kinja
Senior Member
- Oct 10, 2010
- 199
- 25
Huu ni utabiri kama wa tabiri nyingine tu na wasomaji wachukulie kama utabiri. Sina mazungumzo yeyote na chama chochote kuhusu kugombea Urais. Ni kweli nina ambition. Ambition zangu zimo ndani ya CHADEMA, chama ambacho nimeshiriki kukijenga.
Kumekuwa na juhudi za makusudi za watu kutaka nitoke CHADEMA, narudia tena siwezi kutoka. Narudia, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine choochote maishani mwangu tofauti na CHADEMA. Narudia, zaidi ya nusu ya umri wangu nimeutumia CHADEMA. Nimetumia nguvu zangu, akili zangu na rasilimaliu zangu kusaidiana na wenzangu kujenga CHADEMA.
Kwamba nazungumza na NCCR ni uwongo, ni uzushi na propaganda yenye nia mbaya kwangu.
Sizungumzi na mtu yeyote kuhusu kuhujumu chama changu. Nimeshasema yeyote mwenye ushahidi na jambo hili autoe. Gazeti la Mwanahalisi lilitoa muda na namba za simu za watu ninaozungumza nao. Nimewachallenge waseme nilikuwa nazungumza nini. Watoe content ya mazungumzo na kama itaonekana kwa namna yeyote ile nilihujumu chama changu nitawajibika.
Watanzania wamekuwa na tabia ya kuamini mambo kwa mkumbo.
Uzushi dhidi yangu umekuwa ukichukuliwa na watu kama ukweli tena ukweli mtupu. Watu kwa malengo yao wamekuwa wakitumia majina zaidi ya moja kwa mtu mmoja na kuingia JF kuandika uzushi (kama huu wa leo) ili kunichafua na kunigombanisha na wenzangu. Bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wenzangu wa chama wanachukua chuki, fitna na uwongo unaoandikwa humu kama ukweli. Inasikitisha sana.
Ninapenda kuwafahamisha wasomaji wote wa JF kuwa sehemu ya habari iliyoandikwa hapa katika thread hii ni uwongo wa makusudi dhidi yangu. Ni imagination ya mtu ambaye anaumwa ugonjwa wa ZITTOPHOBIASIS! Ugonjwa ambao watu wengi wanaumwa na ninasikitika kuwa dawa ya ugonjwa huu hata kwa babu haupo maana ni ugonjwa unasambazwa na ugonjwa wa chuki, fitna, na WIVU!
hapo umenena kiongozi. Mkapa alipendelea kusema uvivu wa kufikiri ambao wa tz wengi tunao. Chapa mzigo