita 2.png


Utaona hapo, in 2010 GNI per capita ilikuwa $720, na kwa maana nyingine, GNI per capita ilipanda from $720 in 2010 to $980 in 2015! Yaani ilipanda kwa $260, wakati miaka 5 ya JPM imepanda around $54+!

On top of that, mwaka 2005 GNI per capita ilikuwa $500, na kwa maana nyingine, miaka yake 5 ya kwanza, Mzee wa Msoga alipandisha GNI per capita from $500 in 2005 to $720 in 2010... yaani $220 wakati JPM miaka 5 yake ya kwanza inaonesha kapandisha for less than $100.

per capita 3.png


Sio siri tena kwamba, kwa takwimu hizo hapo juu, inathibitisha kwamba Magu ameharibu uchumi!
 
Tanzania Mwaka 2015, wastani wa Pato la kila Mtanzania ilikuwa US $1060. Ili kuingia Uchumi wa kati chini kabisa Pato ni $1090. Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa lengo ni kufika Pato la US $3,000 ifikapo 2025. Hatufikia hata nusu ya lengo. Sherehe za nini ?
Watanzania hawana muda wa kumsikiliz mchawi
 
Zitto tumemzoea ni mtu mwongo sana. Kwa takwimu zilizopo pato la kila Mtanzania limekuwa sana
Limeongeza toka kiasi gani hadi kiasi gani? Nasikia tu ohooo, tumewahi kabla ya muda!! Halafu hata neno uchumi wa kati mdogo, hamuliweki!! Na usije shangaa kurudi tena kulee kwenye nchi masikini, kama sera ya meko ya kukuza population, itazingatiwa.
 
Tanzania Mwaka 2015, wastani wa Pato la kila Mtanzania ilikuwa US $1060. Ili kuingia Uchumi wa kati chini kabisa Pato ni $1090. Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa lengo ni kufika Pato la US $3,000 ifikapo 2025. Hatufikia hata nusu ya lengo. Sherehe za nini?
Zitto hanaga jema!

Ndio maana Bulembo anamsaka kila kona!
 
Back
Top Bottom