Zitto: Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Novemba 20, 2012

Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.

Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya Azimio la Bunge na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza Azimio na sio kutoa kauli tata za kukata tamaa.

Moja, Suala hili japo sio jipya lakini limeandikwa kama ni jambo jipya. Suala la Serikali ya Uswisi kutaka majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akichangia hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya na kwa kasi? Ni wazi Serikali inajihami kwa kuona kuwa itashindwa kutekeleza azimio la Bunge. Watanzania wasikubali propaganda hii ya Serikali.

Bunge limeagiza Serikali kufanya uchunguzi kwa kutumia njia za kiserikali au wachunguzi binafsi wa kimataifa. Kwa nini Serikali inaanza kubwabwaja ilhali wala haijaanza kazi hiyo? Serikali inajaribu kuficha nini? Kwa nini baada ya wiki iliyopita Benki Kuu kufanya uchunguzi kwenye Mabenki ya Biashara jijini Dar es Salaam na namna fedha zimekuwa zikipelekwa nje (international transfers), leo Serikali inakuja na kauli za kukakata tamaa? Kunani?

Pili, Watanzania wajue kwamba Taifa la Swiss limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko. Serikali ya Swiss hata siku moja haiwezi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika suala kama hili. Ndio maana Azimio la Bunge linataka wachunguzi binafsi ambao hawatahitaji ushirikiano wa Serikali ya Swiss.

Nawakumbusha kwamba mwaka 1997 mara baada ya Joseph Desire Mobutu kuangushwa na Rais Joseph Kabila kule Kongo - Kinshasa, Serikali ya Swiss iliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuonyesha ushahidi kuwa hela hizo za Mobutu zilikuwa zimepatikana kwa njia haramu! Waswiss walitaka Kabila awakakikishie kuwa fedha zile zaidi ya dola bilioni nane za Kimarekani Mobutu hakuzipata kihalali ndio waweze kuzirejesha. Zaire ilikadiriwa kuwa na zaidi ya dola za Kimarekani bilioni thelathini katika Mabenki ya nje ya nchi hiyo. Majibu ya aina aina hii ni majibu ‘standard' ambayo kila nchi inapewa.

Hata Marekani ilipokuwa inafuatilia wakwepa kodi wao walijibiwa hivi hivi. Hatimaye Serikali ya Marekani ikaamua kununua taarifa hizo na kuwakamata wakwepaji kodi wao walioficha fedha Uswisi. Hao ndio Waswiss ambao Serikali ya Tanzania inashabikia majibu yao. Bila Aibu Mawaziri wetu wanayanukuu majibu ya Waswiss kama kasuku. Tunasahau historia haraka sana. Tunakuwa kama mazezeta.

Tusiwe Taifa la mazezeta. Mabwege na mazezeta huimba kila wanachoambiwa kuimba. Sasa Serikali ya Tanzania imekuwa msemaji wa Serikali ya Swiss badala ya kuchunguza utoroshaji wa fedha haramu na kisha kutoa taarifa Bungeni. Naitaka Serikali ianze uchunguzi mara moja kama namna ilivyoelekezwa na Bunge. Suala hili sio suala la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni suala la Wananchi.

Wananchi hawataki uzezeta wa watu waliopewa dhamana ya kutekeleza Azimio lao. Kama hawawezi wapishe watu wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya Watanzania kwa kuchukua hatua stahili za kuchunguza utoroshaji mkubwa wa fedha za kigeni, ukwepaji mkubwa wa kodi na ufisadi uliopelekea Watanzania kuficha mabilioni kwenye mabenki nje ya Tanzania. Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu wa suala hili.

Utekelezaji wa Azimio la Bunge itakuwa ni salamu tosha mafisadi na watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa kujificha na Tanzania sio Taifa la kuchezeachezea. Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema. Hatupaswi kuwa Taifa la Mazezeta. Watanzania sio mabwege tena, Mwakyembe alipata kusema.


Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini.
 
Jana nilimwona Mkuchika akiongelea issue hii, nikamtazama usoni nikaona hata yeye hakiamini anachokiongea, sasa inakuwaje aamini sisi wengine ndio tuamini anachokiongea? Serikali yenye vyombo vyote, kuanzia polisi, CID, Usalama wa Taifa, Marehemu Takukuru, leo hii wanataka mtu binafsi ndiye awaelekeze jinsi ya kufanya kazi! Mwisho watamwomba Zitto akawakamate, maana ni hawa hawa waliokwishawahi kutuambia kwamba Wezi wa fedha za EPA(zilizoibwa kwa vimemo vya akina Mangula) wakikamatwa, eti nchi italipuka!
 
hizo hela hata zikirudishwa zitaishia benki kuu alafu ccm watazitumia kwenye kampeni zake za uchaguzi hapa so hizo hela hata zikiletwa hazitatumika kwa manufaa ya watanzania so bora zibakie huko huko kama kukosa tukose wote
 
Mimi ndo nashangaa maajabu ya dunia yapo Tanzania, inakuweje serikali ya Uswisi yenye account number na majina ya walioweka fedha then iulizie tena majina Tanzania kama sio usanii ni nini hapo
 
Watanzania inatupasa kuchukua hatua, kulalamika sasa basi kama tunataka mambo kubadilika kwa manufaa ya wengi
 
Kweli kabisa tusifanywe Mazezeta!

Nilimsikiliza jana Osea wa takukuru ana sema watawashughulikia lakini nikaona ni nyimbo zilezile!
 
Mimi ndo nashangaa maajabu ya dunia yapo Tanzania, inakuweje serikali ya Uswisi yenye account number na majina ya walioweka fedha then iulizie tena majina Tanzania kama sio usanii ni nini hapo

nafikiri Zito amelieza vizuri sana hili tena akatoa mfano wa Zaire, Uswis wanafaidika na hiyo pesa kuwa kwao, so wanajaribu kufanya kila jambo iendelee kubaki kwao.....
 
Mhe.zito kabwe. nakushauri usitaje majina ya watu waliyo ficha fedha za wizi uswisi mpaka bunge litakapo unda kamati maalum kuhusu jambo hilo. sababu ccm wana tafuta pa kutokea Kwani hoja yako imekuwa mwiba sasa wanaweza kukugeuzia ili kukukomesha ndio maana nasema usitowe mpaka tume ya bunge itakapo patikana.
 
Inasikitisha pale MKURUGENZI ANAPORUDIARUDIA kukosa ushahidi ya matukio ya RUSHWA KUBWAKUBWA MARA KWA MARA. JE INAMAANISHA NINI? AMESHINDWA KAMA KIONGOZI AU IMESHINSHINDWA KAMA TAASISI au TUMESHINDWA KAMA NCHI? JE WALE AKINA JULIAN ASSANGE (WENGINE WANAMWITA JULIAN ASENGA UKITAKA) WANAWEZAJE?!!

INASIKITISHA SANA KAMA NCHI INAWEZA KUTOA MAJIBU KAMA YALE. SERIKALI IKISHINDWA KWENYE MAMBO MUHIMU KAMA YA RUSHWA KUBWA KAMA HIZI NI BORA KUKAA KIMYA!! KULIKO KUKATISHA TAAMAA!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
umetoa statement haswa kwa muda muafaka.hiyo hoja ww njoo uiuze kwetu mtaani sisi tuishugulikie serikali
 
Zitto ipo siku serikali itakupigia magoti ukawakamate wewe mwenyewe.
Wewe umeshaonekana ni lulu usalama wa taifa kazi yao uawafanyia wewe.
Safi sana kamanda wa hoja mtetezi wa wanyonge
 
Mimi ndo nashangaa maajabu ya dunia yapo Tanzania, inakuweje serikali ya Uswisi yenye account number na majina ya walioweka fedha then iulizie tena majina Tanzania kama sio usanii ni nini hapo

Mkuu, Bornagain huo ndo utaratibu. Mimi sijui ZZK anachopinga ni nini.

Tuanzeni kuwataja kama tunawajua. Switzerland inahitaji list ya politically exposed persons. Akina Mkuchika hawawezi kumfunga paka kengele. Mimi naanzisha

1.ZZK
2.
3.
Jazia list hiyo. ZZK kwa kigezo kwamba ukiwa POAC kama ambavyo alishakuwa Cheyo michongo kama hiyo you must get your cut. If you think ZZK is squeaky clean, you had better think again
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom