Zitto kweli ni wakati muafaka kutangaza hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto kweli ni wakati muafaka kutangaza hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Mar 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Nimesikitishwa saana na habari zilizo enea na kutangazwa na vyombo vya habari siku ya leo kuwa naibu katibu mkuu ana mpango wa kugombe urais, siyo kwamba nimesikitishwa na nia yake! Bali timing yake, hivi ni kweli mheshimiwa ameona huu ndio wakati muafaka kutangaza nia au kuna ajenda nyingine? Kwa kweli I was so furious with the breaking news, kama ni kweli mheshimiwa Zitto umeona ni muda muafaka nitakuwa na wasiwasi na weredi wako! Kila jambo lina majira yake mheshimiwa Zitto!

  Sio kuwa hustahiri ila muda huu concentration nadhani imekuwa ni uchaguzi wa Arumeru, imekuwaje wewe ukaona tena ndio muda wako muafaka kwa ajiri ya kutangaza nia yako ya kugombea urais! Au kuna ajenda nyingine? Manaake the attention will definitely be drifted from Arumeru mpaka hoja yako, what is that?huelewi kuwa results zake zitakuwa mbaya?

  Kwa kweli nimeanza kuwa na wasiwasi na baadhi ya viongozi kwenye vyama vya upinzani, nilifikiri lengo la vyama ni kuwa na sera mbadara za kumkomboa mtanzania, kumbe naanza kuwa na mashaka, lakini hata kama umewekwa pandikizi, I think you need to be a very introspective pandikizi and muono wako usiwe wa kiafrica I mean thinking of only tomorrow, but uwe unaenda mbali zaidi think of atleast 20 yrs ahead, I can assure you the day will come the rotten System will have to go! Don’t be among the leaders who will have to go with the rotten system.

  Sory kwa kuandika ujumbe mzito namna hii , ila kwa kweli nimesikitika na kwa kuwa mimi ni mpenzi wa mageuzi without a party,but, you have made me doubt your party if you really have good intentions with our mourning nation.

  Nawasilisha
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimeiona kwenye Mwananchi nikjiuliza maswali mengi.
  Moja; Kwa nini Zitto anauwaza sana urais sana? Juzi tu, Zitto na January Makamba wamekaririwa wakitaka kipengele cha Katibakuhusu umri wa kugombea Urais kirekebishwe ili vijana waweze kugombea (kana kwamba miaka 40 si kijana!)
  Pili, hana agenda maalumu aliyonayo. Je akiwa Rais ana agenda gani maalum hata ndani ya miaka 5 ya awali.
  Tatu, kama Mbunge, amelifanyia nini Jimbo lake ndani ya kipindi hicho cha Ubunge alichokaa? Legacy gani ya kipekee ameweka?
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Niseme tu, nilikuwa fan wa Zitto, ni mdogo wangu na ni home boy lkn sasa naanza kumtilia shaka pengine ana agenda nyinginezo na nimekuwa kinyume na wote ambao wanamtuhumu kuwa anawavuruga CDM, sasa naanza kuwa na shaka kuwa yapo mengi tusioyajua nyuma ya pazia kati ya Zitto na viongozi wenzake wa CDM.
  Sio dhambi mtu kuonyesha nia juu ya hilo lkn nia hiyo hadi kujaribu kushawishi umri wa kugombea Urais ushushwe kwangu unaongeza maswali juu ya nia yake hiyo kwani Urais uko pale unamsubiri afikishe umri huo
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Inanikumbusha kauli ya Mwalimu kuhusu wanasiasa wenye haraka ya kukimbilia Ikulu kama Zitto, kwamba Ikulu kuna biashara gani?
  Zitto, hebu tuambie fans wako, mraba wa kule Mwandiga, Bitale, Kalinzi, Mkigo nk, umeshaumaliza? Au utaumaliza kabla ya 2015?
  Kwa kweli Zitto amenifanya nianze kumtilia mashaka.
  Naamini kuwa Mwanasiasa kimbelembele kugombea Urais, hafai kuwa Rais, Urais si nafasi ya kuikimbilia.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkono wa ccm ni mrefu sana, wamefanikiwa kuisambaratisha cuf kwa kutumia vibaraka wao akina hamad rashid, na sasa ni zamu ya cdm. Kwa kweli inabidi kuwa macho sana na nyendo za baadhi ya vibaraka waliopandikizwa na ccm
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mtanzania yeyote, mwenye akili timamu, mwenye elimu ya chuo kikuu-digrii moja na mwenye umri wa miaka 40. Ana ruhusiwa na ni haki yake kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba. Mwacheni Zitto Kabwe ni haki yake....na mkumbuke kugombea si kuchaguliwa kuwa rais.

  NOTE: Hii nchi hata hayawani anaweza kuchaguliwa kuwa rais na mambo yakaenda tambarare.
   
 7. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Zitto nimeanza kumchukia taratibu ni adui wetu alafu tunaishi naye.
   
