Zitto: Manji anakomolewa, sasa anyang'anywa hisa zake za Tigo na Serikali

Na mwandishi wa ujumbe huo aseme wazi kwa nn watawala wanamwandama manji? Ameandika kwamba hisa zake za tigo na pia watawala wanajua kwa nn wanamwandama ebu tueleze izo sabab maana utakuwa unajua..

Wanasiasa watu wa hovyo kweli kweli.

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Kapunguzwa kasi za uchaguzi 2020
Watu wana mbinu chafu wanaona aweza kuwa mbunge au meya kwa kiwango alichonacho
Kumbe watu ni roho mbaya hawamtakii mema
Ujumbe huu umeletwa kwenu na mubashara
 
Tunahitaji serikali ya mipango na maendeleo lakini kwa mwelekeo huu nchi itaangukia pua wafanyabiashara ambao wameajiri zaidi ya watu elfu mbili ambao wanachangia kiasi kikubwa leo hii hawadhaminiki, serikali ya viwanda imeperuka, ajira hakuna, nyongezaa za mishahara kwa wafanyakazi hakuna kila mtu analia shida, maisha bora kwa watanzania sasa umekuwa chungu, tunahitaji mabadiko ya sera na mipango lakini sio kutengeneza vitu vipya ambavyo kwa sasa all chaguo la maisha yetu
 
Kinachonifurahisha awamu hii ni kuona wapinzani wamegeuka kuwa watetezi wa wavunja sheria, wahalifu, wezi na mafisadi. Very interesting.
Hawana namna kosa lao walikubali kupokea mafisadi Na haijalishi fisadi huyo yupo ccm au upinzani nilazima wamtetee zambi ya ufisadi nisawa Na kula nyama ya mtu. Muangalie mboe tulimchukulia kama kioo lakini nae alikua muhujum anakaa ktk jengo tena anafanya biashara lakini kodi halipi mpaka anatupiwa vitu nje, sasa Leo yupo kwenye skendo za madawa ya kulevya. Ngoja tuone mchezo mpaka mwisho.




Sent from my itel it1556 using JamiiForums mobile app
 
Manji hana hisa hata moja tigo, wala serikali haina hisa tigo hata moja .

Uzushi unaosambazwa ni watu tuu wasio Itakia mema Tigo na Tanzania kwa ujumla.

ccm acheni kuchafua serikali ya Magufuli, hata kama mnaisoma namba , mliipenda wenyewe.
 
Umasikini ni mbaya sana maana kila siku utamuona alie nacho kama hakustahili kuwa nacho
Very true hizi chuki ni mbaya sana hakuna siku ambayo chuki imepelekea mtu kufanikiwa au kukawa na matunda mazuri ya chuki. Uchumi utazidi kwa mgumu. Kwa style hii tunazidi kufanya uwekezaji kuwa mgumu sana Tanzania. Kila tusiyemtaka majirani zetu wanamtaka tena na wako tayari kuwasaidia. Matokeo yake ni nini? Watahama na kwenda kuzalisha nje ila bidhaa zao zitakuja tu hapa bei ikiwa juu zaidi na hazina ya fedha za kigeni ikipungua zaidi. Chuki ni miwani ya mbao hauwezi kuona facts
 
Acha kwanza ujumbe ufike vizuri kabisa, hakuna mjinga mwingine atakayekuja kuitukana na kuidhalilisha serikali kwa sababu tu ana vijisenti vyake.
Kuwa na thamani ya zaidi ya USD mil 400 sio vijisent by any scale duniani. Kuna kitu nimetoka kujifunza leo ngoja nishare na wewe hapa uone kwa nini sisi hatuendelei wengine wanaendelea
 
Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe.

Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku.

Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?

Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania.

Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.

Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki. Anyways Kama Mwana Simba, nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote.
ZITTO NI BORA UNYAMAZE MAANA KUNA TAARIFA KUTOKA SHULE ULIYOMALIZA ELIMU YA SEKONDARI INAYOONYESHA YA KUWA ULIFOJI KUINGIA ILI UMALIZIE KIDATO CHA NNE BAADA YA KUFUKUZWA HUKO KIGOMA KWA KUMPIGA MWALIMU, SIKU SIYO NYINGI HABARI HIYO ITARUKA HEWANI KUPITIA MOJA YA MAGAZETI SIRIASI...KUMBE ULIFUKUZWA UKAFANYA MAGENDO KUMALIZIA KIDATO CHA NNE?



NA LISSU AFUNGE MDOMO WAKE, MAANA NA YEYE TUNANGOJA TAARIFA YAKE KUTOKA ARUSHA YA JINSI ALIVYOPNAGA KUMNG'OA MBOWE UENYEKITI, IKUMBUKWE TUNDU LISSU NSIYE ALIEMPA MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO TAARIFA YA KUWA MBOWE ALIPATA SUFURI KIDATO CHA SITA! NA MWENYEKITI HUYO PETER MUSHI YUKO CHADEMA ALIKOHAMIA NA LOWASSA. LISSU ACHA UNAFIKI NA HATA WANASHERIA UNASHIRIKIANA NAO KUMNG'OA MBOWE TUNAWAJUA
 
Wakuu,

Tangu suala la madawa ya kulevya liibuliwa kwa kasi ya ajabu na mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Paul Makonda, muathirika mkuu wa hili suala amekuwa mfanyabiashara mkubwa Yusuph Manji.

Utofauti wa Manji na wahusika wengine unajitokeza katika mambo yafuatayo;

1. Kumfungulia kesi ya kukutwa anatumia madawa ya kulevya. Hili suala linawachanganya sana watu kwani inasemekana kisheria hakuna kifungu kinachosema mtumiaji wa madawa ashitakiwe na kufungwa. Na ndo maana watumiaji kama Chid Benz, TID na Ray C mpaka sasa hakuna alofunguliwa mashitaka. Ina maana hii sheria inamhusu Manji tu?

2. Kuwekwa rumande na kufunguliwa mashitaka kwa kuajiri raia wageni bila vibali vya kazi.

Katika hili suala sina uhakika sheria inasemaje ila najikita zaidi kuangalia wahusika walowahi kukutwa na makosa kama haya na hatua zilizochukuliwa. Mfano, vituo vya habari kama ITV & EATV hata CLOUDS vimewahi kukutwa na tuhuma za kuwa na wafanyakazi wasio na vibali ila inasemekana yalimalizwa kimazungumzo nje ya mahakama. Tumeshudia hivi karibuni makocha wa AZAM FC, SIMBA NA YANGA wakiwa na makosa hayo hayo na yalimalizwa nje ya mahakama.

Inasemekana kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha DANGOTE cha saruji hawakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini ila sikuwahi sikia wamefikishwa mahakamani na nadhani lilimalizwa nje ya mahakama. Iweje hili la MANJI liitiwe wanahabari na lipelekwe mahakamani? Utaratibu wa kumalizana nje ya mahakama haumhusu manji?

3. Tigo na kufunga account zote anazomiliki MANJI zilizo chini ya QUALITY GROUP LIMITED.

Kwa mujibu wa mbunge Zitto Zubeiry Kabwa ni kuwa hisa za Manji Tigo zimerudishwa serikalini bila kufuata sheria. Zitto anasema sheria ambayo imetumika ilikuwa wazi kutumika katika kuchukua mitambo ya IPTL, lakini haikuwa hivyo imekuwa kwa Manji.

Jamani, tunajua kabisa kuwa Manji ameajiri watu zaidi ya elfu tano ambao anawalipa kwa mwezi. Kufunga kwa account za mtu huyu hamuoni kutaathiri watanzania walioajiriwa na Manji? Wataishi je?

Binafsi namuomba rais wetu mtukufu arudie kuliangalia suala la Manji kwa jicho la tatu. Nahisi Manji atakuwa anahujimiwa na washindani wake kibiashara kwa rais wakiwatumia baadhi ya watendaji wa serikali.

Kwa namna ya kipekee namuomba Rais wetu mstaafu Jakaya M. Kikwete, Mbunge wa Chalinze Ridhwan Kikwete, Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba na wote mnaoweza msaidie kufikisha ujimbe huu kwa Rais wetu .
 
Sasa naelewa kwanini inasemekana Yanga watakwenda Zambia kwa Treni ya TAZARA.
 
Hii itakuwa mwanzo wa ku
Tunachukua chetu,hakuna tatizo lolote.baadhi ya viongozi wa serikali waliopora fedha zetu walitumbukiza kwenye fuko la manji.janja yao kwisha.

Mzito kabwela pesa yetu kule Nssf umerudisha tukopeshe wengine?
rudisha vyote vilivyochukuwa kutoka kwa umma bila kuafuata taratibu.
 
ZITTO NI BORA UNYAMAZE MAANA KUNA TAARIFA KUTOKA SHULE ULIYOMALIZA ELIMU YA SEKONDARI INAYOONYESHA YA KUWA ULIFOJI KUINGIA ILI UMALIZIE KIDATO CHA NNE BAADA YA KUFUKUZWA HUKO KIGOMA KWA KUMPIGA MWALIMU, SIKU SIYO NYINGI HABARI HIYO ITARUKA HEWANI KUPITIA MOJA YA MAGAZETI SIRIASI...KUMBE ULIFUKUZWA UKAFANYA MAGENDO KUMALIZIA KIDATO CHA NNE?



NA LISSU AFUNGE MDOMO WAKE, MAANA NA YEYE TUNANGOJA TAARIFA YAKE KUTOKA ARUSHA YA JINSI ALIVYOPNAGA KUMNG'OA MBOWE UENYEKITI, IKUMBUKWE TUNDU LISSU NSIYE ALIEMPA MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO TAARIFA YA KUWA MBOWE ALIPATA SUFURI KIDATO CHA SITA! NA MWENYEKITI HUYO PETER MUSHI YUKO CHADEMA ALIKOHAMIA NA LOWASSA. LISSU ACHA UNAFIKI NA HATA WANASHERIA UNASHIRIKIANA NAO KUMNG'OA MBOWE TUNAWAJUA
Tutatoa za watu waliomwandikia thesis ya phd sizonge na alivyoiba mali za mradi wa irp. Zingine ni za

Kukataa wito wa mahakama kuu Tabora kwenye kesi ya Kafumu
Samaki wa Magufuli
Taarifa ya CAG ya bil 230 wizara ya ujenzi
MV DAR
Uteuzi wa hovyo kwenye kazi za serikali kwa kuwapa mabashite kiukabila kiitikadi na udini

Naomba uzitoe zako haraka na sisi tumwage zetu.
 
88 Reactions
Reply
Back
Top Bottom