Zitto: Membe karibu upinzani

Umenikumbusha namna 2015 ulivyokuwa mwaka wangu mgumu kisiasa. Chama nilichokiamini kilisaliti harakati kimiujiza ujiza. Naona zile tikitaka zinajirudia. Acha waendelee kujivuruga.
Mkuu hakukuwa na usaliti wowote ila inatakiwa ufahamu kwenye Vita yoyote unapopambana na mtu mwenye nguvu basi unatumia maadui zake wote.

Nakumbuka Savimbi alipigana na Kagame mwaka 1996 ila alipotaka kumuangusha kabila 1998 aliungana na Savimbi. Same to siasa za Kenya utaona alliance zinabadilika, pia hata Uganda na DRC. Kwahiyo hakuna usaliti wowote bali kama umefuatilia siasa za dunia nzima zipo hivyo kila chaguzi lazima ukusanye allies wakutosha whether una bifu nao au lah otherwise kura zitagawanyika mnakosa wote.

Ndio maana Hata hao CCM licha ya kusema Chadema wanatumika na wazungu ila wote wakijiunga CCM wanapewa ofisi za serikali! Sasa hujiulizi pandikizi akipewa ofisi si ndio atauza nchi?

Ni political strategy tu
 
Nilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani, ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.

Wataanguka vibaya sana kisha membe atapunguzwa nguvu huko kama lowasa, kisha atafukuzwa na mwisho atajiunga na chama cha dovutwa, hapo milango yake itafungwa rasmi.
 
Ningekuwa Membe, Wakati huu ndio ungekuwa Wakati wa kupumzika kisiasa, kwani si rahisi Kwa mtu kama Membe Kwa siasa alixokuwa amefikia halafu Leo arudi chekechea, hizi siasa ndizo zilizowashusha hadhi kina Sumae na wengine,

Lakini Kwa kuwa huenda tena ikawa na siasa zilezile za CCM na ujasusi wake, Membe nenda kama ulivyotumwa na CCM kafanye yako, na temu hii hili bomu likiwalipukia hawa vichwa maji labda watakoma kushobokea vitu vizuri vizuri vilivyotegwa barabarani vikitafuta wajinga wasio ridhika na vyao

2015 nililazimika kukikacha Chama changu pendwa Kwa vitu hivihivi vya kijinga
Mku huwezi kumununia tajiri. Lazima watampokea agombee urais.
 
Ujenzi wa Chama Imara ni kazi inayohitaji uvumilivu, muda wa kutosha, jasho na damu pia, ni kazi inayohitaji kutumia akiri nyingi na Hekima na Neema za Mungu!
Kiwango ambacho kilifikiwa na Chadema, kukakosekana kitu kidogo tu, kung'amua ujasusi wa Chama tawala,

Si kila mti wa tunda utakaoupanda eti uote,ukue na Kisha uyale wewe matunda yake! Kuna kazi zingine ni za mtu kukumbukwa tu Kwa misingi aliyoiweka

Kwa mwenendo huu, natabiri, hiki Chama cha ACT kama kispobadiri namna ya siasa zake, muundo wake kiongozi, hiki ndicho Chama ambacho hakitakaa Kwa muda mrefu kwenye siasa za Taifa la Tanzania
Mkuu unakuza sana nguvu za CCM, mie binafsi nafahamu watu wa System ambao wapo CHADEMA (of course wapo kila taadisi) so haikuhitaji mpka Lowassa aje ndio eti waidadisi CHADEMA hyo ni propaganda.

Lowassa was serious unless useme aliletwa upinzani ili hta CHADEMA ikishinda basi aje Rais moderate kuliko Dr slaa!! Kwahiyo hyo propaganda ya eti mapandikizi sio ya kweli bali wengi wanakuja kusaka madaraka tu sio kazi maalum.

Kuhusu upinzani kutetereka ni vyama vyote tu sababu ya aina za siasa zilizopo ila sio kisa kuna pandikizi sijui, siasa zetu hazipo organized hivyo hadi zihitaji jasusi kuvuruga chama otherwise kina Waitara wangekua wanatoa shutuma hku wana bank statement za mbowe kabisa.

Tusiikuze sana nguvu ya CCM otherwise wasingejitaji kutumia nguvu washinde uchaguzi maana majasusi wangemaliza kila kitu kwa kumframe Mbowe
 
Mkuu hakukuwa na usaliti wowote ila inatakiwa ufahamu kwenye Vita yoyote unapopambana na mtu mwenye nguvu basi unatumia maadui zake wote.

Nakumbuka Savimbi alipigana na Kagame mwaka 1996 ila alipotaka kumuangusha kabila 1998 aliungana na Savimbi. Same to siasa za Kenya utaona alliance zinabadilika, pia hata Uganda na DRC. Kwahiyo hakuna usaliti wowote bali kma umefuatilia siasa za dunia nzima zipo hivyo kila chaguzi lazima ukusanye allies wakutosha whether una bifu nao au lah otherwise kura zitagawanyika mnakosa wote

Ni political strategy tu
Umempa ukweli lazima usahau usikae na kinyongo
 
Zitto Mwaka 2015 alikuwa mtu wa kwanza kumsema Membe juu ya ufisadi wa pesa za LIBYA alipotangaza kugombea kupitia ccm leo anamsafisha! shame.

Membe hawezi kutoboa na uwenda akauzika upinzani zaidi ya fisadi lowassa alivyofanya.
Mwongo wewe
lete ushaidi
 
Membe ni pandikizi kama Lowassa tu,na akienda jukwaani kwny kampeni hataongea vitu konki kama Lowassa alivyofanya 2015.

Chadema asimame Lissu kama kawa na aongee ufisadi wa hawa jamaa wajiitao uzalendo.

Kifupi Membe amekuja kugawa kura za uraisi na akimaliza kazi yake atarudi CCM kama Lowassa alivyofanya.
 
Tushawaambia "Upinzani bara hakuna presidential materials huko"

Na msichokijua ni kwamba,siku hao wanaCCM mnaowakaribisha wakishika dola kupitia vyama vyenu watawafukuzeni nyinyi wenye chama.
 
Membe ni pandikizi kama Lowassa tu,na akienda jukwaani kwny kampeni hataongea vitu konki kama Lowassa alivyofanya 2015.

Chadema asimame Lissu kama kawa na aongee ufisadi wa hawa jamaa wajiitao uzalendo.

Kifupi Membe amekuja kugawa kura za uraisi na akimaliza kazi yake atarudi CCM kama Lowassa alivyofanya.
Lisu angekuwa serious,angesharudi hivi sasa,,inaonekana hana nia ya kugombea.
 
This is well calculated by chadema! Hawana mbavu za kupimana na jpm, wao watamteua lissu ila lisu atajitoa. Watamuunga mkono membe.
Hiki kitu haitatokea hata kidogo kumuunga mkono mgombea wa chama ambacho hata robo ya wanachama wa CHADEMA hakina ni tusi kubwa sana kwa wanachama wa CHADEMA.

Chadema hakitakuwa tayari kujinyonga kizembe namna hiyo.
 
Mku kubali au kataa mwakani chama kikuu cha upinzani ni ACT sio tena Chadema
 
Membe ni pandikizi kama Lowassa tu,na akienda jukwaani kwny kampeni hataongea vitu konki kama Lowassa alivyofanya 2015.

Chadema asimame Lissu kama kawa na aongee ufisadi wa hawa jamaa wajiitao uzalendo.

Kifupi Membe amekuja kugawa kura za uraisi na akimaliza kazi yake atarudi CCM kama Lowassa alivyofanya.
Lowasa hakuwa pandikizi he was real contender the problem is hakuwa anajua anachokitafuta njia aliyopitia ni ngumu na yenye shuruba nyingi sana.

Lowassa alirudi ccm kwa kushindwa kuendana na shuruba za upinzani kama serikali ya awamu ya tano isingezuia shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani Lowassa angekuwa bado yuko CHADEMA
 
Ningekuwa Membe, Wakati huu ndio ungekuwa Wakati wa kupumzika kisiasa, kwani si rahisi Kwa mtu kama Membe Kwa siasa alixokuwa amefikia halafu Leo arudi chekechea, hizi siasa ndizo zilizowashusha hadhi kina Sumae na wengine,

Lakini Kwa kuwa huenda tena ikawa na siasa zilezile za CCM na ujasusi wake, Membe nenda kama ulivyotumwa na CCM kafanye yako, na temu hii hili bomu likiwalipukia hawa vichwa maji labda watakoma kushobokea vitu vizuri vizuri vilivyotegwa barabarani vikitafuta wajinga wasio ridhika na vyao

2015 nililazimika kukikacha Chama changu pendwa Kwa vitu hivihivi vya kijinga

Mkuu mawazo yako ni mazuri sana.

Hata jiwe ana mawazo kama haya haya.

Mkuu tembea kifua mbele una mawazo kama mkuu wa nchi.

Kuwa na mawazo kama jiwe si haba mkuu.

Ama kweli adui yako mwombee njaa au mshauri avune njaa.
 
Hiki kitu haitatokea hata kidogo kumuunga mkono mgombea wa chama ambacho hata robo ya wanachama wa CHADEMA hakina ni tusi kubwa sana kwa wanachama wa CHADEMA.

Chadema hakitakuwa tayari kujinyonga kizembe namna hiyo.
Subiri sasa...
 
😂😂 mzee Lowasa alikubalika vipi?? Wanasiasa sio watu wa kuwaamini.
Sie tumesomea political science,achana na mahitaji ya moyo wako
ACT kuna mtu anaitwa Juma Duni Haji,ameshafanya kazi na chadema,hawezi kumshauri mwenyekiti wake waungane na matapeli
 
Na Mwandishi Wetu, Kilwa

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa Benard Membe kujiunga na upinzani rasmi hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa, Zitto alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge na waziri wa wizara nyeti hapa nchini ana fursa ya kuunganisha Watanzania wenye kiu ya mabadiliko kupitia vyama mbadala vya siasa.

"Ndugu yangu Benard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM. Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko. Ni hatua sahihi.

"Hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala ili kuwapa Watanzania Mabadiliko wanayoyataka," alisema.

Kiongozi huyo wa ACT ambaye yuko katika ziara ya kichama ya mikutano ya ndani Kusini mwa Tanzania, alisema anaelewa mwanasiasa huyo bado anapambana kubaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini muda huu anahitajika zaidi kwenye upinzani.

Membe, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini, alifukuzwa uanachama wake CCM miezi michache iliyopita na hali yake kwa sasa iko kwenye sintofahamu.

Akizungumza na redio moja ya kimataifa hivi karibuni, Membe alisema ingawa kwa sasa bado anaangalia hatma yake ndani ya CCM, upo uwezekano wa kuwania Urais kupitia vyama vingine mbadala.

Lakini, katika mkutano huo wa Kilwa; Kusini mwa Tanzania anakotokea Membe, Zitto alisema historia itamhukumu vibaya mwanasiasa huyo endapo hatafanya uamuzi wa kujiunga na upinzani sasa.

"Mimi najua Membe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu wa vyama mbadala.

"Kama kuna kosa la uhaini basi itakuwa ni kwa Membe kutofanya maamuzi ya kuwatumikia Watanzania nje ya CCM. Ninamsihi kuwa afanye tafakari na kufanya maamuzi sahihi na wananchi," alisema Zitto huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo.

Membe amegeuka kuwa mmoja wa wakosoaji wa utawala wa Rais John Magufuli, akikosoa hadharani mambo anayodhani hayako sawa kiutawala.

Ukosoaji huo umemjengea umashuhuri mkubwa kiasi kwamba sasa anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuweza kuwania Urais wa Tanzania kupitia upinzani ( vyama mbadala) mwezi Oktoba mwaka huu.

Zitto anaendelea na ziara yake ya mikoa ya Kusini.

Mwisho
Magufuli jana alisema wazi kwamba hajamaliza kazi zake, hivyo msitarajie atatoka madarakani kirahisi rahisi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom