Zitto kweli ni wakati muafaka kutangaza hili?

Status
Not open for further replies.
Timing kivipi? Kwani yeye kusema anautaka urais kutaathiri uchaguzi wa meru?
 
Kuna kambi tatu za kugombea Urais chadema

Kambi ya Dk. Slaa

Kambi ya Mbowe

Kamba ya Zitto

kila kambi ina wafuasi wake lakini wanachadema hawataki siri hii itoke ingawa itakibomoa chama wakati wa kuelekea uchaguzi mwaka 2015
Mama kwa majungu wewe hujambo, najina lako lina akisi tabia yako mbaya.
 
Nimesikitishwa saana na habari zilizo enea na kutangazwa na vyombo vya habari siku ya leo kuwa naibu katibu mkuu ana mpango wa kugombe urais, siyo kwamba nimesikitishwa na nia yake! Bali timing yake, hivi ni kweli mheshimiwa ameona huu ndio wakati muafaka kutangaza nia au kuna ajenda nyingine? Kwa kweli I was so furious with the breaking news, kama ni kweli mheshimiwa Zitto umeona ni muda muafaka nitakuwa na wasiwasi na weredi wako! Kila jambo lina majira yake mheshimiwa Zitto!

Sio kuwa hustahiri ila muda huu concentration nadhani imekuwa ni uchaguzi wa Arumeru, imekuwaje wewe ukaona tena ndio muda wako muafaka kwa ajiri ya kutangaza nia yako ya kugombea urais! Au kuna ajenda nyingine? Manaake the attention will definitely be drifted from Arumeru mpaka hoja yako, what is that?huelewi kuwa results zake zitakuwa mbaya?

Kwa kweli nimeanza kuwa na wasiwasi na baadhi ya viongozi kwenye vyama vya upinzani, nilifikiri lengo la vyama ni kuwa na sera mbadara za kumkomboa mtanzania, kumbe naanza kuwa na mashaka, lakini hata kama umewekwa pandikizi, I think you need to be a very introspective pandikizi and muono wako usiwe wa kiafrica I mean thinking of only tomorrow, but uwe unaenda mbali zaidi think of atleast 20 yrs ahead, I can assure you the day will come the rotten System will have to go! Don’t be among the leaders who will have to go with the rotten system.

Sory kwa kuandika ujumbe mzito namna hii , ila kwa kweli nimesikitika na kwa kuwa mimi ni mpenzi wa mageuzi without a party,but, you have made me doubt your party if you really have good intentions with our mourning nation.

Nawasilisha

Liked by myself, a good about chadema ipo ndani ya nyoyo na akili za watanzania wenye uchungu na nchi yao so whoever thinks he/she can change this will not change within cdm yaani atajikuta yuko peke yake
 
Ndugu Zito mbona una mbio kubwa za kukimbilia Ikulu? Subira huvuta heri! Any sensible man will doubt you aspirations towards Ikulu and such a rush will raise a number of questions with regard to your inner motives from the innermost secret chamber of your heart. Kuwa na subira, ujana una mambo.Kwa speed hii ukiwa Rais katika maamuzi atakuzuia nani????????.
We ni kijana hodari ninakuamini/unaaminiwa /mbele kuna mwanga wako hasa katika utendaji wako, lakini ngoja, vuta subira.
IKULU SI MAHALI PA KUKIMBILIA, ANAYEKIMBILIA IKULU..................................................(Mwal. Nyerere)
 
ana lake jambo tusubiri tuone kutamka tu anautaka urais si busara...... urais unagombea unateuliwa ili hii sijui imekaaje
 
Ktk majibu ya zitto kwa yule aliyemuita mwanazuoni ktk thread ile ya jana sijaona mahali zitto ametangaza nia ya kugombea labda chama kikimtaka! Kama kumbukumbu zangu zimesalimika nadhani kuna sehemu zitto kasema, chama changu kikinitaka niwe rais 2010 na wananchi pia wakinitaka, nitakuwa! Akarudia maneno hayo kwa 2015 na zaidi ya hapo, bali akafika mbali kwa kusema hata kama chama chake hakitataka yeye awe rais acha iwe hivyo, ila urais anautaka kwa 7bu alizoainisha na ni 7bu za msingi. Tatizo liko wapi?
 
Mtamchukia sana ZITO lakini ana haki ya kuomba au kuwa na nia ya kugombea uongozi wowote katika Taifa hili ili mradi awe na ridhaa ya chama/wanachi na akidhi vigezo.
Ninashangaa sana wana CDM wanaotaka madaraka yaendelee kama ufalme!
Ikumbukwe kwamba ZITTO ndiye aliyekijenga na kukiimarisha chama na kikawa na mvuto kwa wengine kujiunga nacho.
Acheni ulimbukeni na upuuzi, kubalini mabadiliko na hamtastawisha demokrasia katika chama kama mtaendeleza monopoly ya kuiongozi kama mnavyotaka nyie.

Hufahamu historia ya CHADEMA....

Mfano mdogo...jiulize

1.katika uhai wa hiki chama, kumekuwapo Wenyeviti wangapi mpaka sasa?

2. Wamekuwapo wagombea urais wangapi kwa tiketi ya chadema, tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi?

TAFAKARI
 
Namkubali sana Mh.Zitto ila binafsi sijapenda ametoa kauli yake si mda muafaka anajua chama kipo kwenye wakati wa mapambano huko Arumeru na ukitoa kauli kama hiyo lazima mijadala mbalimbali itaibuka na kuvuruga baadhi ya mambo mi naona kama jamaa kama kweli anania na mageuzi angekuwa bize na uchaguzi Arumeru kwanza thn mambo mengine yatafuata mi ni kati ya watakao Muunga mkono Mh.zitto ila c kwa 2015 Mungu ibariki Tanzania yetu Mwee!
 
Hajaja kujibu huu uzi ,maana kamanda wetu kila jambo yeye anakuja kujibu ,ndio uzuri wake.
 
Zito njoo CCM huko CDM watakuzito kama walivyofanya ulivyotaka uenyekiti. Tunajua wewe si mwenye kuropoka peoples power wala kuandamana karibu sana CCM muheshimiwa si umesikia Rais anataka wakumrithi awe kijana basi changamkia dili hili Kabwe.
 
Jamani,jamani! Mbona tunapanic? Mbona tunaenda mbali hivyo? Zitto hajaita waandishi wa habari na kusema anagombea urais,kilichotokea ni kuulizwa katikati wa mahojiano kama bwana zitto ana nia ya kuwa rais hapo baadae na yeye akajibu urais anautaka akipata fursa! Ss tatizo liko wapi? Hata mimi ningeulizwa ningejibu kama alivyojibu bwana zitto though timing yangu ni 2035 kupitia cdm.

Hapana ukisoma mwananchi la leo inaonekana zitto amewandikia waraka gazeti la mwananchi kuhusu nia yake.
 
kupenda nako kukizidi mtu unakuwa kipofu wa akili,chadema kama chama makini hatuwezi tena kumtumaini slaa,mtu ambae anaburutwa hata na hawara yake kiasi cha kuwa na maamuzi ataiweza nchi?kwa yeyote mwenye nia njema na chadema hawezi kumpisha slaa.kwa wanaokumbuka jinsi gani hawara wa slaa alipata ubunge kibabe na bila nidhamu,watakubaliana na mimi kwamba kama zitto hafai ni afadhali mbowe arudi ulingoni.jamani matatizo ya slaa ni makubwa ndugu zanguni tukificha maradhi kifo kitatuumbua.
 
Juma labda hujanielewa, ni kwamba huwezi kuima huku unakula, labda uwe mtu wa miujiza, sasa ni wakati wa ku campaign huko ARMR sasa kwa nini hata kama unahojiwa usiseme nitaongelea kwa wakati muafaka? nadhani hebu tuwe na majibu yanayotakiwa kwenda na wakati!

Inategemea, kama aliulizwa ni nini matarajio yake kwa nafasi ya urais, ama swali lenye mlengo huo. Alikuwa na haki ya kujibu chochote. Inawezekana malengo ya kijana ni kuwa rais hapo baadaye, si mbaya. Inaweza kuwa kuanzia 2015 au hata baada ya hapo. Pamoja na hayo, akijitokeza kugombea ndani ya chama chake apewe nafasi. Watu wapige kura, demokrasia ifuate mkondo wake.
 
ndio Kobelo, 100% ni bora kuliko 20%, ukiwa unaongelea jingine unapunguza %concentration
 
Habari wana Jf!

Kwa habari za kutoka kwa chanzo cha habar ndani ya CHADEMA huko arumeru ni kwamba mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Joshua Nassary amesema kwamba amesikitishwa sana na kauli ya Zitto kutangaza nia ya kugombea urais kwan kauli hiyo haijaja muda muafaka na inachochea makundi ndani ya chama pia na kuvunja nguvu ya wapiganaji huko arumeru. Pia ijapokuwa ni haki yake kikatiba lakini haikuwa ni muda muafaka kwa sasa.

My take
Zitto pamojaa na vijana wako wakina benard sanane acheni hila na chuki zenu kwani mnazidi kujiondolea imani kwenye chama, pia jueni kwamba 'this time tommorow' msilete upinzani ndani ya upinzani. Kwani david kafulila aliwahi kusema kwamba

"UONGOZI BILA DEMOKRASIA NI UDIKTETA LAKINI DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO"
 
Da,naipenda chadema na ni mwanachadema lakin kitendo cha zitto kutangaza nia wakati huu wa uchaguz Arumeru east, na kusema yeye na mbowe ndio walihusa kujenga chama kwa kweli kimeniweka njia panda.kiasi fulani naanza kuamini maneno ya mtaani kuwa huyu mtu ni CCM kwa ndani..,japo amezuga kuwa hata ikiwa 2015,2020,2025,lakini lengo lake ni 2015!napenda misimamo yake lakini naona anataka kukizika chama!
 
kupenda nako kukizidi mtu unakuwa kipofu wa akili,chadema kama chama makini hatuwezi tena kumtumaini slaa,mtu ambae anaburutwa hata na hawara yake kiasi cha kuwa na maamuzi ataiweza nchi?kwa yeyote mwenye nia njema na chadema hawezi kumpisha slaa.kwa wanaokumbuka jinsi gani hawara wa slaa alipata ubunge kibabe na bila nidhamu,watakubaliana na mimi kwamba kama zitto hafai ni afadhali mbowe arudi ulingoni.jamani matatizo ya slaa ni makubwa ndugu zanguni tukificha maradhi kifo kitatuumbua.

Wewe ni mtu makini, umegundua kile ambacho wana CDM Hawataki kuambiwa wakaelewa. Sidhani kama mzee huyu anafaa kuwa rais kwa sasa. Ni afadhali Migiro mwanamke aliyekomaa kisiasa kuliko Josephine. Nasema hivyo kwa sababu. Kumpa Slaa urais kwa sehemu kubwa tutatawaliwa na mwanamke. Kama basi tumeamua kujidondosha ghorofani kwa kuchagua rais mwanamke ni afadhali awe mwingine kuliko Josephine.
 
Zitto hii tabia ya kukurupuka na papara ya kupenda madaraka itakuua kisiasa mapema sana. Kwaninu usiruhusu hekima ikuongoze? Uongozi hauji kwa kuforce na kwa vitendo vya kujionyesha. Hao wanaokushauri siyo watu wema kabisa kwa mustakabali wako kisiasa.

Kwanini usiwe mtu mtendakazi mwadilifu then watu wakutambue kwa utendaji wako na nidhami yako? Kwa nini usiwe kama Willbroad Slaa? Yeye hakuomba urais bali alionwa kwa utendaji wake, nidhamu na uadilifu wake, na hiyo ndio inafanya heshima na umaarufu wake uwe juu kadili muda unavyosonga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom