Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,322
2,000
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
 

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,329
2,000
My take; Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Mbona kuna jamaa huwa haendi kabisa kwenye misiba, yeye kazi yake kutuma rambi rambi
 

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,188
2,000
Huyu Zito ni msanii! Alikuwa busy tweeter kusambaza habari mbaya kuhusu afya ya mzee wetu Maalim Seif leo ndio anasema aliogopa?

Mtu hadi leo na genge lake wamekuwa kama Radio Tz matangazo ya vifo ndio muoga huyo?

Nashauri familia na serikali impige stop kuanzia leo aache kuuchukulia huo msiba kick ya kisiasa!!!! Marehemu apumzike kwa AMANI!
 

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,188
2,000
Kupokea taarifa na kwenda msibani ni vitu viwili tofauti bwashee!
My take; Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Mbona kuna jamaa huwa haendi kabisa kwenye misiba, yeye kazi yake kutuma rambi rambi
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,214
2,000
Kiongozi ambaye hasikilizi wasaidizi
Kutopokea sim ya msaidizi wa maalim seif ni dharau. Sijui kama za wasaidizi wengine na wananchi zinapokelewa
Haikuwa daharau mkuu kutokana na hal aliyokuwa nayo maalim lazma hofu ingemjaa

Sorry kwa mfano huu umeenda nyumban umekuta hal ya mama yako n mbaya au umepigiwa simu kuwa mzee yupo hoi hospital na mmetuma pesa za matibabu au ana bima kubwa baada ya muda mfupi unakuta missed call nyingi au unapigiwa sana lazma uchanganyikiwe kidogo kwakuwa utajua lolote limetokea huko kutokana na hal uliyomuona au muacha nayo mzee/mama

Itakubid uvute pumz ujiandae kisaikolojia il upokee simu hyo
 

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,688
2,000
Ni tabia mbaya sana ya kutokupokea simu muhimu, ingekuwa mimi ningekatiza hata hotuba na kwenda kuisikiliza hiyo simu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom