Zitto kweli ni wakati muafaka kutangaza hili?

Status
Not open for further replies.
Nimesikitishwa saana na habari zilizo enea na kutangazwa na vyombo vya habari siku ya leo kuwa naibu katibu mkuu ana mpango wa kugombe urais, siyo kwamba nimesikitishwa na nia yake! Bali timing yake, hivi ni kweli mheshimiwa ameona huu ndio wakati muafaka kutangaza nia au kuna ajenda nyingine? Kwa kweli I was so furious with the breaking news, kama ni kweli mheshimiwa Zitto umeona ni muda muafaka nitakuwa na wasiwasi na weredi wako! Kila jambo lina majira yake mheshimiwa Zitto!

Sio kuwa hustahiri ila muda huu concentration nadhani imekuwa ni uchaguzi wa Arumeru, imekuwaje wewe ukaona tena ndio muda wako muafaka kwa ajiri ya kutangaza nia yako ya kugombea urais! Au kuna ajenda nyingine? Manaake the attention will definitely be drifted from Arumeru mpaka hoja yako, what is that?huelewi kuwa results zake zitakuwa mbaya?

Kwa kweli nimeanza kuwa na wasiwasi na baadhi ya viongozi kwenye vyama vya upinzani, nilifikiri lengo la vyama ni kuwa na sera mbadara za kumkomboa mtanzania, kumbe naanza kuwa na mashaka, lakini hata kama umewekwa pandikizi, I think you need to be a very introspective pandikizi and muono wako usiwe wa kiafrica I mean thinking of only tomorrow, but uwe unaenda mbali zaidi think of atleast 20 yrs ahead, I can assure you the day will come the rotten System will have to go! Don’t be among the leaders who will have to go with the rotten system.

Sory kwa kuandika ujumbe mzito namna hii , ila kwa kweli nimesikitika na kwa kuwa mimi ni mpenzi wa mageuzi without a party,but, you have made me doubt your party if you really have good intentions with our mourning nation.

Nawasilisha
 
Kwani Dr akimpisha Zito na akampa suport si inawezekana? Ni mipango tu, nia ya kwanza ni magamba waondoke magogoni.
 
Mbona Lowassa katangaza tokea 1995 mpaka sana anaendeleza mapambano. WHY NOT ZITTO? Go Go Go Kamanda!
 
Kauli ya kutangaza kuutaka urais haina muda. Wakati wowote mtu anaweza kutangaza nia, hiyo ndiyo demokrasia. Wanaoona Zitto kafanya makosa wana lengo la kufinyanga demokrasia huru. Kwa nini iwe kwa Slaa pekee wakati chama kina viongozi wengi wenye uwezo?
 
Tatizo sio Zitto kutangaza nia ila timin, nadhani tunapotoa kauri lazima tuzingatie tunatoa wakati gani? kauri gani e.t.c
 
mimi sioni kama ni vibaya cause kama mtanzania ni haki yake yakimsingi kabisa. labda ukute una lako jambo dhidi yake.
 
Juma labda hujanielewa, ni kwamba huwezi kuima huku unakula, labda uwe mtu wa miujiza, sasa ni wakati wa ku campaign huko ARMR sasa kwa nini hata kama unahojiwa usiseme nitaongelea kwa wakati muafaka? nadhani hebu tuwe na majibu yanayotakiwa kwenda na wakati!
 
Dah!namkunali sana zitto ila kwa hili kanishangaza sana sikutegemea km atasema haya kwa wakati km huu chama kikiwakwenye chaguzi mbalimbali na kwenye mabadiliko ya kichama(M4C) na licha ya yote hayo mda wa kutoa kauli km hizo tena kupitia vyombo vya habari na si ndani ya chama bado sasa ni 2012 jaman.plz zitto conc. Kwenye jimbo lako n kamati yako (POAC) zaidi mambo mengine yatakuja 2
 
Kuna kambi tatu za kugombea Urais chadema

Kambi ya Dk. Slaa

Kambi ya Mbowe

Kamba ya Zitto

kila kambi ina wafuasi wake lakini wanachadema hawataki siri hii itoke ingawa itakibomoa chama wakati wa kuelekea uchaguzi mwaka 2015
CDM haina wafuasi wanaofuata mkumbo au ufuasi kama wa Simba na Yanga au wafuasi maslahi kama CCM kwa vile maslahi hakuna. Kila CDM inapoimarika ndio vizabizabina mnapopata povu na kuleta vihoja ambavyo havina mpango. Huu uzushi wenu unaimarisha sana CDM kwa kuwa hawavimbi vichwa. Mbowe alitukanwa sana humu jamvini miaka ya nyuma ikamsaidia sana kujirekebisha na sasa ni Mwenyekiti imara sana wa CDM. Mwenzie JK amebaki kuhangaika tu na limeli lake li COSTA CONCORDIA na leo ndo nimejua kuwa nyie wanaccm mna kambi zenu...
 
Alichosema mtoa mada kama mmemuelewa ni kwamba, yeye hapingani na Ndugu Zitto kugombea urahisi, tatizo amekosea timing. Right now concentration yote ipo kwenye uchaguzi mdogo Arumeri ya mashariki, na alichofanya Ndugu Zitto ni kama kudrift attention ya watu toka kwenye kampeni to this ya Urahisi.
Ndugu Zitto, nia yako ni nzuri, I'm your fan, but even I'm starting to have doubt on you.
All the best bytway..!:attention:
 
Hii ndio kama ile unapokua mtoto mdogo huamini kua wakubwa hasa mama na baba nao hua waenda haja. Siku kwa bahati mbya ama nzuri ukagundua hilo bado unataka kupingana na ukweli sababu unapenda uendelee kuamini vile vile vya zamani. Mnampenda Zitto alafu hammjui kua yeye ni Uraisi tu hautaka? au sababu katamka?
 
nafikiri si afya kichama,nikipindi ambacho chadema inahitaji mshikamano wa hali ya juu sana,iweje yeye aibuke na kauli kama hizi,sipingi yeye kugombea.lahasha still bado mda upo he can wait hata iaproach hiyo 2015,nina wasiwasi na nia ya dhati ya moyo wa Zitto katika hili juu ya chadema....over.
 
Ningepewa fursa ya kumshauri mdogo wangu Zito ningemwambia hivi:

ZZ, mimi ni fan wako mkubwa sana, and I am not kidding! Nautambua na kuuheshimu mchango wako katika siasa za nchi hii. Nauheshimu uwezo wako wa kujenga hoja na kusimama katika kauli zako, ingawaje ziko nyakati msimamo wako huwa unayumba (sijui ni sababu za mgongano wa masilahi au na wewe wakati mwingine unanunulika, sina hakika). Hata hivyo katika umri wako huu mafanikio yako kisiasa ni makubwa sana na ninakupongeza. Ningependa nikuone unapaa zaidi na hiyo inakudai ujijenge zaidi kwa kutumia jamvi hilo hilo la mjengoni.

Ila ndoto za kuwa rais wa nchi hii miaka 3 ijayo ungeziweka pembeni. Kwa sasa HUCHAGULIKI! To be honest kama kuna kitu kitakumaliza kisiasa wakati huu ni hiyo haraka yako ya kukitamani kijiwe cha Magogoni. Bado una fursa nzuri zaidi mbeleni kama ukitumia vizuri wakati huu ku-win support ya watanzania, na insallah Mwenyezi Mungu atakujaali AFYA!
Ni ushauri tu.
 
Nikiliangalia hili ( ishu ya Zitto) kwa mtazamo Chanya.

Yawezekana ni mbinu sahihi ya kuwaweka tayari Watanzania waamini kuwa Rais 2015 atakuwa mwanachama wa CDM.

Kwa sababu kulikuwa na harakati nyingi za kusema kuwa Rais 2015 atatoka CCM huku wakitumia kigezo cha Mkuu wa kaya anaandaa wa kurithi nafasi yake ya Urais, huku wengine wakimpigia chepuo Waziri mkuu Aliyejiuzulu EL (WAEL) ambaye ni mwana CCM.

Na hii inaweza kuwa kweli kwani Mh. Sitta naye kajiingiza huko kwenye kujitangaza kuwania urais ili kuua move ya CDM kupitia Zitto.

Mtazamo wangu huu utapata mashiko kama Zitto alijaribu kuwasiliana na viongozi wa CDM na washauri wengine aliowataja wakati akijibu hoja za Mwandishi wa Gazeti fulani lichapishwalo hapa nchini, kabla ya kutoa hoja hii.
 
...hapingani na Ndugu Zitto kugombea urahisi, tatizo amekosea timing. Right now concentration yote ipo kwenye uchaguzi mdogo Arumeru.... alichofanya Ndugu Zitto ni kama kudrift attention ....
Ndugu Zitto, nia yako ni nzuri, I'm your fan, but even I'm starting to have doubt on you. ...

Kama Zitto amepita humu bila shaka atagundua kuwa ameanza kupoteza mashabiki wake. Nimesema ktk thread nyingine humu leo kuwa mimi ni fan wake lkn nimeanza kupoteza imani kwake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom