Zitto: Kwa sasa na mwaka 2016 mauzo ya nje tupo vizuri sana

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Tupo vizuri ?

MAUZO NJE
Mwaka unaoishia Machi 2016
- Bidhaa za Viwanda $1.4B
- Maua na Mbogamboga $960M
- Samaki $402M

BAADA YA MIAKA 5

Mwaka unaoishia Machi 2020
- Bidhaa za Viwanda $805M
- Maua na mbogamboga $174M
- Samaki $155M
 
Sekta ya uchumi imeyumba sana, hii imesababishwa na kutegemea ukiritimba wa mawazo ya mtu mmoja, mtu asietaka kusikiliza ushauri wa yeyote.

Yeye ndie mwanasiasa, mchumi, mhandisi, daktari wa Corona, na mengine yote.
Na ndivyo ilivyo alafu anapata muziki mororooo kutoka kwa DJ Zero Mr. Mbowe Mugabe!
 
Mauzo ya samaki nje kwa Sasa Ni makubwa kuliko miaka mitano iliyopita, aache uongo huyo zitto
 
Tupo vizuri ?

MAUZO NJE
Mwaka unaoishia Machi 2016
- Bidhaa za Viwanda $1.4B
- Maua na Mbogamboga $960M
- Samaki $402M

BAADA YA MIAKA 5

Mwaka unaoishia Machi 2020
- Bidhaa za Viwanda $805M
- Maua na mbogamboga $174M
- Samaki $155M

corona plus miezi 3 ambayo bado ili mwaka wa fedha ukamilike, hope tutafika tu
 
Samaki tumeamua kuwala wenyewe baada ya kupata elimu ya lishe bora kutoka kwa Mh. Luhaga Joelson Mpina!
Vitu vingi tulivyokuwa tunauza nje kwa sasa tumeona umuhimu wa kuvitumia, kwa mfano korosho tunazila wenyewe, chai na kahawa tunakunywa wenyewe, bidhaa za viwandani tunatumia wenyewe, hata bandari zetu tunazitumia wenyewe, n.k. Njia bora ya kupambana na mabeberu ni kujitegemea na tumefanikiwa kwa muda mfupi sana.
 
Back
Top Bottom