Zitto, Makamba wautaka urais?

Sioni kama ni tatizo mradi wao wote January, Zitto na Said Bagaile wanapigania maslahi ya Taifa. Acheni majungu

Mkuu, hata jk wakati anaomba kuingia ikulu aliahidi kuipitia upya mikataba ya madini kwa lengo la kuiboresha, hiyo ilionekana kuwa ni maslahi ya taifa, ameshaipitia?
 
Zito anajibagua sana na wana mabadiliko wenzake,tulisha mzoea yule,nafikiri udini unamsumbua sijui kwa nini asirudi ccm

Zito ni mzalendo anaweka maslahi ya taifa lake mbele. Kama hao waliowaalika wamemwalika yeye na akina Januari angefanya nini? Udini kwa Zito hauna nafasi, mbona huwa anamkosoa Rais ambaye ni dini moja na yeye? Kwanini mnapenda "kupalilia" hii mbegu ya udini? Zito pia hajawahi kuwa CCM. ZITO CHAPA KAZI USIOGOPE MAJUNGU KAMA HAYA. Aluta Continuaaaaaaaa
 
Zitto na January wanasimamia kitu kimoja - utaifa - wakiwa na itikadi tofauti, hilo wote wanalitambua. Wakiwa wanashughulikia jambo kwa mstakabali wa taifa tofauti zao wanaziweka pembeni. Mnaomwona kabadilika au ana ajenda ya siri ni sawa sawa na hao wanomwona Mhe. Mbilinyi (Mr. II) kama Ruge B, What a misconception!
 
CDM na CCM wanatofautiana kiitikadi na kisera tu. Na ukaribu wa hawa watu hauzifanyi hizi itikadi na Sera za vyama hivi kubadilika kabisa (isipokuwa pale penye maslahi mapana ya nchi na wananchi kwa ujumla).

Jamani tutoke nje ya box na tuelewe kuwa siasa si uhasama na chuki. Wenzetu wameenda mbali zaidi na kushirikiana na mpinzani wako kwenye Serikali kama wanakubaliana na weledi na utendaji wake. (refer Robert Gate na Serikali ya Rais Obama). Sijui ingekuwa hapa J.K akamteua Dr. Slaa (kama waziri wake) watu wangesemaje

Mbona Mke wa Dr. (wa zamani) alikuwa Diwani wa CCM na mambo yalikuwa yanaenda vizuri? Jaman katika maslah ya Taifa, ruksa kutoka kwenye minyororo ya vyama vyetu. Na hawa vijana wanastahili pongezi kwa kwenda mbele zaidi ya vyama vya Siasa na kuweka maslahi ya taifa mbele (kama ndio lengo lao).

Kuna msemo unasema"huwezi kupata joto kwenye chumba chenye baridi kuliko mwili wako au chenye joto sawa na mwili wako". Hivyo ukitaka Joto zaidi, tafuta chumba chenye Joto zaidi yako
 
Mgheni Amani;

Unachohitaji kusaidiwa wewe ni kufundishwa ama kujuzwa mambo haya Elimu ya Siasa, Elimu ya Uraia, na ya Utaifa; na ufundishwe vile vile tofauti zilizopo kati ya Siasa za Jukwaani, Siasa Ndani ya Bunge na Siasa Nje ya Bunge, na ujue mahusiano ama ushirikiano wa watu binafsi dhidi ya Vyama ama Itikadi zao. Kuna wakati mnaenda beyond limit sasa halafu mnalaumu tuuuuu.......... Alisema Malcom X "I know the essence of brotherhood and I know what it feels like fighting for the right of your people but I'll stand and fight for those who recognise my efforts and those who appreciates it and here I need not applying the sense of brotherhood but the sense of togetherness" sasa kama wengine hawatambui ama wanadharau juhudi zake ana haki naye ya kushirikiana na wale wanaoheshimu juhudi zake hasa katika kutimiza yale yawapasayo katika Taifa hilli....
 
Jamani! Kweli vijana tunahitajika katika kushiriki maamuzi ya mustakabali wa nchi yetu, lakini sio mpaka tuwe marais, tunaweza tukashiriki kwa namna tofauti tofauti. Nafasi ya uraisi yataka Hekima sana ya hali ya juu kuliko hawa ndugu wanavodhani, hebu fikiria hawa jamaa Zito na mwenzake Makamba sina hakika kama hata kuoa wameshaoa, na kujipima hata kiuongozi katika taasisi ndogo tu ya ndoa, then wanataka Urais. Please let them wait until they grow much. Kuna njia nyingi sana za kuisaidia nchi hii kimustakabali na si kwa kuwa Rais, Ikulu si mahali padogo jamani. Nimuulize Zito matatizo ya wanakigoma yameisha? Umeyatatua yote? Makamba je?
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI


Mkuu kwenye itikadi hapo; Zitto na January wana itikadi moja in common: Wote wanapinga posho za vikao ila hao makamanda wengine unaosema hawana nia thabiti ya kuzipinga posho.
 
1. Miaka 16 as a lower bound for votting sawa ila kwenye urais I beg to differ. Vijana wengi waliopewa uwaziri kwa kweli mimi binafsi sijaridhishwa na ufanisi wao....tunaweza kuweka vifua mbele na kusema huyu ni waziri kijana kapewa nafasi na katuwakilisha vema kwa matarajio yetu????

2. Kwa nafasi zao naomba wawe mfano kwa matendo kitaifa na vitu viwe tangible si kwa michango ya maneno au maandishi bungeni, propaganda ya vyombo vya habari zimetosha sasa.....waanzie kwenye vyama vyao huko hayo mabadiliko iwe case study....wakiweza kwa moyo mmoja tufikirie hili wanalopendekeza kama litakuwa na manufaa kitaifa

3. Hivi kweli mafanikio ya nchi hii hayawi kama yanavyotarajiwa kwa sababu ya umri wa Rais???? Zitto na January kweli hii ndo thinking yenu kwa manufaa ya Taifa hili ??? Y dont yu guys encourage vijana wengi kugombea ubunge ili serikali itokane na vijana wengi kupitia uwaziri????? Au uwaziri iwe ni kazi ya ku apply ili vijana wengi wenye uwezo na wasiopenda siasa za majimboni wawe na nafasi kulitumikia Taifa kwa nafasi hizo as well???

4. Kweli ninyi ni vijana.....mmepata ubunge n hence platform n access ya vyombo vya habari BUT BUT BUT hoja zipo nyingi za kwanini kijana kakwama na si umri wa kugombea urais I believe and know and am sure mnajua na kuamini pia vyanzo vya mkwamo, strategies za kujinasua na jinsi ya ku-emplement towards a success....anzieni hapo kwanza ili mtakapokuwa at fourties muwe na sababu ya kuonekana as to why nyie muwe candidates wazuri.....

5. Njooni huku kwa vijana wa kawaida "commons" mfanye capacity building country wide, mpate mawazo yao, priorities nakadhalika hii yaweza kuwa mbegu nzuri sana...anzeni kwa mfano na wafanyakazi, wafanyabiashara then wasio na ajira.....(......kaeni nao, mle na mnywe nao....)

6. Dhambi ya jinsia isije tena kwenye sura ya umri chonde chonde tuwe macho Watanzania
 
No! Problem sir, with that so long as they have the same idiology in fighting against selfish. Ushirikano ni mzuri sana katika mustakabali wa kujifunza mambo na kuikulia siasa, learn what others are doing so that you can be more perfect.
 
Hakuna ubaya wowote Zitto kufanya kazi Janauri, kinachotakiwa ni kuwa mzalendo na nchi yako kwa mustakabali wa taifa letu.

Mkuu pia kumbusha kwamba siasa si uadui hata kidogo. WanaJF wengi wanadhani ukiwa mwanasiasa unatakiwa uwanunie ambao hawako chama kimoja na wewe! Hawajui kwamba Dr. Slaa na Dr. Kikwete ni marafiki wakubwa ila wakiwa kwenye majukwaa ya kisiasa wanasemana.

Wacheni vijana waje na hoja kwa mustakabali wa nchi. Wanaweza kuamua kuunda Chama chao wakaachana na hivyo vyama vyenu na wakasonga mbele. Wana hoja kubwa mbili zinazofanana: Kupinga posho za vikao na kutaka umri wa mgombea urais ha TZ uwe kuanzia miaka 35.

Hayo si mambo mazuri kwa taifa kweli?
 
Uraisi miaka 35 jamanii too young to hold such a possition!
Ila kwa kupiga kura iyo 16 sawa bse mitoto ya siku izi inakuwa kama inakula pumba!
 
Maikitika kusema kuwa vijana hawa wawili ZITTO na JANUARY wana lao jambo......Naweza kusema kuwa wana uchu wa madaraka...HIVI JAMANI ikulu kuna nini? Mbona kila mtu anataka kukumbilia pale? ZITTO anampango wa kuibomoa CDM ndio maana ameona aanze mkakati wa kuingiza suala la umri wa uraisi kwenye katiba. Tukumbuke ni ZITTO huyu huyu aliwahi kuwaambia wapiga kura wake kule Kigoma kuwa mwaka 2015 hatagombea tena Ubunge bali Urais. Hivi ni nani amemuakikishia kuwa CDM watamteua yeye kuwa mgombea wao wa Urais ? Kwanza kwa umri wake alio nao kama katiba mpya isipo afiki swala la umri wa miaaka thelathini na tano kwa mgombea urais hatan kidhi vigezo maana atakuwa na miaka 39 tu!!! Tujiulize sasa je? Hakuna mkono wa mtu hapo!!! KUONAO nasema KUNAO!!! Mtizame anavyoshirikiana na Magamba Sikatai kushirikiana ila tujiulize mbona ukaribu wake na magamba ni mkubwa kuliko hata wake na Makamanda wenzake wa CDM??? ''''' HILO ANGALIZOooooooooooooooooooooooooooooooooooo''''
 
Sioni sababu ya kuweka umri wa kugombea urais uanzie miaka 40.Ni vigezo gani vinatumika kuweka age limit?Najua kuna baadhi ya wazee na vijana wenye fikra mgando watakaopinga hili.Huwezi kupinga notion ya kizuzu kwamba vijana ni taifa la kesho kisha ukaendekeza hoja ya age limit iwe miaka 40,huko ni kutokujitambua.

Naamini katika uwezo wa mtu lakini pia umri ni kigezo muhimu.Nikipewa watu wawili wenye uwezo sawa (ceteris peribus) basi nitachagua mmoja ambaye ni the youngest among the two....!
 
Wana JF

Mimi ni miongoni mwa wale wanao amini kuwa siasa kati ya vyama na vyama si uadui bali ni kutofautiana kwa hoja katika kusukuma gurudumu la maendeleo. Hivyo ni muhimu kwa wanasiasa wetu wapingane kwa hoja lakini yanapokuja katika kusimamia maslahi ya taifa wayasimamie kwa pamoja bila kujali itikadi zao. Pia si vibaya kwa wanasiasa wetu kushirikana iwe kwa wale wa upinzani na wa chama tawala.

Bada ya kusema hayo nataka kutoa angalizo kwa CHADEMA juu ya ushirikiano wa kisiasa kati ya Makamba na Zitto niseme tuu huu ni mtazamo wangu naweza kuwa sahii au laa. Ukitazama kwa sasa juu ya harakati za kisiasa za hawa mabwana ni kama vile utadhani wako chama kimoja,huoni wakipingana kwa hoja wao kwa wao pia utaona kuwa vyombo vyote vya habari vile vinavyoshabikia propaganda mbovu kwa CHADEMA kama Jombo leo, TAZAMA, na Clauds FM vipo mstari wa mbele katika kuwashabikia hawa wawili kwa mfano ukiridi kwenye suala la posho za wabunge utaona kuwa CHADEMA na wabunge wake wote wamekuwa wakipinga hoja ya poshao za wabunge hadharani sijawahi kumwona Januari akipinga jambo hilo nje ya vikao vya bunge lakini imejengwa dhana na vyombo hivi vya habari kuwa hawa tuu ndio wapingaji wa suala la posha katika msingi huo ndipo ninapojenga hisia na angalizo kwa CHADEMA kuwa makini na urafiki huu yawezekana ukawa ni mkakati maalumu wa CCM kumbuka wamesema wamefungulia mbwa kwa sasa na hakuna kulala mpaka 2015.Nirudie tu niseme huo ni mtazamo wangu naweza kuwa sahihi au kinyume chake na hili ni angalizo tuu.
Lack of credibility
 
kama kweli Nimesikia JK kasema wazee hawana nafasi 2015 ni vijana na haya madai ya zitto na january napata wasiwasi ni coincidence au kama kuna ajenda inaendelea
 
Mkuu kwenye itikadi hapo; Zitto na January wana itikadi moja in common: Wote wanapinga posho za vikao ila hao makamanda wengine unaosema hawana nia thabiti ya kuzipinga posho.
Wote hapo ni corrupt leaders ndio maana wanajidai kupinga posho huku wakijua kuna mahali wanavuta pesa kisirisiri.
Mshahara wa mbunge ni 2.300.000 na kila mwezi anakatwa 700.000 ya kodi za serikali na 900.000 ya shangingi!
inabaki 700.000 take home! sasa kama sio mafisadi wanaishije kwa huu mshahara wa 700.000?
 
putin kawa rais kamaliza mwenzake anamaliza anarudi tena umri unadai,netanyahu kawa waziri mkuu kapoteza karudi tena baada ya miaka kadhaa,kawawa hivyo hivyo,kabila ,tatizo ni sera zetu za kutunza hawa wastaafu kwa pesa nyingi itatugharimu tukichagua vijana,inabidi rais mstaafu asighramiwe sana.
 
Back
Top Bottom