Ndiyo nimeibuka kutoka hapa Kurasini kwa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania na maneno ya kichwa cha habari hicho ndiyo maneno nimeambiwa nimweleze Mh. Zitto kupitia njia yeyote ile. Kwa kuwa mimi sina ukaribu naye ila nimegundua kwamba ni mwanachama hai wa JF mimi naufikisha ujumbe huu kwake na kwenu wote .
Mh.Zitto mimi nimefikisha ujumbe tu na wao wanasema wanafunga na kukuombea maisha mema na Mungu atawaumiza maadui wako .
Maaskofu wa Katoliki wanadhani Zitto anasimamia haki za wanyonge na wanasema kwa kuwa Zitto ni mtumishi wa watu na hivyo ni mtumishi ambaye amekuwa annointed na Mungu wana endelea kumuombea afya njema na maisha marefu na wanamtaka aendelee kupambana bila woga ila awe mwadilifu na aseme ukweli bila ya kuchanganya uongo.
Wanaona madai ya Zitto na Slaa ni ya muhimu kwa uchumi wa Nchi, na kama yakipuuzwa basi yana athari kwa uchumi wetu na usalama wa Taifa hili la kondoo wa Mungu .
Wakaniambia, ndugu mwandishi tafadhali mwambie Zitto kwamba mchango wake na msimamo wake sisi watu wa Kanisa tuna uunga mkono. Kwa ushahidi wakaniambia nimweleze Zitto asome gazeti la Kiongozi ambalo ni la Kanisa Katoliki la wiki hii ama iliyopita. Kama unalitaka nenda pale St. Joseph Cathedral utaona maneno ama ujumbe na msimamo wa Kanisa kuhusiana na Kanisa.
Mh.Zitto mimi nimefikisha ujumbe tu na wao wanasema wanafunga na kukuombea maisha mema na Mungu atawaumiza maadui wako .