Uchaguzi 2020 Zitto: Mgombea atakuwa mmoja kati ya CHADEMA na ACT Wazalendo

Humu naona watu wanarushiana tu majigambo, watanzania wote hawapo JF, wapiga kura hawapo mitandaoni peke yake, afu watanzania ndo wanajua ukweli, huwezi kuwaaminisha watu kuwa hakuna kitu wakati wanaona, hapa kwenye nyuzi mnajazana tu matumaini, nyuzi za kutambiana zimekuwa nyingi, jitahidini kupunguza ushabiki, japo kuongea ni haki ya kila mtu pasipo kuvunja sheria.
Mgombea urais chadema anaamini issue yake ya kupigwa risasi basi anauwezo wa kubeba nchi tayari, watanzania hawapo hivyo, mshaurini mapema abadili upepo maana si muda watu watamuona anatamaa tu ya madaraka na mihemko, wakati JPM atakaposimama jukwaani kusema kajenga barabara madaraja zahanati na kadhalika sijui hao wengine watasema nini. Watanzania hawahitaji porojo za kuseti watu upate kiki
 
Toka mfumo wa vyama vingi uanze, mwaka huu ndo ccm inakwenda kukabiliana na wagombea wa upinzani yaani lissu & mwalimu maana hawana historia ya ukada wa ccm katika maisha ya siasa. Hivyo kama ni kuiondoa basi ni mwaka huu tofauti na hapo hakuna. Kwanza zanzibar kule ACT wako vizuri na watashinda kwa kishindo kikuu maana aliyepitishwa upande wa pili siyo chaguo lao kiuhalisia.
 
Lowassa alikuwa hajui kumwaga sumu kwa kutumia mdomo wake. Lissu anamwaga sumu acha kabisa.Hapo CCM wanatamani wamuue tu.
Hili taifa lina 50+ years toka lipate uhuru watu aina ya lissu na wenzake walikuwepo toka enzi hizo na walishindwa kufanikiwa na agenda zao za hovyo hovyo na mwaka huu 2020 wataisoma namba kisawasawa
 
Watumishi woote wa Tanzania hawaitaki kabisa ccm, wakulima woote Tanzania hawaitaki ccm, wafanya biashara woote Tanzania hawaitaki ccm, machinga woote Tanzania hawaitaki ccm.
Endeleeni kuota
 
Hongereni sana walinzi wetu kwa kuliona hilo maana hata nyinyi mmetokea huku uraiani, kuna baba zenu, mama zenu, shangazi zenu, wadogo zenu na kaka zenu pia
Naona unatoa hongera bila kujua ni nani unaempa.
Kweli hamjakomaa huyo analevo gani
 
Kama nilivyosema muda siyo lrafiki kwa hawa ndugu zetu, wangetaka hivyo wangefanya kabla hata ya kuchukua hizo fomu huko NEC. Sasa kila mtu kesha chukua, je NEC ikiwapitisha wote watafanyaje na sisi mfumo wetu sio kama wa Kenya kuwa mnaweza kufanya Coalition baada ya kukubaliana namna ya kugawana hizo nafasi za ulaji na uongozi? Anyway tusubiri tuone.

Kila kitu kinawezekana iwe baada au kabla, MMOJA kati yao anaweza kuachia ngazi muda wowote akasema anajitoa katika kinyang'anyiro cha urais na kuunganisha nguvu kumpigia kampeni MMOJA.
 
Back
Top Bottom