Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
Na Elius Ndabila
Leo chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mh ZITTO KABWE wamezindua ilani yao ya uchaguzi baada ya makubaliano yao ya kuungana dhidi ya CCM kugonga Mwamba. Katika hafla hiyo ya kuzindua ilani yao, pamoja na wazungumzaji wengine Mh KABWE amezungumza mambo mengi ili kujaribu kuudanganya Umma na kuichafua taswira ya CCM na Serikali yake.
ZITTO KABWE amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano serikali ya CCM imetekeleza asilimia 31 tu ya yale ambayo yaliandikwa kwenye Ilani na asilimia 69 eti hayakutekelezwa. Good! Inawezekana KABWE akawa sahihi lakini hajaeleza kwa nini anadhani hayakutekelezwa.
Nimkumbushe Mh ZITTO kuwa wakati hayo mengine inayodai hayakutekelezwa na yaliandikwa basi pia yapo mengi ambayo hayakuandikwa kwenye Ilani na yametekelezwa.
Tafiti zinaonyesha wazi kuwa Tangu nchi ipate uhuru basi hakuna kipindi cha miaka mitano ya kiongozi yeyote kilichowahi kufanya kazi kubwa kama kipindi hiki cha JPM. Nikukumbushe machache ambayo ameyatekeleza na hayakuandikwa kwenye Ilani ambayo kwa tafsiri yangu ndiyo yalienda kufanya *substitution* ya yale ambayo kwa tafsiri yako umesema hayakutekelezwa.
Kwenye Ilani ya CCM hakukuwa na kipengele cha Elimu bure, lakini Mh Rais na serikali yake wamefanya hivyo. Wametoa elimu bure, wameboresha majengo na kujenga shule mpya na vyuo.
Kwenye Ilani ya CCM hakukuwa na mradi mkubwa wa Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Nyerere ambako fedha nyingi zimeelekezwa. Pamoja na hayo kwenye Ilani ya CCM kulikuwa na kuboreshwa kwa miundombinu lakini hakukuwa na ujenzi wa Reli ya Umeme kutoka Dar kwenda Mwanza ambayo inatumia trilioni of money.
Kwenye Ilani ya CCM hakukuwa na kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma lakini kwa miaka mitano mfupa uliowashinda wote JPM amefanya.
Kwenye Ilani ya CCM kuliandikwa kuboreshwa kwa mawasiliano, lakini haikuandikwa kufufua usafiri wa Anga. Mwanaume kwa miaka mitano amenunua ndege 11 ambazo hata wewe unazitumia unapoenda Kigoma.
Kwenye Ilani ya CCM haikuandikwa kuwa ataziba mianya ya watu kwenda kutibiwa India na kuboresha hospitali zetu, lakini JPM alipoingia aliona umuhimu wa hilo akaamua kuongeza bajeti kwenye afya na kuboresha hospitali zetu za ndani. Leo ukienda Mhimbili wanafanya opareshi ambazo mwanzo tulitumia fedha nyingi kwenda nje ya nchi. Hii haihitaji kwenda shule kusoma.
Ninatambua Mh Kabwe unakumbuka pia kuwa kwenye Ilani ya CCM hakukuwa na daraja la juu la Ubungo, terminal three na viwanja mbalimbali mbali vya ndege lakni JPM amefanya.
Mh ZITTO kwa kuwa ni msomaji mzuri wa Ilani ya CCM, basi kwa leo nikupe haya tu ili kukufahamusha kuwa wakati hayo mengine hayajatekelezwa ikiwepo milioni 50 kwenye kila kijiji,basi mambo makubwa zaidi yamefanyika ambayo hata kwenye Ilani hayakuandikwa.
Hivyo basi unapolalamika kuwa haya hayakutekelezwa, basi ilipaswa uwaambie pia yaliyotekelezwa lakini hayakuandikwa. Vinginevyo kuongea juu juu ni kuacha ombwe na kuweka uhalali kana kwamba kushindwa kufanya yaliyoandikwa kwenye Ilani basi hawakufanya chochote.