 8. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Yale yale ya kibaraka wa ccm HR ndani ya cuf ndiyo nayaona yanaanza kujitokeza ndani ya cdm. ccm itahakikisha inavivuruga vyama vyote mpaka vivurugike na kusambaa kabisa kabla ya 2015. Hii yote ni baada ya kusoma alama za nyakati kwamba kukiendelea kuwa na upinzani imara, mwaka 2015 hawatakuwa na chao.
   
 9. bepari1

  bepari1 Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Jamani,jamani! Mbona tunapanic? Mbona tunaenda mbali hivyo? Zitto hajaita waandishi wa habari na kusema anagombea urais,kilichotokea ni kuulizwa katikati wa mahojiano kama bwana zitto ana nia ya kuwa rais hapo baadae na yeye akajibu urais anautaka akipata fursa! Ss tatizo liko wapi? Hata mimi ningeulizwa ningejibu kama alivyojibu bwana zitto though timing yangu ni 2035 kupitia cdm.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Utingo, mwaka 2015, Zitto atakuwa bado hajafikisha miaka 40, na hii ndiyo inamsumbua sasa Zitto.

  Sijui kwa nini ana haraka za Seif Sherrif Hamad wakati wa Mwalimu. Seif alikuwa kwenye njia nzuri sana kuwa Rais wa Tanzania ila alipofanya haraka ya kujiita MPEMBA, ngoma ikawaka. Sasa kama Makamu wa Rais Zanzibar, what a shame.

  Nafikiri anafanya haya huku akiwa amesahau kuwa Kikwete alilia sana kuwa kiongozi wakati kwenye history, hakuwa amefanya chochote cha maana kwa Taifa zaidi ya kusema "Rais kijana, anapenda michezo, ni Handsome nk nk". Kila atakayefuata huko mbeleni, hili la KIJANA halitauzika tena.

  Nina amini wengi watampigia KURA Lowassa (hata mie itabidi nifanye hivyo) kwa kuwa walau Lowassa namfahamu kuwa ni Mkapa Mkapa vile, Mwizi, Muuwaji(Sina uhakika ila yupo CCM), Fisadi ila ni Mchapa kazi si kawaida. Ni Mpiganaji asiyechoka na kwa CCM nzima, ndiyo mtu mwenye nafuu na unapomchagua unajua kabisa unanunua PILIPILI (Utamu wa pilipili ni muwasho wake) na siyo wanakupa Pilipili hoho na kumbe ndani wameficha pilipili kichaa.


  MTU ANAYEKIMBILIA IKULU, MUOGOPENI KAMA UKOMA (Hayati baba wa taifa Mwalimu J. K. Nyerere).
   
 11. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtamchukia sana ZITO lakini ana haki ya kuomba au kuwa na nia ya kugombea uongozi wowote katika Taifa hili ili mradi awe na ridhaa ya chama/wanachi na akidhi vigezo.
  Ninashangaa sana wana CDM wanaotaka madaraka yaendelee kama ufalme!
  Ikumbukwe kwamba ZITTO ndiye aliyekijenga na kukiimarisha chama na kikawa na mvuto kwa wengine kujiunga nacho.
  Acheni ulimbukeni na upuuzi, kubalini mabadiliko na hamtastawisha demokrasia katika chama kama mtaendeleza monopoly ya kuiongozi kama mnavyotaka nyie.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sijaona Tatizo la Zitto! Naamini Zitto ana maana kubwa kuliko tu kutangaza hivyo. Ngojeni Magamba wakavyo react
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kuna kambi tatu za kugombea Urais chadema

  Kambi ya Dk. Slaa

  Kambi ya Mbowe

  Kamba ya Zitto

  kila kambi ina wafuasi wake lakini wanachadema hawataki siri hii itoke ingawa itakibomoa chama wakati wa kuelekea uchaguzi mwaka 2015
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Jana niliona thread yenye maneno mengi sana aliyoandika zito.yeye anasema alikuwa anamjibu mwanazuon mmoja.ktk kujibu nilisema 'zitto ana tatizo moja kubwa'
   
 15. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni kweli. hakutaka kuwa mnafiki.
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Jana niliona thread yenye maneno mengi sana aliyoandika zito.yeye anasema alikuwa anamjibu mwanazuon mmoja.ktk kujibu nilisema 'zitto ana tatizo moja kubwa'
   
 17. Jaffary

  Jaffary JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 758
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  kauli aliyoitoa Mh kabwe haukuwa muda wake muafaka kwani watu wameconcetrate kuona kitakachojiri arumeru! Uwezo anao tena mkubwa lakin itafikia mahali kwa hizi kaul zake kukosa suport ya vijana! Nafikir jamaa anahitaji more 5yrs kukomaa kisiasa ikiwa ni pamoja na kufahamu anatoa kauli wakati gan na impact yake
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hili ni bomu la kugombea Urais chadema litakapopasuka chama kitasambaratika kabla ya 2015
   
 19. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Namshukuru zito kujitokeza mapema hii kwakua tutapata mda wa kupembua na kuchambua
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wishful thinking!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...