Zitto kutua Tabora Jumamosi: Mapokezi Makubwa yamsubiri

Status
Not open for further replies.
Labda wanatabora watabadilika this time maana wao ni ccm na chama chao cha upinzani ni CUF! Let me wait and see.
 
nauliza tu hivi zitto aliwahi kufanya ziara za aina hii mwaka gani, yaani ziara zisizo na itikadi ya chama (chadema) , kwanini wakati huu??
La.kuvunda halina ubani atadondoka tu hawezi kwenda kinyume na mapenzi ya mungu...lazima atadondoka tu.mifano ya watu sampuli ya zito ipo mingi na walivyoishia tunajua ni suala la muda tu
 
Hahaha CDM,Hata mkimfukuza ZZK uanachama hakika atawaacha na majeraha makubwa coz ana siri nzito juu ya CDM na kwa kua jamaa nae huwaga ana genuine data cku akizishusha CDM kwisha kabsa
dogo anafukuzwa na hakuna kitakachotokea.niijuavyo mimi cdm haina cha kuficha.Cdm damu tumeshamjua kuwa ni msaliti na siku anaondolewa wengine tutasherekea
 
Hizo ziara zake zinaratibiwa na nani ? Amepata wapi ruzuku ya kufanya mikutano hii? Lengo hasa ni kutukana viongozi wa CDM au kujenga CDM? Kama ni kujenga CDM mbona anazuia upeperushaji wa bendera za CDM? Lengo ni kubomoa CDM au kujenga? Hivi kuna chama kinaitwa Tanzania? Au katiba imeishapitisha mgombea binafsi? Anataka kugombea Kigoma, Tabora au kote na kwanini anapita alipopita Slaa na mfano asianzie kusini au kaskazini? Kumbe ZZK ni billionaire wa kuweza kupiga kampeni mwenyewe? Kwa chama kipi??? Aaaah kumbe naota tu!!
 
Taarifa nilizo zipata muda mchache uliopita ni kuwa teamwork ya mwana siasa machachari,kijana, mwenye mvuto, anayependwa na vijana wengi hapa nchini Zitto Zuberi Kabwe imewasili mjini Tabora kwa ajili ya kuratibu mapokezi ya mwanasiasa huyo ambapo anategemea kuwasili mjini Tabora siku ya Jumamosi.

Jembe letu ZZK endelea kuwasha moto sisi tuko nyuma yako.

Kasafishe taka zote zilizoachwa kila pembe wahafidhina walikopita kisha umma utaamua nani mwongo na nani mkweli.
 
Zitto KAPANIC na KUCHANGANYIKIWA....alafu mtoa taarifa hayo manen ya kusema anapendwa na vijana unakosea....vijana hasa wasomi wanamwona kama MSALITI
 
Yaaani huyu jamaa ni kero
kweli naomba sana afukuzwe chadema na wafuasi wake waende naye waone km
tutatetereka..huyu ni mamluki tu tamaa ya madaraka imemjaa hana
lolote..yaaani i wish..ninge.mmmm....za

lazima mumtambue kijana wa kiha, siku 14 kwisha hakuna cha lissu wala nani, ukiona issue mnyika yuko kimya ujue hali ni tete, anaendelea kupiga deki matapishi, akifika kahama mwanza tayari sebule itakuwa safi, lissu na dadayake wajue bungeni hawarudi tena.
 
CDM ni taasisi kubwa,wakati munapiga ramli cc makamanda tupo field na CDM NI MSINGI!

Nani kakudanganya, cdm ni saccos ndogo mno ni kampuni binafisi ya wachaga kama inavyofahamika CDM yaani Chaga Development Manifesto.

Acha kabisa kudanganya watanzania kuwa hiyo kampuni ni taasisi kubwa!!!!

Achaaaaaa!!!!!!!
 
Yaaani huyu jamaa ni kero kweli naomba sana afukuzwe chadema na wafuasi wake waende naye waone km tutatetereka..huyu ni mamluki tu tamaa ya madaraka imemjaa hana lolote..yaaani i wish..ninge.mmmm....za

Division v at work. Hata hoja huna ni kubwabwaja tu. Kweli mbege ukichanganya na viroba lazima kichwa kipate moto.
 
Haende mpaka vijijini, anaogopa nini kwenda mpaka vijijini
Tulia na uandike vema, hakuna neno "haende" katika lugha ya Kiswahili, iwe ni sanifu au fasihi halipo neno hilo bali lipo neno "aende au waende au tuende".

Isije kuwa ni ghadhabu juu ya kulisikia jina la Zitto likishamiri, tofauti na ilivyofikiriwa.
 
Zitto ana haki ya kwenda popote, lakini maamuzi yake ya kufanya mkutano wa adhara katika mikoa aliyopita dr. Slaa hayana malengo mema zaidi ya kubomoa au kutibua chama!
 
Tulia na uandike vema, hakuna neno "haende" katika lugha ya Kiswahili, iwe ni sanifu au fasihi halipo neno hilo bali lipo neno "aende au waende au tuende".

Isije kuwa ni ghadhabu juu ya kulisikia jina la Zitto likishamiri, tofauti na ilivyofikiriwa.

Mkuu asante kwa masahihisho, tunajifunza kila siku... Pia zingatia huo ushauri 'aende mpaka vijijini'
 
Status
Not open for further replies.
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom