Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo; Spika Makinda akiri, amtaka Mkulo arekebishe

Hongera Chadema kweli mnastahili kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni na chama kikuu cha upinzani.
sikubaliani na wewe kabisa , hawa inabidi wapewe nchi waongeze . wana kila sababu na uwezo wa kuiongoza
 
this is serious! na makampuni ya auditing nayo wanakaa na kusema eti bajeti nzuri! hii nchi sijui ina shida gani!wasomi hawawezi kuikomboa,sijui tukimbilie wapi?
 
Kobello, Kobello!

Usituaminishe mawazo yako kuwa ndo uhalisia wa mambo yanavyoenda hapa Tz. Huyo mtaalamu mmoja wa IT aliyepewa 15m kama posho tu hawezi kubeba uhalisia wa malipo kwa watendaji wengine hasa wa serikali za mitaa inawezekana ana mjomba hapo ama aina yoyote ya upendeleo anapofanyia kazi.

Mimi binafsi ni mtumishi wa serikali lkn mara ya mwisho kupata malipo ya allowance ni mwaka jana mwezi juni hata kujaza fomu ya posho nimeshasahau. Ukweli tunaitaji mabadiliko ktk nchi yetu.
 
1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali,mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

3. Kuhusu posho, ni wajibu wetu watanzania, hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini..... hapatakalika!

4. Jumatano nakuchallenge Zitto, usome bajeti itakayoonyesha vyanzo mbadala vya kodi na makato ya matumizi, ili elimu iwe bure!...cos you promised this in your campaigns na ilani ya CDM, kama haita-include free education huo utakuwa ni uhuni tu! Ninayo video ya Mnyika akielezea what you will do in your first year kwenye utawala kama mngepata ridhaa.

Maneno yako mazuuuriii sana, lakini maneno hayo yenye nyekundu ndio jibu lako tosha. Je, wamepata ridhaa au????
 
Cha kushangaza! wengi wa changiaji humu, wanasifia na kuponda bila mantiki. Ni matatizo tuliyonayo Tanzania. Upinzani haumaanishi hata mema tuyapinge.

Taarifa ya Zitto inaonesha kabisa kuwa ni upinzani usio na mantiki, mpaka kiasi inanishangaza, najiuliza kwa hayo aliyoyaandika, alikuwa labda ametingwa na kazi nyingi sana mpaka akakubali kuandika mambo yanayoitia aibu kambi ya upinzani?

Kutumia nembo za bunge na kuishusha hii taarifa kwenye tovuti ambayo wengi, wa ndani na wa nje, wataiona na kuona makosa ya kipuuzi kabisa kutoka kwa Waziri kivuli wa fedha? Hata namba zinampiga chenga! ni kujivunjia hadhi kwa Zitto. Hivi Zitto na umakini wake wote anaweza kufanya makosa ya kijinga kama niliyoyaainisha katika post yangu hapo juu? Au Regia? Halafu kwa nembo ya Bunge?

Inasikitisha sana, hata kukiwa na kosa moja tu la spelling kwa taarifa muhimu kama hiyo lazima ikemewe sana seuse hiyo yenye makosa mpaka ya sentensi nzima. Ni aibu kwa upinzani na inaonesha jinsi upinzani unavyokurupuka kutafuta makosa mpaka kiasi wao wanajiingiza kwenye makosa makubwa.

Au ndio yule Zitto anaesemwa kuwa yuko pale si kwa ajili ya upinzani na ana agenda zake? Nashindwa kuelewa.

Naomba Zitto au Regia aliyobandika hiyo taarifa, wawaombe radhi wa Tanzania kwa kuwawekea taarifa yenye nia ya kuupotosha umma ya ama kwa makusudi kabisa au kwa uzembe wa kukurupuka.

Na hata baada ya makosa yote hayo, wanazi wa cdm bado wanashangilia tu, inanikumbusha ile habari ya "kufungwa twafungwa lakini chenga twawala". Nawaonea huruma kwa kutoyaona makosa ya viongozi wao.
 
Zitto,

Nakuheshimu sana mdogo wangu.

Nasikitika sana ninapoona, kwa umakini wako wote ulionao, unaaandika kwa kubabaisha na kupotosha. Mimi sijaipitia bajeti yote, lakini hayo ulyoainisha hapo ya ama umefanya makusudi kupotosha katika maandishi yako ya ama hujui namna ya kuandika, hususan ikija kwenye namba.

1. Mstari wa kwanza umeandika "shilingi 537 Bilioni", mstari wa tatu na wa nne ukaandika "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" na "shilingi 325,448,137,000." halafu mstari wa nne ukarudia tena "Shilingi Bilioni 325".

Swali: Kwanini
"shilingi 537 Bilioni" ziwe ni billioni? na kwanini "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" ziwe millioni? na kwa nini "shilingi 325,448,137,000." ziwe si millioni wala billioni? na halafu "Shilingi Bilioni 325" ziwe tena billioni?

2) Unaeleza kuwa:
kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa.

Halafu unasema:
Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011

Swali : Mbona hizo "
shilingi trilioni 11.624" "za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 huoneshi ngapi kati ya hizo zililipa madeni?

3) Swali: Jee, bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 zilikuwa ngapi? mbona huoneshi?

4) Kauli ilikuwa baadhi ya posho zitafutwa na baadhi ya posho zitapunguzwa.

Jee, ni nini kilichozugwa hapo?
.
Na kauli uliyowekea "bold" haihusiani na kufutwa au kupunguzwa kwa posho, kauli hiyo inaongelea "kusamehe" kodi, sasa mdogo wangu Zitto huelewi maana ya kusamehe kodi? Kama huelewi, hiyo kauli inamaanisha zile posho ambazo hazijafutwa na ambazo zimepunguzwa na ambazo hazijapunguzwa, zitasamehewa kodi. Sasa nini unachoona hakiko sawa hapo?

5) Labda ili ueleweke vizuri, ungeweka hizo faini ambazo zitafikia 50,000/= na ambazo zitazidi zaidi ya 50,000 na kufikia 300,000/= Usitupotoshe na usiupoteshe umma kwa kuwaambia kuwa huku hivi huku hivi.

Kwa kukukumbusha tuu, ingawa faini za barabarani tunazijuwa kikawaida ni 20,000/= tuliona hata Chenge alichapwa faini ya 700,000/= kwa makosa hayo hayo ya barabarani. Nimekutajia ya Chenge kwa kuwa ndio kesi maarufu na ni wengi wanayoifahamu. Kwa mantiki hiyo, inabidi ufafanue kwa kina hiyo faini ya 300,000 na ya 50,000. Tafadhali usipotoshe watu.

Hapo hapo, sentensi yako hii haieleweki "kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho". sijui inamaanisha nini?

6) Jee, ulitaka serikali isilipe madeni? na Jee, ulitaka serikali isilipe posho?, kama hutaki serikali ilipe posho, kwanza onyesha mfano kwa kuzikataa posho zako kama mbunge, kwani mojawapo ya wenye posho kubwa katika watumishi wa serikali ni wabunge. Halafu onesha na takwimu za bajeti iliyopita, asilimia ngapi ililipa madeni na asilimia ngapi ililipa posho. Usiandikie mate na wino upo.

7) Tunaisubiri kwa hamu na kama ni nzuri tutaiomba serikali iifate, kwani upinzani ndio kazi yake kuu, kukosoa ili serikali ijirekebishe.

Kwa kusherehesha tu, ningeomba ajibu Zitto mwenyewe kama anavyonukuliwa kuwa ndio muandishi wa taarifa hii, nikimuomba mleta mada Regia Mtema ajibu ntakuwa sikutenda haki kwani yeye inaonesha kuwa ni kipaza sauti tu cha Zitto.

Nadhani hii taarifa ndio ina kusudio la kupotosha wananchi kwa kuandikwa ndivyo sivyo.
Mkuu hizo ulizotaja ni nukuu za bajeti na si Zitto mengine uliyouliza nafikiri Mkuu Zitto atakujibu naamini ila tatizo umehukumu kuwa Zitto amepotosha bila kwanza kuomba ufafanuzi maeneo unayoona tata then ndio uhitimishe.
 
HTML:
2. Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

Mh Zitto hongera kwa maandiko hayo. Mengine nadhani tumeyajadili kule kwenye business forum. Lakini kabla hujaenda bungeni namba mbili hiyo umechemsha. Unataja asilimia za kulipa mkopo kisha una relate na whole budget ya 2010/11 unasahau kuwa ulitakiwa kwenye budget ile usubtract malipo ya madeni pia ndio ulinganishe. Kwa andiko lako inamaana kwamba bajeti iliyopita madeni hayakulipwa. Hapo umechemka. Kiukweli nashangaa hizo facts za real terms hukuzisema kwenye kilimo, elimu na afya. Napo kuna matatizo makubwa sana.
 
Mkuu hizo ulizotaja ni nukuu za bajeti na si Zitto mengine uliyouliza nafikiri Mkuu Zitto atakujibu naamini ila tatizo umehukumu kuwa Zitto amepotosha bila kwanza kuomba ufafanuzi maeneo unayoona tata then ndio uhitimishe.

Nukuu za bajeti? hiyo ni Taarifa iliyoandikwa na Zitto na kupitiwa na kurushwa hapa na Regia. Inashangaza kuona hawa Mawaziri vivuli wanaotegemewa na wafuasi wao wengi sana wawe wazembe kiasi hiki. Wakati vifungu vinasomwa bungeni hata herufi ikikaa upande watu ndio hupatia mwanya wa kuonekana kwenye TV, wanakosoa haraka haraka, sasa leo unanambia nukuu? be real please.
 
Maneno yako mazuuuriii sana, lakini maneno hayo yenye nyekundu ndio jibu lako tosha. Je, wamepata ridhaa au????
Akinisomea hiyo bajeti,nitambana korodani mbunge wangu mpaka aipitishe ya Zitto!....kumbuka,miaka ya 80s mbunge wa temeke masoud ali masoud alitoa shilingi mpaka warioba akaingilia,tukapewa pantoni....it is still possible,hoja zimeleta mapinduzi zaidi ya damu!
 
Huiwelewi hii topic,
Zitto kawakilisha makosa au udanganyifu.....
Mimi sioni cha ajabu kusema bajeti imeongezeka lakini ukilinganisha na dola imepungua....okay,so?Je waongeze SHILINGI trillion mbili? Halafu?
Na kuhusu serikali kuongopea kuwa inawekeza more kwenye nishati,angetoa a comparative analysis....sio kusema not enough
Na kuhusu madeni,kulipa deni ni maendeleo,au wewe ulitaka wasilipe?
Kama umefurahishwa just piga mayowe..PEOPLEZ!!!!!!!
Ila kama unaona bado ni upupu,criticize!......muwekee mbunge wako kiwango cha hekima na utashi unachotegemea kutoka kwake,He is a damn hardworker and he got love for his country,I RESPECT THAT but I think he can do better than this.
Sasa ngoja nikapige box.
umeelewa ndivyo sivyo dola wapi na sh. wapi, Tr 13.525-1.901=11.624 na ya mwaka jana 11.6 ambayo ukiangaia budget frame work ya 10\11 ndio utaona nini anazungumzia Zitto.
Bado nakutaka tena uwe na subira hadi j5 uone a comparative analysis usiwe na haraka.Hivi mradi wa 160MW ndio utatufanya tupige maendeleo?
Kulipa deni ni maendeleo? kama itakuwa deni limezalisha ziada sina shaka, Ukweli ni kwamba hakuna kilichozalishwa ni zile zilizopotea kifisadi
Niweke unapo niweka sizungumzii kwa misingi ya chama ila utaifa, na wala c mwanachama wa chama chochote cha siasa nipo nipo tu.
And that what you think?
 
Kweli CCM wanatutesa hivi dhuruma hii itaisha lini mbona 2015 mbali jamani,kweli MKULO, na serikali yake wanatudanganya sisi,hakika KIKWETA hamalizi mda wake,sisi kweli wakuwanyiwa hivi kama watoto?
 
Nashangaa sana nnapoona hata Zitto ambae ni Waziri kivuli wa Fedha haelewi "strategy" za kuainisha kulipa madeni kwenye bajeti. Kasoma uchumi kweli huyu?
 
umeelewa ndivyo sivyo dola wapi na sh. wapi, Tr 13.525-1.901=11.624 na ya mwaka jana 11.6 ambayo ukiangaia budget frame work ya 10\11 ndio utaona nini anazungumzia Zitto.
Bado nakutaka tena uwe na subira hadi j5 uone a comparative analysis usiwe na haraka.Hivi mradi wa 160MW ndio utatufanya tupige maendeleo?
Kulipa deni ni maendeleo? kama itakuwa deni limezalisha ziada sina shaka, Ukweli ni kwamba hakuna kilichozalishwa ni zile zilizopotea kifisadi
Niweke unapo niweka sizungumzii kwa misingi ya chama ila utaifa, na wala c mwanachama wa chama chochote cha siasa nipo nipo tu.
And that what you think?
hivi mkuu unajua hata ukiongeza trillion 2 baada ya miezi nane takuwa dola ngapi?
Nani kasifia hiyo miradi mbuzi?
 
hili ni tatizo la nchi kuendeshwa kwa kuangalia upepo wa siasa na inaposahau vipaumbele vyake, matokeo yake ni kujikuta inaangukia pua.
hakuna ufanisi kwenye kichwa cha serilkali isiyokuwa na viongozi walio commited.

mwanga huleta mwanga, giza huleta giza.
 
Cha kushangaza! wengi wa changiaji humu, wanasifia na kuponda bila mantiki. Ni matatizo tuliyonayo Tanzania. Upinzani haumaanishi hata mema tuyapinge.

Taarifa ya Zitto inaonesha kabisa kuwa ni upinzani usio na mantiki, mpaka kiasi inanishangaza, najiuliza kwa hayo aliyoyaandika, alikuwa labda ametingwa na kazi nyingi sana mpaka akakubali kuandika mambo yanayoitia aibu kambi ya upinzani?

Kutumia nembo za bunge na kuishusha hii taarifa kwenye tovuti ambayo wengi, wa ndani na wa nje, wataiona na kuona makosa ya kipuuzi kabisa kutoka kwa Waziri kivuli wa fedha? Hata namba zinampiga chenga! ni kujivunjia hadhi kwa Zitto. Hivi Zitto na umakini wake wote anaweza kufanya makosa ya kijinga kama niliyoyaainisha katika post yangu hapo juu? Au Regia? Halafu kwa nembo ya Bunge?

Inasikitisha sana, hata kukiwa na kosa moja tu la spelling kwa taarifa muhimu kama hiyo lazima ikemewe sana seuse hiyo yenye makosa mpaka ya sentensi nzima. Ni aibu kwa upinzani na inaonesha jinsi upinzani unavyokurupuka kutafuta makosa mpaka kiasi wao wanajiingiza kwenye makosa makubwa.

Au ndio yule Zitto anaesemwa kuwa yuko pale si kwa ajili ya upinzani na ana agenda zake? Nashindwa kuelewa.

Naomba Zitto au Regia aliyobandika hiyo taarifa, wawaombe radhi wa Tanzania kwa kuwawekea taarifa yenye nia ya kuupotosha umma ya ama kwa makusudi kabisa au kwa uzembe wa kukurupuka.

Na hata baada ya makosa yote hayo, wanazi wa cdm bado wanashangilia tu, inanikumbusha ile habari ya "kufungwa twafungwa lakini chenga twawala". Nawaonea huruma kwa kutoyaona makosa ya viongozi wao.
Wewe use your brain rather than your effort,your future is still in your hands,if this is not my country i could leave but i should fight till the end,hivi huoni ZITTO alicho analyze,kweli wewe GAMBA na unaakili mgando huna huruma na watanzania,haya wasalimu Masaki mwambie na yule mdogo wako aliyepo MAREKANI anayesoma kwa wizi wa kodi za watanzania anarudi Tanzania kuwasalimu maskini wa Tanzania
 
HTML:
2. Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

3. Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (non discretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.
Ukiangalia hizo percentage ni kichekesho kidogo. Yaani 0.9 inakuwa 13% halafu 1.9 inakuwa 14% wakati double. Sijui anasemaje na hapa au ndio ule umakini?

watanzania tuwangoeni hawa ccm hawana uwezo wa kututalawa..waliwakamata viongozi wetu ilikuwafanya wawe busy na kesi, walijua hawataishitukia utumbo wao...jk tuachia nchi yetu huna tena uwezo wa kututawala
 
Back
Top Bottom