Zitto Mungu akubariki tuko nawe kwa sala-TEC

mimi nafikiri viongozi wqa dini ndio watu ambo wapo karibu zaidi na wananchi, hivyo ningeona kuwa wao ndio wangekuwa wa kwanza kabisa kuwaambia wananchi na serikali kuwa hapa sio sahihi, hiki sio sahihi.
\kwa sababu hata hao viongozi wa kiserikali wana dini zao na wanakutana na hao viongozi wa dini kwa hiyo wao ndio wanabidi wakemee viongozi waovu
 
Viongozi wetu wa dini wanatatizo moja kubwa sana la "undumilakuwili" au 'unafiki' kwa lugha ya kawaida. Leo wanatoa tamko hili la kukemea kitu fulani, kesho unaona wako kwenye hafla na haohao waliowakemea! Haiingii akilini kila siku hasa za ibada utaona na kusikia mara Rais kaendesha harambe ya kuchangia ujenzi wa kanisa, mara waziri mkuu, mara mkuu wa mkoa.... n.k. Yote hayo wanayafanya wakijua kabisa kuwa hiyo ni 'rushwa ya madaraka'. Haina tofauti na michango ya lazima wanayoichangisha viongozi wa ccm kwa wafanyabiashara kama ule walimsusia Lowassa Arusha.

Kama viongozi wa dini wanataka kweli kukemea uozo ndani ya serikali wayafanye kwa uwazi na vitendo, si kwa kujificha nyuma ya mapazia. Haiingii akilini viongozi wa dini wanaandaa mikutano ya viongozi wa siasa ili waende kutolea matamushi ya kibabe kwa wanaowashutumu(mf. mkutano wa Laiser na JK juzi). Kama wamedhamiria kupambana kuanzia kwa hili la Mh Zitto na Slaa, basi waitishe press conference washutumu hadharani siyo kutuma 'vimemo' huu utakuwa ni woga na unafiki.

Mimi ni mkatoliki, tena mseminari najua kabisa kuwa kanisa katoliki lina nguvu na linaweza kufanya zaidi ya kutuma 'vimemo' na sasa ni wakati wa kuwa huru na kukemea kwa dhati kama wako tayari kusaidia taifa hili.
 
Ni kweli naungana nawe Kalimanzira .Mimi ni Mkatoliki na Mseminary kama wewe lakini nataka kusema kwamba Kanisa katoliki chini ya Pengo halitaweza kusema baya juu ya CCM. Kuna close ties na CCM kwa kuwa Pengo kama mwanadamu ni muumini mzuri wa Mwalimu na kuisema vibaya CCM hawezi so yuko tayari kuona watu wake wanaumia lakini yeye abakie na CCM. Huu ndiyo ukweli na nimesha sema huko nyuma kwamba Kanisa Katoliki linaweza kuleta mabadiliko ya haraka kama linataka . Kanisa halina njaa hata mara moja ila Umimi ndiyo mwingi
 
TUTAFAKARI JUU YA JAMII YETU​



1. Maadili ni ya lazima katika kujenga jamii.

Hatuwezi kuishi katika jamii ya watu bila dira ya kimaadili. Watu wote, hata wale wasiomwamini Mungu wanahitaji dira ya kimaadili ili msimamo wa kimaadili kuongoza jamii yao. Bila hivyo, jamii inakengeuka na kuwa uwanja wa mashindano ambamo wenye kumudu na wenye nguvu wanakuwa na fursa ya kuishi vizuri na wanaobaki wanasakamwa na maisha duni. Jamii ya namna hii inapoteza hulka na wasifu wa kuwa jamii ya wanadamu.

Kwetu sisi tunaomwamini Mungu, tunatambua na kukiri kuwa Mungu aliumba ulimwengu katika mchakato endelevu ambamo kwa kutaka kwake, aliwapa wanadamu nafasi na wajibu wa pekee.

Mungu alimuumba mwanadamu katika sura yake, akamjalia akili, utashi na moyo ili kumwezesha kushiriki katika mchakato huu wa uumbaji na kuifanya dunia iwe mahala pa kiutu, ambamo kila mmoja ana nafasi yake, haki na wajibu wake. Kwa hiyo, hadhi ya utu wa kila mwanadamu na ubora wa jamii nzima ndio msingi mkuu wa mambo ya kijamii na ndio msingi wa kutengeneza sera za kijamii. Kila mwanadamu amekirimiwa sifa ya asili na uwezo wa kutambua nini maana ya kuwa mtu. Sheria ya asili inaongoza dhamiri ya kila mtu na ya jamii.

Uwezo huu ni lazima ujengwe kwa bidii na kufanyiwa tathmini endelevu – kama mtu binafsi na kama jamii. Sehemu moja ya uwepo wetu kibinadamu na kuwa na uwezo wa kuchagua na kufanya maamuzi ni kwamba tunaweza kuchagua mema ama maovu. Hata hivyo kuna jeraha katika tabia ya mwanadamu ambalo ni uwezo wa kufanya maovu.

Upande mmoja kuna hali au uwezo wa kutenda maovu kama mtu binafsi, lakini pia kuna dhambi ya jamii, maovu tunayofanya kama jamii, au kama kikundi ndani ya jamii. Kwa maovu hayo watu binafsi au makundi fulani katika jamii wanakuwa ndio wahanga.

Ndio maana lazima tujifunze kuwa na mwenendo mwema na kukubaliana kushughulikia maisha ya pamoja yanayofuata haki na wajibu ambazo msingi wake ni hadhi ya utu wa kila mmoja. Hizi ndizo tunu au thamani za jumla na mtu hawezi kuondolewa haki na wajibu hizo.

Jamii inaweza kuwa ya kiutu ikiwa tu inaheshimu hadhi ya kibinadamu ya kila mmoja, kujali faida ya jamii nzima, Kumwezesha kila mmoja kuchukua nafasi yake na kujenga kwa mshikamano ubora wa maisha ya wote.

Ili jamii iwe ya kiutu, lazima iishi kwa kuzingatia – Ukweli – Uhuru – Haki – Upendo.


2. Sera za kijamii lazima zionyeshe dira ya kimaadili.

Shughuli zote za kiuchumi na maendeleo ya vitu lazima viwe katika kumhudumia mwanadamu na jamii. Uzalishaji kiuchumi, utajiri, bidhaa za vitu, ugawaji wa faida, kugawana uchangiaji na kubeba majukumu lazima vilenge kumnufaisha mwanadamu na watu wote katika jamii – iwe hapa nchini ama katika upeo wa kimataifa.

Katika msingi huu tunaona kwamba nguvukazi (watu) ni muhimu kuliko mtaji, (vitu), inamaanisha kwamba kujitafutia faida ni halali lakini isiwe kwa gharama ya wengine au kuwanyima wengine haki zao. Ni kwamba kufanya biashara ama kuendesha Taasisi ya Fedha haifai iwe ni shughuli ya kiuchumi tu, ila inapaswa ifungamanishe tunu za kijamii zinazowekwa katika sera zao ambazo zinaheshimu hadhi ya utu wa watu. Mfano; kulipa mshahara unaotosheleza mahitaji muhimu, kurekebisha riba, kuweka bei za bidhaa au mazao zilizo za haki.

Tunaweza kukubali kuwa mfumo wa soko huria una mazuri mengi na unaweza kuwa chombo kizuri katika kutenda haki. Lakini uhuru huo unapaswa kudhibitiwa ili uwe wa kuhakikishia uwiano, hadhi ya utu wa wenye kipato cha chini, maskini na wasio na uwezo.

Serikali, kwa hiyo ina wajibu wa kuingilia kati ili kuyakabili mambo ambayo yanaonyesha matumizi mabaya ya uwezo wa kiuchumi na kuleta uonevu kwa walaji na soko kama tunavyoona sasa katika sekta ya fedha, ya nishati na ya madini na vile vile katika biashara ya fedha kimataifa.


3. Utekelezaji wa masuala mbalimbali katika Tanzania leo

Kuna mambo mengi tunayotakiwa kuyatafakari kwa mtazamo huu wa kimaadili.

a) Tumepoteza uwiano kati ya mtaji na nguvukazi.

Katika zama zetu hizi, mtaji, fedha, faida na ukuaji wa uchumi vimekuwa ndio kipaumbele dhidi ya mambo ya kijamii na mahitaji ya kijamii ya watanzania wengi. Hali ilivyo sasa ni lazima tuache maneno na kuchukua hatua. Suala kama la mshahara toshelezi, huduma ya afya katika mahospitali na ubora wa vifaa na mazingira ya elimu, na karo katika shule za binafsi, gharama ya usafiri, kuchangia elimu ya juu, huduma ya maji safi – haya yote yanahitaji kuangaliwa zaidi.

Yatubidi sasa tuache kusema kwamba hakuna fedha – hili ni suala la utashi wa kisiasa na kutambua vipaumbele kimaadili. Watu sasa wanajisikia vibaya na hivyo hasira inajengeka. Hapa ni lazima tuchukue wajibu wetu.

b) Utamaduni wa bahasha

Hapa hatuhitaji kuzama katika maelezo ya kina, kwani kwa hakika, sote tunaelewa kinachozungumziwa hapa. Malipo ambayo hayako katika mfumo wa kawaida na wa kisheria wa nguvukazi na gharama. Malipo ya namna hii yamekuwa ni mfumo sanjari wa kujipatia kipato. Tatizo hapa ni kwamba mfumo huu ni kwa wale tu ambao wanaweza kuingia katika mfumo wenyewe.

Malipo ya bahasha yanafanyika kimya kimya, bila uwazi na hayapo katika udhibiti, hayatozwi kodi na wala hayana msingi wa kisheria. Haya ni mambo ambayo ni kinyume na maadili, ni matendo maovu. Tunaelewa kuwa kuna malipo halali kama bonasi, motisha kwa ajili ya kuboresha utendaji, malipo ya ziada kwa ajili ya utendaji au utumishi bora, zawadi kwa bidii na ubora wa kazi. Haya ni malipo halali, hayapingani kinyume na maadili.

Kumpatia malipo “bahasha” mtu kwa kuhudhuria mkutano ambao ni sehemu ya kazi yake au kwa mtu unayempelekea ombi lako au mradi wako haya sio sawa, ni makosa. Huu ni mwelekeo unazidi kujijenga katika nyanja nyingi. Hakuna haja ya kuendelea.

Hatari ya kuendeleza “utamaduni wa bahasha” ni kuwapatia wachache fursa ya kipato na kujenga tabaka la matajiri na kuwaacha walio wengi wakiwa na vipato duni na maisha duni.

Katika utamaduni wa bahasha hatari kubwa zaidi ni kwamba inabomoa maadili ya jamii juu ya kazi na uwajibikaji. Halikadhalika fikra ya kujali, kuthamini na kupenda kufanya kazi vinadhoofishwa. Katika msingi wa kimaadili kinachozingatiwa ni ubora wa kazi, thamani au tunu ya mradi na majukumu mtu anayoyabeba. Inamaanisha thamani ya mchango wa mtu anaoutoa kwa njia ya kazi yake. Katika “utamaduni wa bahasha,” haya yote hayazingatiwi.

“Utamaduni wa bahasha” unawajengea watu fikra kwamba haijalishi nini unachofanya, lakini cha msingi ni lazima kuwa mjanja na kutumia mitandao. Na madhara yake ni kushuka kwa maadili, na watu kutojali na kuthamini kazi ya mwanadamu na kutamani furaha ya kufanya kazi ambayo mtu huipata katika maana ya kuwa na hadhi ya utu wa mwanadamu.

Stahili na sifa njema, uwajibikaji, wajibu wa kuhudumia wengine ni tunu ambazo zinafifia na kupotea na badala yake uchoyo na ulafi, tama iliyokithiri ya kupata mali, ufujaji ndizo tabia zinazoshamiri miongoni mwa watu.


c) Takrima

Kwa miaka kadhaa viongozi wa dini wamekuwa wakisema kwamba takrima ni malipo yasiyo halali hasa inapotumika wakati wa uchaguzi. Lakini wagombea, halikadhalika wananchi kwa jumla wamekuwa wakiendelea kufurahia takrima. Ikiwa kweli tunataka kujenga utamaduni wa demokrasia ya kweli na kuiwezesha nchi yetu kunufaika na siasa ya vyama vingi, sasa ndio wakati wa kulifanyia kazi tatizo la takrima kwa makini.

Ukweli ni kwamba kinachotokea wakati wa uchaguzi hakihusiani kabisa na takrima, bali ni biashara kabisa. Wagombea wanawaendea wapiga kura kuwalaghai wawape kura zao, na wapiga kura wanafurahia kupokea fedha au zawadi ndogo ndogo. Ni biashara ya kubadilishana kura – fedha/zawadi za vitu vidogo vidogo.

Lakini lazima kuelewa kuwa uchaguzi katika jamii ya kidemokrasia ni jambo lenye maana kubwa linalochukuliwa na kufanyika kwa makini. Ni jambo linalohusiana na namna taifa litakavyoongozwa, na watu wenye mawazo gani na watajali na kuweka vipaumbele gani na sera zipi – haya yakiwa yamefungamanishwa na aina ya watu wanaoshika uongozi.

Wakati umefika sasa wa kuangalia suala la vyanzo vya fedha za uchaguzi za vyama vya siasa. Vyama vinapata fedha kiasi gani na kutoka wapi? Fedha hizo zinatumikaje? Je, taasisi za umma na za huduma zinahusika vipi? Ni wakati sasa wa kudai uwazi katika mambo haya, haifai yabaki kuwa katika siri kwa kuwa yanahusu maisha ya jamii yetu.

d) Rushwa

Hili ni suala la kimaadili kwanza. Kudhani kwamba Polisi, Mahakama au TAKUKURU ndio vyombo pekee vya uhakika katika kupambana na rushwa – ni kujibu kwa njia rahisi mno. Ukweli ni kwamba rushwa imeshamiri kwa sababu watu wengi wanapenda rushwa na wanafanya vitendo vya rushwa.

Lazima tuanzie hapa na kuanza kampeni ya kujenga upya maadili. Viongozi wa kidini lazima waongoze jitihada hizi. Lakini pamoja na viongozi wa dini kuna mabadiliko pia yanayohitajika katika ngazi itakayohusisha asasi na miundo. Suala zima la upatikanaji wa taarifa na sheria ya usiri katika utumishi wa umma, maandalizi na maamuzi ya mikataba mikubwa – hufanyika katika usiri mkubwa wakishirikishwa watu wachache tu wanaokubalika ni changamoto inayodai kukabiliwa. Kuna pia desturi ambayo imejengeka ambayo ni hatari. Desturi hii ni kuunganisha mambo ya kibiashara na uongozi wa kisiasa. Vile vile kuna kukosekana udhibiti na uchunguzi na pia kunakosekana uwiano katika mgawanyo wa madaraka kati ya mikono mitatu ya Serikali – Dola, Mahakama na Bunge.

Haya sio masuala ya kisiasa au kisheria tu. Haya kwanza kabisa ni masuala ya kimaadili. Lazima tuanzie katika dira tunayoiwekea jamii yetu na kwa vipi jamii yetu inavyoweza kujipanga. Dira hiyo inajengwa katika msingi wa kimaadili wa taifa letu na sheria ya asili kama ulivyoelezwa hapo.

Katiba ni matokeo tu ya dira hiyo, na imeandikwa katika namna ya mkataba wa kijamii. Serikali inayokuwa madarakani sio mtawala wa mkataba huu wa kijamii, bali serikali inakuwa mtumishi wa Katiba na mkataba wa kijamii.



HITIMISHO:

- Kusimama katika ukweli, kuruhusu ukweli ujulikane na uzungumzwe, kutasaidia kupunguza tabia ya kusema uongo, majungu na kuongeza sifa nzuri katika jamii.

- Kuwa na kiburi cha kutotambua na kukubali makosa ni jambo linalovunja mshikamano wa kijamii na kujenga hali ya kutoaminiana.

- Kuishi katika hali ya kukataa ukweli wetu, kutotaka kuona na kutambua ukweli wa tabia yetu kibinafsi na kijamii, kunapunguza au kudhoofisha nguvu ya kimaadili ya jamii na kuizuia marekebisho yanayohitajika katika kushughulikia makosa na madhaifu yetu. Tusiogope kuwaelimisha watu kufanya ukosoaji wenye kuleta mawazo yenye kujenga, na pia kuwatia moyo kushiriki katika maamuzi.

- “Hasira takatifu” ni tunu au fadhila ya kimungu. Mara nyingi tunaona katika vifungu mbalimbali ndani ya Biblia jinsi Mungu akiongea kwa hasira na katika hali ya kukasirishwa na kukerwa anapowaona maskini, wasio na uwezo wakiwa ndio wahanga. Na pia hasira ya Mungu inawaka juu ya watu wanaowatumia wengine vibaya.

Tunahitaji moto huo katika mioyo yetu, tusimame upande wa maskini na kuwatetea na vivyo hivyo kwa wale wasio na fursa, tuweze kukataa rushwa na kuachana na mambo yanayowasababishia watu mateso hata kifo. Tuombe kuwa na hasira hii kila tunapoona mambo mbalimbali yanayodhihirisha kuwa watu hawajaliani.

Tuchukue changamoto hii kama wito na tuitikie kwa kuwajibika na kazi hii. Mungu abariki jitihada zetu.




+Paul Ruzoka
Askofu Mkuu wa Tabora
Mwenyekiti wa Tume Haki na Amani
Baraza la Maaskofu
 
Najiuliza,

Hivi kama LOWASSA angekuwa mkatoliki na sio anglikana tungeona haya?

Hivi kama kanisa liko serious ni vipi waendelee kuwaenzi wafuasi wao ambao ni mafisadi serikalini na uraiani na wanashindwa kuwatenga?

Najiuliza, najiuliza....

Tanzanianjema
 
Ukimaliza kusoma haya ya Mzee Mwanakijiji ni vizuri kupitia makala ya Muhingo Rweyemamu katika RAI la leo ambaye pia anaongelea maadili. Yaani ni kweli kabisa MUHINGO huyuhuyu tumjuaye anaongea kuwa tatizo ni maadili...

Kweli ukombozi wa mtanzania umekosa JEMEDARI MADHUBUTI...

Tanzanianjema
 
Mzee mwanakijiji nimekupata!! shule yako kubwa... Kumbe na wewe ni Mtumishi wa Mungu huko kijijini mkuu! Kimsingi nakubaliana na wewe.. Viongozi wa dini wanatakiwa kuacha uoga na kutoificha nuru wakati dunia ina giza. Wanatakiwa waige mfano wako mtumishi mwenzao.

Lakini pia, kila mtu anayo nafasi ya kujifunza na kubadilikia positively kutokana na mafundisho yanayopatikana toka kwa wenye kuelewa zaidi au kutoka kwenye uzoefu wa hali halisi ya maisha na tabia za watu(experience of everyday realities kama nitakuwa sahihi). Katika kubadilika, hata viongozi wa dini wanayo nafasi hiyo iwapo wamegundua udhaifu wao. Nijuavyo mimi viongozi wa dini wanajua fika wajibu wao kupambana na uovu na uozo wote kwene serikali ili kujenga mazingira mazuri kwa kondoo. nafikiri tatizo kubwa ni UOGA katika sura isiyo sahihi ya uvumilivu!Ninaamini kuwa ni uoga sababu wakiwa kwenye majukwaa ya kidini.. huwa wanatamka madhambi ya mafisadi lakini hawapo tayari kufanya hivyo kwa kutumia njia zitakazofanya walengwa wapate huo ujumbe.

Support (na sala zao)kwa Zitto inaweza kuwa ni dalili njema kuwa wamegundua dhambi yao ya uoga na wameanza kujirudi. Naunga mkono wazo la kufanya mpango viongozi wa dini wapate elimu toka JF. Na pia labda tutumie ule msemo wa Bwana Yesu aliposema "yeye asiye kinyume nasi yu pamoja nasi". Kama ni kweli wanaunga mkono juhudi za Slaa na Zitto basi inawezekana hawako kinyume nasi.
 
green29

.......nafikiri hayo maandishi aliyoyaweka MKJJ ni Tamko la Baraza la Maaskofu wa kikatoliki.......

Tanzanianjema
Lowassa ni KKKT.....hata askofu wake Mkuu wa KKKT alishawatolea uvivu serikali kuwa jamii ya kItanzania inahitaji majibu makini kutokana na shutuma zilizowekwa juu ya serikali.

HAKUNA hata sehemu moja ktk Imani zetu ya kwamba eti tunafundishwa UFISADI, viongozi wetu wa imani wamekuwa wanatufundisha maadili mema siku zote. Na wamekuwa wakikemea UFISADI siku zote kwa waumini wao, kuwasema eti ndumilakuwili nadhani sii uungwana, pengine wenzangu nyie hamuhudhurii ktk nyumba za Ibada...........otherwise nafsi zetu zinatushtaki kwa haya tuyasemayo hapa
 
Nimsahihishe Tanzanianjema pale anaposema kwa nini Kanisa lisiwatenge viongozi wasio na maadili mema. Kanisa haliwatengi wandambi. Kwanza sote ni wadhambi wa aina mbali mbali. Kanisa linafundisha, halihukumu.

Maaskofu wamefanya vema kushutumu uovu. Wanashutumu uovu, lakini hawana budi kuonyesha upendo hata kwa hao waovu. They hate the sin, not the sinner. Lazima Maaskofu waendelee kuonyesha upendo na ushirikiano kwa kondoo wao wote, ikiwa ni pamoja na viongozi, hata viongozi wa CCM.
 
Kanisa haliwatengi wenye dhambi ila linataka mdhambi ajirudi atubu na amrudie Mungu. Huu ni wajibu wa kanisa. Na ni wajibu wa kanisa kukemea na kukataa tabia zote za unyanyasaji na ufisadi wa aina yeyote ndani ya jamii.

Mla rushwa na fisadi anajulikana, kwa matendo yake na maamuzi yake. Inaweza kuwa vigumu kwa Watu kuona rushwa ikitolewa lakini ni rahisi kuona matokeo ya rushwa, sasa hapa ndio inabidi kuwatolea uvivu wala Rushwa.

Ninakubaliana na mtoa hoja kwamba kanisa linakemea maovu hiyo ni kweli kabisa halina ubishi. Ila inabidi kuonyesha moto na matendo na chukizo la maovu, ufisadi, wizi na utendaji mbovu ambao haukubaliki mbele ya macho ya Mungu, tusiwaonee haya wala kuwalinda kwa jinsi yeyote.

Kanisa liwe la kwanza kukataa misaada ya mafisadi, lazima kuwe na kuhojiwa je msaada huu ni fedha halali au ni fedha za damu ya wanyonge?

Kanisa lazima lifuate mifano ya Yesu, Nenda kauze ulivyonavyo ulivyovipata kwa mauti ya wanyonge uwagawie hao masikini kisha tuchangie madirisha ya kanisa.

Wakati umefika wana JF kwenda kushika nyadhifa mbalimbali ili kuleta mabadiliko ya kweli kiuchumi, kwani waliopo madarakani kwa sasa wanaganzi ya kifo.

Ni lazima kizazi hiki kiingie madarakani kabla ya Tanzania yenye neema.
 
kama lowasa katoa sh. laki moja kwa ajili ya kujenga hospitali inayosimamiwa na kanisa, sio msaada kwa kanisa bali kwa wananchi. sasa watakataa kumkomoa nani?

pili,KKKT na askofu wao wamemsifu rais pale Arusha mkasema wanakumbatia ufisadi

RC na maaskofu wao wamebariki kazi ya Zitto dhidi ya serikali ya rais, mkasema ni wanafiki. pia wakikaa kimya, mtasema ni mbumbumbu. je hiki kizazi nikilinganishe na nini?

katiba ileile inayokubana wewe kutotoa maoni ndiyo inayowabana wao. na ni ileile iliyombana Zitto pale bungeni.

Unajua kitu wanachoepuka ni hili, kanisani kwao wanaongoza kondoo zenye itikadi mbalimbali, kuna akina Kilitime wengi, na akina Mwanakijiji wengi. akimshambulia kilitime atapoteza kondoo, hivyo lazima awe mwangalifu, na akimshambulia M/kijiji vilevile.

kanisa sio sehemu ya siasa ambapo mkutano unakuwa na watu wenye itikadi moja. ukifanya vibaya utazomewa kama CCM mbeya, au kupigana mapanga kama KKKT Arumeru.
 
Nadhani Ujumbe huo UPUUZWE, wakitaka siasa wafungue chama! Unataka tuamini hayo ni mamaneno ya wakatoliki!!! Jamani jamani,,, Mashekhe na Maaskofu, Wainjilisti,,, endeleeni kuwapa kondoo chakula cha bwana kabla hata hawajapata... mnaenda kuwapa kuku mchele... jamani jamani tulieni huko kwenye imani!!!!

Si ndiyo ninyi mlituambia JK ni mteule wa Mungu, Je na ZK naye Mteule wa Mungu...

Alafu, naomba kuuliza,,, hivyo ukiwa uanatoa mabomu unakuwa kiongozi Mzuri,,eeehhh... Hivyo Mrema Kiongozi Mzuri, Marehemu Kiongozi Mzuri... Jamani Jamani.,...

Upuuzwe kwa kuwa unatoka kwa Maaskofu wa Katoliki au upuuzwe kwa kuwa aliyeuleta hapa si Askofu na kuwa hajazungumza kwa niaba ya Maaskofu?

Kusema kuwa waendelee tu kuwapa chakula cha Bwana Kondoo ni upotofu kwa kuwa nijuavyo mimi wao inawapasa kusimamia haki na pia haiwafanyi kupoteza haki yao ya kutoa maoni kama Watz wengine ati kwa kuwa tu ni Maaskofu!Huu ndiyo msimamo wa Wanasiasa wa Tz pindi itokeapo viongozi wa dini kupingana nao kimsimamo au kimawazo na hutumia kauliza zao "kama vile JK ni mteule wa Mungu" kuhalalisha uwepo wao kwenye madaraka kwa manufaa yao kisiasa. Nadhani ni vema kuachana na hilo na badala yake Wanasiasa wakubali vyote-lawama na pongezi vinginevyo Wanasiasa wetu ndiyo Wanafiki.

Ni vizuri pia ujue kuwa kwa kutuambia kuwa JK ni mteule wa Mungu si kuwa ni makosa. Biblia inasema kila jambo limewekwa kwa kusudi la Mungu; hata kama ikitokea JK akaja kuwa kiongozi mbaya sana bado haikanushiki kuwa ni Mteule wa Mungu maana ni Mungu aliyemtia mafuta Mfalme Sauli kwa makusudi yake mwenyewe ingawa Sauli alikuwa mfalme mbaya!
 
Hivi jamani IS IT A CRIME FOR RELIGION LEADER to give his views on political issues as a normal Tanzanian? Mi nadhani KILA MWENYE NIA NJEMA na Tanzania anayo haki ya kumpongeza mtu aliyefanya JEMA kwa ajili ya maslahi ya TANZANIA yetu. Ni ni haki ya kila mtu kumkosoa mtu anapokwenda kinyume na MASLAHI ya Watanzania. Kwani ZK ni wa CHADEMA tu au watanzania wote? Hapa inabidi tueleweshane. Hapa tunazungumzia maslahi ya TAIFA sio ya CHADEMA wala Slaa wala ZITO "KABWA" hapa. Tunakaribisj=ha mtu yoyote mwenye nia njema na nchi. TUACHE UBINAFSI BWANA, hapa HAIBIWI TEC wala "SILAHA" wala "KABWA" hapa, TUNAIBIWA WATANZANIA WOTE
 
Maaskofu, hasa wa TEC, wana wafuasi wengi sana Tanzania. Zitto amepata ushindi mkubwa kwa kupongezwa na TEC. He has not won the war yet, but he has won an important battle.

Kama alivyosema mmoja wetu, ni muhimu sana kuwatia moyo Zitto na Slaa. Wanapambana na watu ambao tunafahamu wana uwezo mkubwa wa kufanya maovu ya kutisha, hata ya kuua.

Tunawashukuru Maaskofu kwa tamko lao, na tunawaomba viongozi wengine wa dini watoe tamko la kuwaunga mkono Zitto na Slaa vile vile.
 
Waheshimiwa

chonde chonde!!!!!!

Mmewajadili wachungaji wa kondoo za Bwana vya kutosha. Hata hivyo najua kuna mengi sana ya kuwasema hawa viongozi wetu wa dini.

Lakini kwa upande wangu ambaye nimefanya kazi kwa muda mrefu na kanisa sioni sababu hata kidogo ya kutokufurahia mapinduzi haya makubwa.
Historia ya kanisa Tanzania inaonyesha kuwa viongozi wake hawana ubavu hata siku moja wa kuikosoa serikali. Upo hata wakati niliamini kuwa dunia nzima kanisa ni chombo cha kuhakikisha kuwa serikali inakaa salama madarakani.

Atokeze mkristo leo hapa jamvini aniambie siku ibada imefungwa vingozi wa serikali hawakuombewa kwa majina. Lakini hawajajaribu hata siku moja kuwaombea viongozi wa upinzani kanisani. Nilishaamini kabisa kuwa viongozi hawa wanaogopa kuonekana kuwa wanaipinga serikali. Na huu ndiyo ukweli!!

Sasa waheshimiwa kwa hatua hii kwamba wamefikia kutamka wazi kuwa wanafunga na kumwombea Zitto na Wapambanaji wenzake, mimi nafikiri hii ni hatua muhimu sana ya kufikia kwenye demokrasia ya kweli.

Mkjj nakubaliana na hoja zako. Lakini nakushauri tuwapongeze kwanza kwa hatua hii waliyofikia na kuwataka wasonge mbele zaidi.

Kamende
 
Kamende, wachungaji hawaonekani kwa kupigia kelele kondoo wanaokufa njaa zizini! Wachungaji hutoka na kwenda kuhakikisha kuwa wale waliomuia wanagangwa, waliopotea wanarudishwa kundini, na anapotokea mnyama mkali, basi mchungaji mwema yuko tayari kuutoa uhai wake kulinda kondoo wake.

Haya maneno ya kutoa pongezi kewnye comfort ya vyumba vyenye baridi vya TEC au kwenye mimbari iliyoinuliwa juu ni nzuri na ya kuungwa mkono. Lakini binafsi nitaguswa pale wao watakapoanza badala ya kusubiri wengine waanze ndio wao wadandie.
 
Hawa hawa ambao Waziri Mkuu alipokuwa anafungua Kliniki kule Mwanza aliwaambia kuwa kwa wao kuleta huduma za jamii "wanasaidia kutekeleza Ilani ya CCM" na wakakaa na kupiga makofi..?
HAPA MKUU CHUKI IMEISHINDA REASONINGI MZEE NAKUJUA KWA KUCHANGIA MADA MOTOTO KWA HILI UMETOKOTA.
 
Pezzo, ina maana makanisa na misikiti yanapojenga shule yanatekeleza Ilani ya CCM? niko tayari kukosolewa.
 
Pezzo, ina maana makanisa na misikiti yanapojenga shule yanatekeleza Ilani ya CCM? niko tayari kukosolewa.
LOOK HERE SIR, ISSUE HAPA NI MAPAROKO KUMWOMBEA DUWA MPIGANAJI KWELI WOTE HAPA TULIDHANI KWAMBA LABDA SASA TUNA MTU MAKINI, HATA WAO YAWEZEKANA HAWAKUJUA USANII WA AKINA JK ,SASA KAMA JAMAA KADAI HIVYO HADHARANI WAO WASEME NINI WAMUMBUE HADHARANI ONLY TIME HAS TELL THE TRUTH ASASA WANA KUJA NA KUTOA CONCLUSION ZAO KWAMBA ZITO CHOMBO SASA NI MIMI NA WEWE KUSEMA AMINA
 
Back
Top Bottom