Zitto: Moja ya kampuni ya kusindika tambaku yafungasha virago sababu ya mazingira magumu ya biashara

Awamu ya pili mpaka ya nne walitukanwa sana kwa ‘kucheka cheka na Wawekezaji

Sasa awamu ya tano nayo inatukanwa kwa kutocheka cheka na Wawekezaji


Tatizo ni sie Wapenzi walalamikaji

Wakati ule akina Mkapa wanaweka Tax holiday kuvutia Wawekezaji Walikuwa wanamtukana
 
Watanzania mtembee vifua mbele tuko vizuri sana uchumi wetu unakuwa vizuri sana.

Eh! Mwendawazimu! Mbona umeshalalamika mara nyingi tu ULAIS mgumu sana!? Kwanini usituachie nchi yetu salama salmini ukarudi kwenu Uhutu kufuga mbuzi!?

Ziito Kabwe:

Baada ya Korosho iliyoleta nchini Fedha za Kigeni $512m Mwaka 2017, zao la pili ni Tumbaku iliyoingiza $280m. Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 imeua Korosho Mwaka 2018 na sasa sera zake fyongo zinaua Tumbaku Mwaka 2019.Mwaka 2017 iliua Mbaazi $200m. Wahujumu Uchumi hawa watatumaliza.


Zitto Kabwe:

Moja ya Kampuni yenye kusindika Tumbaku Morogoro imefungasha virago kuondoka Tanzania sababu ya mazingira magumu ya Biashara. Watanzania takribani 3,000 wamepoteza ajira na maelfu kupoteza ajira kwenye mnyororo wa thamani. Wakulima kuathirika zaidi kwa kukosa soko na bei kushuka

Zitto Kabwe:

It is history. Business are closing down and people lose their jobs. This month , a tobacco processing plant has closed down and moved out of Tanzania due to poor business environment putting in danger 500,000 farmers from Tabora, Shinyanga, Kigoma, Mbeya and Ruvuma regions.

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.
 
Aandike na biashara mpya zilizoanzishwa ambazo pia zimeajili maelfu ya Watanzania
N ujinga kuandika negative issues bila kuweka positive issues as well
Ni ujinga mkubwa kuukataa ukweli,yeye kaandika negative issues na wewe andika positive issues tuone.mmezoea propaganda ili hali Mambo ni hovyo! mnataka mseto wa muarobaini na asali?haipo hiyo,pumbavu kabisa
 
Hizo tumbaku tutavuta wenyewe kila mtanzania atapewa kilo 3 na uchumi utakua kwa 35%. tuko vizuri mabeberu tutawakomesha
 
Aandike na biashara mpya zilizoanzishwa ambazo pia zimeajili maelfu ya Watanzania
N ujinga kuandika negative issues bila kuweka positive issues as well
Yeye ameandika negative sasa wewe andika positive ili tuthibitishe ujinga wa Zito
 
Mungu hawezi kuhusika na tumbaku, ainue mkono kwenye mambo mengine sio tumbaku yenye madhara kiafya na faida kiuchumi..kuna mazao mengi yasiyoathiri watumiaji yatafutiwe soko na mbinu bora...
Wamebaki kukimbizana na Vitambulisho vya Machinga...hakika akili za Vifutu ni za makalioni..

Mungu na ainue mkono wake...kulinusuru Taifa...

Toka matamanio ya kuwa Nchi ya Viwanda mpaka Nchi ya kutegemea Machinga...

Jiwe limeweka Historia ya ajabu kupata kutokea Ulimwenguni...
 
Mafisadi na wakwepa kodi acha waondoke watakuja wengine au titafanyabiashara wenyewe!!
Kiwanda cha tumbaku imekuwa ma miaka tangu labda hujazaliwa miaka leo ndo wamekuwa mafisadi?ukiwapoteza hao ,unauhakika gani wengine watapatikana?kwann usitengeneze mazingira rafiki mtaji ulikuwepo unazunguka kutoa ajira,kulipa kodi,na kusaidia wakulima kupata soko unawaona mabeberu na mafiaadi?lugja hiyo si uungwana
 
kama ni Alliance one hii kampuni bora ilivyofungwa maana ilikua haina faida kwa faida hii zaidi ya kuwanyonya wafanyakazi wake kwa ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi..Hii kampuni nakumbuka ilianzishwa around 1998 pale kingorwila morogoro ikiitwa Dimon lakini kutokana na sera mbovu za nchi hii kwamba kampuni inatakiwa kulipa kodi miaka kumi baada ya kuanza kufanya kazi mnamo 2008 ikabadilishwa jina na kuitwa ALLIANCE ONE..mwaka huu wamebanwa ktk kodi wamejitia kujifanya biashara ngumu...
MAGUFULI BANA HAPOHAPO USIACHIE
Zana Za Kilimo anasemaje kuhusu hili au ndio anacho unga mkono?
 
Back
Top Bottom