Zitto: Magufuli aliendesha nchi Kwa kudanganya, sasa tunatumia uongo ule kuwapima walioko madarakani

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,165
4,581
ZITTO AMTETEA JANUARY MAKAMBA

"Ukweli usemwe, awamu ya tano hakuna ongezeko la uzalishaji umeme lililofanyika, miaka5 bila kukarabati njia za umeme, Magufuli aliendesha nchi kwa kudanganya, sasa tunatumia uongo ule kuwapima walioko madarakani, hatujaogeza hata 1MW kwa miaka 5"@zittokabwe

IMG_20211118_200419.jpg
 
Yaani sie wananchi tunataka umeme wa uhakika, kinyume cha hapo ni utapeli tu.

Waziri anasema planned maintenance, mkuu anatuambia ukame unatutafuna.

JPM anawezakuwa na mapungufu yake kama binadam lakini vitu vyake vilikua vinaonekana.

Mbona alivyopiga mkwara watu kulipwa kukatakata umeme hovyo tukasahau mgao?

Unajua huu upuuzi upuuzi ndio unazidi kuchochea tuhuma kwamba mzee wa watu alihujumiwa.

Unatudanganyaje kweupe kwamba mgao ni matokeo ya utawala uliopita?
 
Tatizo la watanzania wengi ukubwa wa ubongo wetu unaweza ukawa kama wa mende au mende akatuzidi kidogo.

Wakati tunaambiwa kuhusu umeme wa gas,ualisemwa mengi sana yenye matumaini.Wengi tuliamini hasa pale tulipoambiwa kuwa kwa hatua tu za awali hakukuwa na sababu kuendelea kuwatoza watanzania service charge. Kweli zilifutwa kwa vile bomba la gas lilikuwa tayari.

Tuliambiwa umeme wa maji si wa kuaminika kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.Tuliamini kwa kuwa kila mwaka tunashuhudia ukame na mabwawa kupungua maji na hivyo kusababisha mgawo wa umeme.

Alipokuja Magufuli tukaaminishwa tena eti umeme wa maji ni nafuu na uhakika.Watu wakaamini isipokuwa mimi.Tena niliwahi kuhoji hapa hapa jf kuwa ni kwa nini akina Zitto wanasahau maneno yao ya kupigia debe umeme wa gas wakaanza kuimba tena stigler's gorge hydro power project?!!

Leo mnatukumbusha tena umeme wa gas baada ya kuona ukame?!!

Watanzania tutabaki na mitimu yetu ya kipumbavu na kutukanana humu jf lakini ukweli utabaki wazi kuwa Magufuli alifanya maamuzi mabaya kuhusu mradi wa kutegemea maji katika hali ya hewa kama hii
 
Tunasikia kwamba ccm wanatafuta hela ya kampeni 2025 na 2030 kwani hawajui hali itakuwaje huko mbele hivyo wanaona waanze mapema.

Mtasema mengi sana, mara Magufuli alikuwa hivi mara Samia yuko vile lakini ukweli utabaki palepale kwamba ccm ndio tatizo.

Ccm, imebaki na kazi moja tu sasa hivi, kupigana kufa na kupona kung'ang'ania kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile hata kama kwa kufanya hivyo itamaanisha kuangamiza wananchi.
 
Back
Top Bottom