Zitto: Mradi wa Kabanga Nickel ni Mradi wa Barrick uliofichwa kupitia kampuni ya LZ Nickel ya Uingereza

Haya mambo ya madini na nguvu ya rushwa iliyosambaratisha mataifa mengi ni hatari kuyajadili kwa mihemuko. Kwa kariba ya JPM , siwezi kununua stori ya ZZK hasa nyakati hizi ambazo kuna kila harufu ya wapigaji kukaa mkao wa kula!

Tunachosahau ni kitu kimoja, ipo siku hakuna jiwe litalosalia juu ya jiwe! Let's wait and see
Kama sio kweli,je,serikali haioni umuhimu wakutoa ufafanuzi?hoja mzito kama hizo unasema huwezi kununua,ndio kawaida yenu kupinga Pinga kila hoja zinazotolewa na wapinzani,Buzwagi 2007,Zitto alipingwa hivi hivi,EPA,Dr. Slaa alipingwa pia,scandal kibao huwa mnapinga
 
Haya mambo ya madini na nguvu ya rushwa iliyosambaratisha mataifa mengi ni hatari kuyajadili kwa mihemuko. Kwa kariba ya JPM , siwezi kununua stori ya ZZK hasa nyakati hizi ambazo kuna kila harufu ya wapigaji kukaa mkao wa kula!

Tunachosahau ni kitu kimoja, ipo siku hakuna jiwe litalosalia juu ya jiwe! Let's wait and see
Nilifikiri watu wenye akili wameisha JF nimefurahi kujua kuwa bado mpo
 
Zitto hivi Barrick wakikuandikia demand note ukathibitishe madai yako mahamani utaweza?

Mambo ambayo huna uhakika nayo ni vizuri ukanyamaza.
 
Kama sio kweli,je,serikali haioni umuhimu wakutoa ufafanuzi?hoja mzito kama hizo unasema huwezi kununua,ndio kawaida yenu kupinga Pinga kila hoja zinazotolewa na wapinzani,Buzwagi 2007,Zitto alipingwa hivi hivi,EPA,Dr. Slaa alipingwa pia,scandal kibao huwa mnapinga
Na miradi ya NSSF mwenyekiti wa PAC alikuwa pinga pinga, na kamati ya Bomani mjumbe mojawapo alikuwa Pinga Pinga
 
Zito Kabwe la yuko kimya kwenye maswala muhimu ya kitaifa kwa sababu yupo pale kimaslahi. Huyu ndiye mvujisha siri zote za Serikali wakati wa JPM kupitia Rais SSH. Joka la kibisa. Ipo siku inawangojea tupo wazima tunawaangalia.
JPM ni hayati keshazikwa, nadhani unatafuta hasira ambazo zitaishia kukuumiza tu nafsini mwako.
 
Mtazamo wangu haya maelezo ni ya kutumwa na ushindani wa kibiashara wa makampuni makubwa.Nia pia ni kushawishi serikali kubadilisha kamati ya akina Kabudi.Haya mambo ya kutumwa yalituathiri sana huko nyuma ikafikia hadi mashaka ya viongozi au kamati ya bunge kula rushwa.
 
Aisee huu upigaji kwenye madini yetu utaisha lini?
Tulifikiri Magufuli kafanya jambo la maana kwenye madini kumbe naye kaingia mkataba usiokuwa na kichwa wala miguu

Changamoto ya waTanzania au Waafrika ni kwamba tunawekeza matumaini yetu kwa individuals baada ya kupambania mifumo bora na ya kudumu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Wanasiasa wanatudanganya na sisi tunakubali kirahisi kwamba watatuondolea matatizo yetu lukuki yanayotukabili huku tukisahau kwamba wanasiasa hao hao ndo chanzo kikubwa cha haya matatizo yetu.

Ukweli ni kwamba kuna mamilion ya watanzania waliwekeza imani na uwezo wao wa kufikiri kwa Magufuli wakiamini kwamba ndo mtu sahihi. Wengine walithubutu hata ku-support uamuzi wa JPM kuvunja katiba, kusigina haki za watu na mengine mabaya, wakiamini kwamba ilikuwa gharama stahiki kuyapata "maendeleo". Lakini ukweli ni kwamba JPM alionekana anafanya kazi kwa sababu kwanza ali-control uhuru wa wananchi kupata habari na kujieleza (JPM alikuwa ni adui wa ukweli). Wananchi wengi walikuwa wanaambiwa yale aliyotaka wayajue au wayasikie. Kiongozi asiyependa ukweli, anayependa giza badala ya nuru si kiongozi mwema. Imagaine mpaka maprofesa wanapewa kazi si kwa ujuzi bali kwa hisani ya kuwatoa jalalani!

Mimi mpaka leo siamini kwamba JPM alikuwa ni kiongozi bora-alikuwa bora kiongozi (alikuwa kiongozi wa kawaida tena wengine walimzidi). Lakini kama mfaidika wa utawala wake, naweza kusema alikuwa kiongozi mzuri kuliko wote waliowahi kutokea-ingawa ukweli wote tunaujua! Maendeleo siyo madaraja au barabara (ni sehemu tuu). Mpaka leo TZ inaheshimika kwa sababu ya misingi ya mwalimu aliyoijenga. Kiufupi Taifa letu mpaka leo tunakula pension ya kazi aliyofanya mwalimu.

Unless tuwekeze kwenye mifumo ya uongozi, hata huyu Mama ataondoka atatuacha mikono mitupu, tutaanza kuimba vigelegele kwa mrithi wake.... Ndo maana ukiongelea swala la katiba utapingwa na kupewa majibu marahisi (Kenya wana katiba mpya mbona wana changamoto za utawala nk). Ukweli ni kwamba watawala wanajua wanachokifanya. Ukitaka kuwatawala watu, wapumbaze, waite wanyonge au wadunishe. Ndo maana mpaka leo "wanyonge" wanamkumbuka JPM. Lakini ukweli ni kwamba, ukishaitwa mnyonge wamekumaliza. Utu wako umedumazwa. Unategemea hisani ya wengine kuiona kesho. Na katika hilo JPM alifanikiwa sana!

Kwa Tanzania sioni tukitoka hapa tulipo kirahisi, kwa sababu juhudi zote za maendeleo zinafanyika kama hisani ya watawala. Na uwajibikaji ni utashi wa mtu mmoja mmoja. CCM imewafanya watu- vijana kwa wazee wawe waoga, wasiojiamini, wanaoamini kwamba uwezo wao wa kuiona kesho au kutengeneza maisha yao wenyewe yapo mikononi mwa watawala.

Aliyoyaandika Zitto si mageni na ni mengi sana ambayo hatuyajui. Na kipindi cha JPM haya yasingejulikana kwa sababu mazingira yaliyokuwepo yalikuwa hayaruhusu haya tuyajue.

Kwangu mimi JPM alikuwa mzalendo na mthubutu, aliyeipenda nchi yake. LAKINI siiombei nchi yangu ije ipate tena kiongozi wa aina yake.
 
Mikataba mipya ya Madini (Frameworks Agreements) itazamwe tena

Na. Zitto Kabwe

Hivi karibuni Waziri wa Madini Dotto Biteko ameainisha uwekezaji wa miradi mipya mikubwa mitatu inayoanza kufanyiwa uwekezaji hapa nchini. Miradi hiyo ni mradi wa dhahabu Nyanzaga wilayani Sengerema mkoani Mwanza, mradi wa Jumbo graphite wilayani Nachingwea mkoani Lindi na mradi wa Kabanga Nickel wilayani Ngara mkoani Kagera. Hii ni miradi mikubwa sana, yenye uwekezaji wa thamani ya dola za kimarekani milioni 942.

Katika orodha hii sikutaja mradi wa rare earth metals, madini ambayo ndio yanaendesha simu za mkononi, kompyuta na magari ya umeme. Mradi huu unafanyika huko mkoani Songwe. Ukijulimsha miradi yote hii pamoja na miradi mingine kiwango cha fedha za uwekezaji kinazidi Dola Bilioni Moja za Marekani. Hii ni hatua inayostahili pongezi nyingi kwa Serikali kwa ujumla lakini pia kwa Waziri wa Madini na watumishi wote wa Wizara hiyo. Vile vile miradi hii inakuwa miradi ya kwanza kufanyika nchini tangu mabadiliko makubwa ya sheria ya madini mwaka 2017, mabadiliko ambayo kwa kiwango kikubwa siyaungi mkono kwani yana madhara makubwa zaidi kwa nchi kuliko sheria ya madini ya mwaka 2010.

Mradi wa Kabanga Nickel una madini ya Cobalt mengi sana na ndio madini yenye thamani kubwa. Cobalt ni sehemu ya madini ambayo pia yanaendesha simu zetu na magari ya umeme na hii ndio sababu kubwa ya Wamarekani na Wachina kugombania DRC ambayo ina 60% ya hifadhi ya Cobalt duniani. Kwa lugha nyingine, haya ni madini Mkakati. Mwenye kudhibiti Cobalt ndio mwenye Dunia kwa miaka 50 ijayo. Tani moja ya Cobalt ilikuwa inauzwa Dola 53,500 za Marekani mwezi Oktoba mwaka 2021.

Tanzania inatarajia kuuza nje tani 3000 za Cobalt kwa mwaka zitakazoingiza zaidi ya Dola za Marekani Milioni 160 kwa mwaka. Kwa upande wa Nickel Tanzania inatarajia kuuza nje Tani 40,000 kwa mwaka zitakazoingiza Dola za Marekani Milioni 700 kama fedha za kigeni. Mradi huu peke yake unaweza kuingiza zaidi ya Dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka kwa miaka karibu 30. Hata hivyo ni mradi wenye mazonge yake kutokana na kugubikwa usiri mkubwa wa namna Mwekezaji alivyopatikana.

Mnamo tarehe 19/01/2021 Serikali yetu iliingia Mkataba na Kampuni ya LZ Nickel ya Uingereza ambayo siku moja baadaye ikabadili jina na kuitwa Kabanga Nickel limited. Wakati huo kampuni ilikuwa na mfanyakazi mmoja na asset za paundi milioni 8 tu lakini Serikali ikawapa mradi uliotafitiwa kwa dola za kimarekani milioni 250, kwa maana hiyo tumewafanyia utafiti bure. Thamani ya fedha zilizowekwa kwenye utafiti zilikuwa nyingi sana kiasi kuugawa mradi ule bure ilishangaza sana.

Siamini kuwa Timu ya Majadiliano ya Serikali iliyoongozwa na Waziri Palamagamba Kabudi ilikuwa haijui ukweli huu. Kama hawakuwa wanajua basi mikataba mingi ambayo timu hii imeingiza nchi kwayo itakuwa ni ya hovyo sana. Muda utasema.

Maswali ya msingi ya kujiuliza ni kwanini hatukufanya zabuni ya wazi ya mradi huu badala ya njia ya maombi ya kawaida ya leseni? Serikali kwa mujibu wa sheria ilichukua leseni zote za miradi iliyokuwa haiendelezwi (retainer licences) jambo ambalo pia lilikuwa hovyo kwani ni sawa na utaifishaji. Kwanini Serikali hiyo hiyo ikaamua kutoa bure mradi ambao umefanyiwa kazi ya mabilioni ya fedha kutumika? Hawa LZ Nickel limited ambao hawapo kwenye soko lolote la hisa duniani walipatikanaje?

Nyaraka zinaonyesha kampuni hiyo ilisajiliwa Mwezi February mwaka 2019, ikaanza mazungumzo na Serikali mwezi Agosti 2020 na kupewa mgodi Mwezi Januari 2021. Hii timu ya Majadiliano ya Serikali chini ya Prof. Kabudi lini iliijua hii kampuni, iliijuaje? Kampuni ilijuaje kuwa Serikali inataka kutoa mashapo haya kwa kampuni nyingine?

Mpaka kufikia wakati kampuni ya LZ/Kabanga inaingia mkataba na serikali, kampuni hii ilikua na shareholders 18. Kampuni ya Lifezone Limited ilikuwa na hisa nyingi zaidi, hisa 100,000 kati ya hisa zote 343,894 sawa na asilimia 29. Katika wanahisa wote hapakuwa na hata mmoja mwenye uzoefu wa uchimbaji wa Nikeli popote duniani.

Nilitumia njia zangu mbalimbali kuwajulisha watu wa Serikali kuhusu makosa makubwa wanafanya lakini hakuna aliyesikia. Prof. Palamagamba Kabudi na timu yake iliyojadiliana na mwekezaji mkataba huu wa LZ/Kabanga Nickel wamefanya dhambi kubwa ambayo huko usoni itakapofahamika wataingia kwenye historia mbaya sana.

