Wakuu hivi punde Star Tv wametangaza kuwa Jumapili ya tar 16.10.2011 kutakuwa na Mdahalo kuhusu Nishati na Tanzania tuitakayo. Mdahalo utaongozwa na Rosemary Mwakitwange kuanzia saa 3.00 mpaka saa 5.00 Usiku.
Washiriki ni Zitto Kabwe (Mb), William Mhando (CEO-Tanesco), January Makamba (M/kiti-Kamati ya Bunge nishati na Madini) na Eliakim Maswi (Jairo wa sasa i.e Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini)
LIVE TEXTS:
Washiriki ni Zitto Kabwe (Mb), William Mhando (CEO-Tanesco), January Makamba (M/kiti-Kamati ya Bunge nishati na Madini) na Eliakim Maswi (Jairo wa sasa i.e Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini)
LIVE TEXTS:
- Mwakilishi TANESCO: Sisi ni watumishi wa watanzania, sisi si waheshimiwa.
- Zitto: Tumebwagwa kwenye kesi ICC na hata Mahakama Kuu ya Tanzania. TANESCO haistahili kubebeshwa deni la DOWANS.
- Zitto: Hakuna tofauti ya DOWANS na Symbion, tofauti moja inatoka Marekani (Symbion) na nyingine haitoki Marekani. Terms ni zilezile.
- Makamba: TANESCO wanajitahidi kupunguza upotevu wa umeme kutoka 21% mpaka 14% ifikapo mwaka 2014
- Makamba: Haina haja ya kubadilisha gari, masuala haya tuyazungumze kwakuwa yanazungumzika.
- Marcus (LHRC): Ili miaka 50 ijayo tupate umeme wa uhakika, basi kwa mujibu wa katiba serikali inaposhindwa tuchukue hatua za kuiwajibisha serikali hii, hatuwezi kuvumilia kuendelea hivi.
- Dr. Kitila: Kuna tofauti gani kati ya Symbion na DOWANS?
- Dr. Kitila: Kulalamika na kupiga kelele ni sehemu ya kazi ya mbunge kwa niaba ya wananchi.
- Dr. Kitila: January, kama gari lililotubeba limeelemewa, unaonaje mkikabidhi gari jingine liendelee na safari?
- Dr. Kitila: Kujumuisha maoni ya January na Zitto ni kuwa TUMESHINDWA.
- Regia: Kama tumewafikishia wananchi 14% tu ya Tanzania kwa miaka 50, inakuwaje watudanganye kuwa miaka 3 ijayo tutawafikia 30% kwa ujumla?
- Makamba: Maelezo ya Zitto ni sahihi. Kama waziri mwenye dhamana na Mwanasheria mkuu walishasema kuwa 'TULIPE' basi deni hili si la TANESCO bali serikali. Wanasheria wanaitumia kesi kama biashara.
- Zitto: Tumebwagwa kwenye kesi ICC na hata Mahakama Kuu ya Tanzania. TANESCO haistahili kubebeshwa deni la DOWANS.
- Zitto: Nitayaongea ninayoamini ni sahihi, mpende kuyasikia au msipende kuyasikia juu ya DOWANS.
- Zitto: Turuhusu wazalishaji na wasambazaji binafsi kwenye sekta ya umeme
- Zitto: Athari za mgao wa umeme kwa watu wa kima cha chini zinajidhihirisha wazi, ametoa mfano
- Makamba: Ni afadhali kutokuwa waziri kuliko kuwa waziri ukawa unatoa kauli tata zisizotekelezeka
- Makamba: Watu wanadai sisi tunaopigia kelele sana masuala haya tunatafuta uwaziri. Hapana, wanaokaa kimya labda ndo wanaoutaka uwaziri
- Makamba: Hatuwezi kulazimisha mtu kujiuzulu, tutasema tunachoamini ni sahihi ili mtu ajihukumu mwenyewe.
- Makamba: Kuna tatizo la ucheleweshwaji wa 'procurement' ndani ya TANESCO
- Zitto: NSSF walienda kuangalia mwekezaji wa kushirikiana naye huko Marekani wakakuta hakuwa na ofisi, ikawa ni sawa na Richmond nyingine.
- Zitto: Ukweli ni kuwa kilichoahidiwa bungeni juu ya kutatua tatizo la mgao hakijatekelezwa. Ni 37MW zilizozalishwa kati ya 207 zilizotakiwa. Wengine wote bado!
- Mwakilishi TANESCO: Ni kweli TANESCO inapoteza 21% ya umeme uliozalishwa (wakati wa transmission) lakini tunatafuta ufumbuzi
- Mwakilishi TANESCO: Katika hali ya kawaida mitambo ya haraka kubabiliana na hali tuliyo nayo ya mgao ni lazima iwe ya mafuta.
- Mwakilishi TANESCO: Shirika lipo chini ya serikali, hivyo mwenye mali bado anaweza kuingilia maamuzi.
- Zitto: Iwe marufuku wanasiasa kuingilia utendaji wa TANESCO
- Zitto: Reform ya TANESCO ni jambo ambalo halina mjadala.
- Makamba: Hatujawekeza vyema kwenye transmission system, tunapoteza umeme mwingi njiani kabla haujafika kwa watumiaji.
- Makamba: Kwa miezi minne tu, TANESCO inaiomba serikali Bilioni 108 kuweza kuzalisha umeme (mzigo mkubwa)
- Zitto: Utamaduni wa kulalamika tu hauwezi kutatua matatizo yetu, mimi (Zitto) na January ni mifano hai.
- Zitto kaulizwa nani atatua tatizo la 'Poor Planning' na Mwakitwange. Kasema tuache kuainisha matatizo tu, tuanze kusuluhisha matatizo yenyewe.
- Zitto: Tuna 'poor planning'. Hatutakiwi kuendelea kutegemea umeme wa mafuta wala wa maji.
- Zitto: Tuna rasilimali za kutosha kuzalisha umeme, gharama ingepungua kama tungetumia gesi asilia na makaa ya mawe
- Makamba: Kama mvua haitegemewi tena kwenye kilimo ni wazi haiwezi kutegemewa pia kwenye umeme!
- Makamba: Hali si nzuri, uwekezaji umekuwa mdogo sekta hii na mipango haikuwa madhubuti
- Makamba: Mwaka 1990 hatukuwa na mgodi hata mmoja, kwa sasa migodi ni 8 na inakula umeme sana.
- Zitto: Hatujawekeza kwa miaka 10 wakati wa 'transition period' ya TANESCO kipindi cha ubinafsishaji.
- Zitto: Kuna tatizo la kuingia kwenye mikataba inayotubana kiasi tunashindwa kujiondoa.
- Zitto: Toka uhuru (miaka 50) tumewafikishia umeme watanzania asilimia 14 tu.
- EWURA wamehudhuria, Zitto Kabwe na January Makamba wapo. Wizara haijapata mwakilishi na wala Mhando hajaja katuma mwakilishi (Engineer Maneno)
- LHRC wamehudhuria pia, watapewa nafasi