Zitto kuwadanganya umma kuhusu mahesabu ya vyama vya siasa

Mwenyekiti wa kama ti ya PAC Zitto Kabwe alikuwa wa kwanza kuvishukia vyama vya siasa kuwa mahesabu yake hayajakaguliwa na CAG lakini kwenye Taarifa ya Kamati yake iliyopelekwa Bungeni inasema sababu kuu ya kutokukaguliwa mahesabu ya vyama hivi vya siasa ni Serikali kushindwa kumpatia fedha CAG ili kumuwezesha kukagua hivi vyama vya siasa (Tundu Lissu ali quote kutoka kwenye taarifa waliyoiandaa wao wenyewe).

IKIWA HILI HALITOSHI


Zitto huyuhuyu alisema ana majina na A/C No. za watu walioficha fedha Uswisi mara kwa mara alipokuwa akiitwa kwenye kamati amekuwa akitoa visingizio vingi sana vya kutofika mbele ya kamati hiyo. Mpaka ilipopelekea Serikali kupitia Mwanasheria mkuu ilipomuhoji na kula kiapo akikiri kuwa hakuna lolote analojua kuhu fedha hizo. Akiwa amepoteza muda wa Wananchi wengi ambao tulitaka watu hawa wafikishwe kwenye vyombo vya dola na fedha hizo ijulikane walizipataje.


Zitto hafai kuwa Mbunge kwani anatafuta umaarufu kwenye hoja potofu na za kizushi. Kwa mchezo huu Zitto anaowachezea watanzania kwa kutumia upotoshaji mkubwa anapaswa kuwajibishwa hawezi chezea akili zetu kiasi hiki.

Nawasilisha
Unakatika katika sikupati eti unasemaje?
 
Hoja ya ZITTO ni kwamba baadhi ya vyama vya siasa avijakaguliwa ikiwemo chadema,na ni kweli chadema awajakaguliwa,hata kama makosa ni serikali na cag,ukweli autobadilika.Tusimzungumzie zitto kama zito bali tuzungumzie kamati nzima,PAC yenye wajumbe kutoka vyama tofauti
 
Zitto anasumbuliwa na upweke ndio maana yuko busy kutafuta attention ya watu, inapaswa arudishwe india kumalizia matibabu.

Mkuu kwani kuna uhusiano wowote kati ya kusumbuliwa na upweke na kutibiwa India?? may be am lost!
 
Zitto mwanamume wa shoka CCM wanamwashia moto CDM wanamwashia moto Serikari pia inambana,lkn mwisho ataibuka kidedea
 
Waambie mafisadi warudishe hela zetu walizofisha huko Swiss
EPA, radar etc
Umaskini ulioko nchini ni kwa sababu ya mafisaidi wa ccm

Watazania kwa kulalamika,Ni nchi gani iliyotuzunguka wana maisha mazuri kiivyo?Nimeenda Kenya,Congo,Malawi,Msumbiji,Burundi ,Rwanda,Kenya Uganda,Nchi hizo zote maisha magumu Chakula bei mbaya Juzi nilikua Kenya wakati sisi kilo ya mchele 1200 wao kwa pesa yetu ni 2000.Tembeeni acheni kulalamika tufanye kazi.Congo mtu ukimshitaki akipatikana na hatia unauliza ulieshitaki utamletea chakula tukimfunga!!!Msumbiji nilikuwa juzi tu,askari mukipishana maneno tukukurukia kichwa jambo lakawaida.
 
Zitto hajatulia.Namshauri aoe, umri wa kukaa msela ushapita above 35, lazima utakuwa na mambo ya ajabu kama hujaoa.
 
Watazania kwa kulalamika,Ni nchi gani iliyotuzunguka wana maisha mazuri kiivyo?Nimeenda Kenya,Congo,Malawi,Msumbiji,Burundi ,Rwanda,Kenya Uganda,Nchi hizo zote maisha magumu Chakula bei mbaya Juzi nilikua Kenya wakati sisi kilo ya mchele 1200 wao kwa pesa yetu ni 2000.Tembeeni acheni kulalamika tufanye kazi.Congo mtu ukimshitaki akipatikana na hatia unauliza ulieshitaki utamletea chakula tukimfunga!!!Msumbiji nilikuwa juzi tu,askari mukipishana maneno tukukurukia kichwa jambo lakawaida.
Unajua kipato cha mwalimu wa shule ya msingi Kenya? Hata ukienda SA bei ya kilo ya Michele iko juu kuliko hapo bongo......Sasa ukishatumia kwa ukilinganisha bei bila ukilinganisha kipato ...your lost....ndio maana embe Mliman city ni ghali kuliko gengeni....au embe Tandale na embe hilo hilo Masaki kwanini bei zake ni tofauti?
 
Back
Top Bottom