Zitto kuwasilisha Bajeti 'Mbadala' ya Upinzani Juni 18, 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto kuwasilisha Bajeti 'Mbadala' ya Upinzani Juni 18, 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jun 17, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia ni waziri kivuli wa Fedha Zitto Kabwe leo atawasilisha bajeti mbadala ya upinzani bungeni.

  Macho na masikio ya watanzania yanatarajiwa kushuhudia kile kilichoandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo kama majibu kwa bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri wa fedha William Mgimwa.

  Bajeti hiyo ya serikali inapingwa kila kona ya nchi kutokana na serikali kujitengea asilimia 70% ya bajeti hiyo kwa matumizi yake huku miradi ya maendeleo ikitengewa tu asilimia 30%

  Watu kadhaa waliohojiwa wanasema wanategemea CDM kupeleka bajeti mbadala itakayowakilisha maoni halisi ya wananchi.

  CDM ambayo kwa sasa inaungwa mkono na idadi kubwa ya watanzania itazidi kujikita mioyoni mwa wananchi kutokana na bajeti mbadala itakayowasilishwa na mbunge wake machachari Zitto Kabwe.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya CDM zinadai bajeti mbadala imeandaliwa kwa ustadi mkubwa ili kuwaonyesha wananchi CDM itafanya nini itakapoingia madarakani.

  Tayari kiongozi wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa alishasema chama chake kitatumia kila njia kuipinga bajeti hii kwa manufaa ya watanzania wote.
   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri kwa hamu najua zitto kichwa hatatuangusha
   
 3. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  inabidi wajipange vilvyo ili imani iwe kwao
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Hivi wakuu haiwezekani kama bajeti ya upinzani itakuwa nzuri tukaitumia na kuachana na hiyo ya hao wezi?
   
 5. B

  Bubona JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naamini CHADEMA itatoa bajeti mbadala inayolenga kutatua matatizo ya watu kwa sababu kipaumbele cha CHADEMA ni watu.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Macho na masikio ya watanzania yatakuwa Dodoma kesho
   
 7. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Kwa serikali yetu isivyo kuwa sikivu................Time will tell.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Haitokuja kutokea ktk nchi hii.
   
 9. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Believe me or not, kesho maeneo kadhaa wa kadha umeme utakatika wakati Zitto atakapoanza kusoma bajet mbadala.
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  tunaisubiri kwa hamu kubwa
  kwani kaanda zito kama chadema au imeandaliwa kwa kushirikiana na kambi yote ya upinzani bungeni?
   
 11. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Kwani akisoma hiyo bajeti mbadala ndiyo itakayotumika? Sioni hata umhimu wa bajeti za upinzani hapa Tanzania.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 12. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  mimi nina kasimu ka mchina kana tv ,labda wazuie tbccm isioneshe
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipya. Chadema hawana uwezo wa kuandika bajeti.

  Bajeti ya mgimwa ilikuwa sio mbaya ila yeye mwenyewe ndio hajajuwa kui-present.
   
 14. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Du, ama kweli kwa mjinga hakuna dawa! kwa hiyo watanzania wote hawajui kusoma na kuelewa!
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huwa najiuliza kama wote tunajenga nyumba moja sasa kwa nini mawazo ya upinzani yasiwe yanachukuliwa na kufanyiwa kazi.
  Maana come kesho utakuta kuna gap kubwa kati ya bajeti ya CCM na ile ya CDM
   
 16. M

  Museven JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Perfect view!
   
 17. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni changamoto kubwa kwa serikali na watanzania kwa jumla mana híi nchi haina vitega uchumi zaidi ya pombe na sigara huu ni uongo na ufinyu wa mawazo nchi hii ina rasilimali nyingi na kama zitatumika ipasavyo miaka miwili tu tutakuwa matajiri wa kutupwa tunaomba bajeti ya upinzani iwe yenye tija kwa wananchi masikin wa nchii si km ya ccm yenye manufa kwa matajili.

  Huwez kutuambia eti fedha za matuizi ni nyingi kuliko za maendeleo taifa linazidi didimia mana hakuna akiba ambayo tutatunza mana huwez ukawa na laki katika mtaji alafu unakula elfu sabin unategemea nini lazm ufilisike tu biashara yako haiwez kuendelea hata ukienda kuloga ni kaz bure

  Jamani tuamke au nao ndo wameamua KUTUDANGANYADANGANYA WATANZANIA
   
 18. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 255
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Rais wetu ni msikivu mno. Amekusikia na atafanya hivyo kama ulivyomshauri, we subiri uone....
   
 19. p

  petrol JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  tumewasikia viongozi wa vyama vikuu vya upinzani bungeni wakitokwa mapovu vinywaji kupinga bajeti kuegemea zaidi kwenye matumizi ya kawaida. hata baadhi ya wanaccm wamekuja juu. wakati mwingine watanzania tuna memory fupi na hivyo kuwa watu wa jabu kidogo. Kabla ya uchaguzi wa 2010, rais alitangaza kusudio la kuongeza idadi ya mikoa na wilaya. tulishangilia sana. mvutano uliojitokeza ni katika suala dogo juu ya makao makuu ya mikoa na wilaya hizo mpya. Lakini hatukutaka kukuna vichwa vyetu kutaka kujua gharama za uamuzi huo. Kuongeza mikoa/wilaya maana yake ni kuongeza gharama za utawala. Mara zote katika kufikia maamuzi kama hayo vigezo vinavyotumika ni kusogeza huduma kwa wananchi. tumesogeza, na gharama yake tumeiona. Wakati tunaridhia kusudio la rais la kuongeza mikoa/wilaya tungetambua tunaongeza gharama za uendeshaji wa serikali. Pia baraza la mawaziri limepanuka. hizo zote ni mianya ya kuongeza gharama za uendeshaji. Kwa hiyo tusilalamike sana.
   
 20. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muungano ukivunjika watabaki wao wapemba sisi waunguja,
  badae sisi waislamu wao wakisto.
  badae,sisi UAMSHO wao BAKWATA
  Badae sisi weupe wao weusi
  Badae wao warefu sisi wafupi
  Badae wao wannene sisi wembamba
  Badae wao wamesoma sisi hatujasoma
  mwishoni sisi CUF wao CCM.
  We acha tu wakologane,watajiju

  acha sie tuendelee Zetu na M4C
   
Loading...