Nina taarifa kuwa kampuni hii ni Barrick kwa mgongo wa nyuma. Prof Kabudi na Timu yake waliwapa zawadi kampuni ya Barrick baada ya majadiliano yao kuhusu mgogoro wa Acacia. Tutafafanua zaidi siku za usoni kuhusu hili. Lakini ibakie kuwa Mradi wa Kabanga Nickel ni Mradi wa Barrick uliofichwa kupitia kampuni ya LZ Nickel ya Uingereza.

Ni muhimu sana Serikali iweke wazi wamiliki wote (beneficial owners) wa LZ/Kabanga Nickel. Kuna tatizo kubwa zaidi kwenye mikataba ya uendeshaji ambayo Tanzania inaingia na makampuni haya kwa kinachoitwa Framework Agreements.

Tangu makubaliano ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania ya kuundwa kwa Kampuni ya Twiga Minerals Watanzania tumepokea mambo haya kibubusa bila kufanya tathmini ya kina. Sheria mpya ya Madini inakataza Mikataba ya Madini ambayo tuliita MDAs. Lakini ukitazama kwa jicho la uchambuzi Hizi Frameworks Agrements ni sawa na kurudi kwenye MDAs.

Serikali inatuambia kuwa inamiliki 16% ya hisa kwenye migodi lakini ukisoma hizi framework agreements huu ni uongo kwani umiliki ni kwenye hiyo kampuni ya uendeshaji na sio migodi. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na Kanuni zake ilitaka Migodi mmoja mmoja uorodheshe hisa zake kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam mpaka 35% ya mgodi mzima lakini hizi Framework Agreements za Kabudi na wenzake zinatoa mianya ya wawekezaji kutoorodhesha hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam.

Muhimu kuliko yote ni kuwa Leseni ni ya Mwekezaji sio ya Kampuni Hodhi kwa hiyo hicho kinachoitwa 16% kinakuwa kiini macho tu.

Kwa mfano, Kampuni ya Tembo ambayo ndio ubia wa Serikali ya Tanzania na LZ/Kabanga Nickel haina leseni ya madini ya Nickel. Mwenye Leseni ni LZ/Kabanga Nickel. Mwenye leseni ndio mwenye mali.

Walichotufanya kina Kabudi na Timu yao ya Majadiliano (GNT) ni kutuuzia nyumba ambayo mmiliki wa kiwanja ni mwingine, itakuwa chumba yako hiyo?

Jambo linalonishangaza ni kuwa Serikali mpya ya Rais Samia Suluhu Hassan bado imeendelea kuwatumia kina Kabudi katika mazungumzo ya miradi mingine. Siku Rais akishtuka kuhusu ubovu wa hizi frameworks agreements, nchi yote itakuwa imeshawekwa rehani na kina Prof. Palamagamba Kabudi.

Kinachoitwa GNT kivunjwe na kazi yote ifanywe na Tume ya Madini. Vile vile zinazoitwa Frameworks Agreements zifutwe na kila mwekezaji aingize mtaji wake kwa mujibu wa Sheria. Usiri wa mikataba ya Madini bado ni tatizo kubwa ambalo linaondoa imani ya wananchi kuwa miradi hii ina maana yoyote kwao.

Uchambuzi niliofanya kwenye Uwekezaji wa Mradi wa Kabanga Nickel unaonyesha kuwa bado tunatoa rasilimali za Taifa kama zawadi kwa wanaoitwa wawekezaji. Uchambuzi huo huo unaweza kufanywa kwa makubaliano ya Serikali na Barrick kupitia Twiga Minerals. Hebu tuweke mikataba hii wazi ili Serikali ipate mrejesho kutoka kwa watu na kuboresha zaidi.

Jambo lingine la kufanyiwa tathmini ni maandalizi yetu katika fungamanisho kati ya Sekta ya Madini na Sekta nyingine za uchumi. Kwa mfano mpaka sasa mgodi wa Geita bado unazalisha Umeme wake wenyewe. TANESCO haijafikisha Umeme mgodini na hivyo kutopata Mapato ya dola za kimarekani milioni 3 kila Mwezi (TZS 80 bilioni/Mwaka). Migodi hii 3 mipya na mgodi mwingine wa rare earth metals kule Songwe inahitaji umeme na ndio hatua ya kwanza ya fungamanisho.

Nyanzaga hakuna umeme mkubwa, Kabanga hakuna Umeme mkubwa, Lindi graphite hakuna Umeme mkubwa na wala Songwe, hivyo tunarudi kwenye makosa yaleyale. Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa TANESCO wanafikisha umeme kwenye migodi hii na mingine inayokuja ili kufaidika na uwekezaji.

Pamoja na kumpongeza Waziri wa Madini Bwana Biteko kwa kazi kubwa ya kuwezesha Miradi hii niliyotaja itakayopelekea kuongeza mauzo nje ya Tanzania kwa dola za kimarekani bilioni 6.3 kwa mwaka ndani ya miaka 3 ijayo na kwa miaka takribani 30 ijayo, anapaswa kuanza maandalizi ya FUNGAMANISHO.

Waziri wa Madini afanye kikao na Waziri wa Nishati ili kuhakikisha kuwa migodi yote iliyopo na mipya itatumia umeme wa TANESCO ambao sasa 60% unatokana na Gesi Asilia ya hapa hapa nchini, 25% unatokana na maji hivyo fedha yote itabakia Tanzania.

Afanye hivyo kwa sekta zote. Ni nasaha zangu pia Wizara ya Madini ishughulike moja kwa moja na mikataba ya madini kupitia Tume ya Madini badala ya kinachoitwa Timu ya Majadiliano ya Serikali ambacho ni kichaka chenye madhara makubwa kwa uchumi wa Tanzania na madhara hayo tutayaona siku sio nyingi.

Tanzania haipaswi kufurahia faida za takwimu tu bali Watanzania wanapaswa kufaidika na matunda katika mnyororo mzima wa thamani ili rasilimali zetu zifaidishe watu wetu. Ni aibu kubwa kwamba mpaka leo GGM wanazalisha umeme wenyewe kwa mafuta ya dizeli na hivyo kupeleka fedha nyingi nje. Mikataba ya madini sasa iwekwe wazi kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Hakuna sababu yoyote ile inayozuia mikataba kuwekwa wazi.
===============

Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.
Absolutely brilliant
 
Zito Kabwe yuko kimya kwenye maswala muhimu ya kitaifa kwa sababu yupo pale kimaslahi. Huyu ndiye mvujisha siri zote za Serikali wakati wa JPM kupitia Rais SSH. Joka la kibisa. Ipo siku inawangojea tupo wazima tunawaangalia.
Anazungumzia issue ya madini lakini sio gas. 😂 😂 😂 😂 😂
 
Zito Kabwe yuko kimya kwenye maswala muhimu ya kitaifa kwa sababu yupo pale kimaslahi. Huyu ndiye mvujisha siri zote za Serikali wakati wa JPM kupitia Rais SSH. Joka la kibisa. Ipo siku inawangojea tupo wazima tunawaangalia.
Sioni mbaya kama Zitto alikuwa analikisha Siri za Serikali ya JPM. Ile ilikuwa ni Serikali ya DHULUMA sana, kwa hiyo yeyote aliyechangia kuidhoofisha ni SHUJAA.
 
Kila kona ni kupigwa tuu, gas sio yetu tena na hata dhahabu hakuna tulichopata zaidi ya mashimo, sasa hii nickel watabeba bure inayoonekana, Mkapa alikuwa anaonekana very smart lakini huwezi kuamini jinsi mikataba ya ovyo kabisa ilivyo sainiwa wakati wa utawala wake na JK ndio kabisa kauza sijui kagawa gas yote ambayo ingeweza kutupa umeme nchi nzima kwa mika 100 ijayo, huwezi kuamini vitu vinavyofanywa na hawa viongozi wetu sometimes unafikiri uko ndotoni
 
Zitto na makamba hawafai kuwa marais ila uwaziri ni wazur ,ni bora arudi magu kuliko zitto
 
Ninachojua nikua zito anajua fika kua kizazi hiki ni Cha mazoba, hata akiongea upupu, lazima majority watamwamini.
Sisi wachache tunaoelewa tunashindwa kumdhibiti.
Na Hawa wawekezaji watamwita na kumziba mdomo kwa milioni kadhaa.

Hiyo ndo style yake ya maisha, maisha ya kitapeli. Kiboko yake alikua JPM. Alipauka hatari.
 
Back
Top Bottom