Zitto: Kutajwa kwa Mbowe ni siasa tu,Makonda atabeba msalaba wake

Hivi kama umesikia kuna mtu anafanya hiyo biashara ni lazima uende kwenye public kumchafua na huna ushahidi? Makonda kwa hili kakurupuka. Naona anataka apate attention kubwa na aonekane anafanya kazi. Kila kitu yeye ni kukimbilia vyombo vya habari. Honestly haya mambo yanachosa sasa
 
Mungu nijalie roho na moyo kama wa Zitto niwaonyeshe waliokuwa wananichukia na kunidhalilisha kuwa bado nawapenda.Naomba usinipe roho yakulipiza kisasi."Watakucheka,watakudharau,watajaribu kupambana na wewe,utawashinda,watakuona lulu siku moja" muda utaongea.
 
Kwa ufupi........

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amenukuliwa na Gazeti la Mwananchi akisema kuwa kutajwa kwa Mwenyekiti wa Chadema katika Sakata la Madawa ni siasa za kuchafuana na kuchafua upinzani...Ameongeza kuwa Makonda atabeba msalaba wake kwa kukurupuka

Hapo ndipo makonda alipokosea, hata vita yenyewe ya madawa ya kulevya imepoteza maana

Binafsi nimemdharau aliyemwagiza Makonda amtaje Mbowe.

Hivi nchi hii ukiwa mpinzani umekuwa malaika, ama ukivunja kanuni, taratibu na sheria usishughulikiwe kwa sababu tu ni mpinzani? Tuache dhana hiyo ni ya uvivu wa kufikiri, tuwe wenye subira, kama mh Mbowe amesingizwa ukweli utatamalaki tu, hatuna sababu ya kutokwa mapovu, je ikiwa ni kweli kesho tutarudi hapa kusemaje? Tunalaumu watu wanafanya siasa kumbe na sisi ni wale wale! Aliyemtaja Mbowe, na anayemtetea mpaka wakati huu hawana tofauti mpaka vyombo vya sheria vitakavyosema vinginevyo!
 
Kwani MBOWE NI NANI asiweze kuhusika kwenye maovu????????KWA ALICHO ONGEA ZITTO anajaribu kutuambia UKIWA KIONGOZI MKUBWA WEWE UNA KUWA NI MSAFI KAMWE HAUWEZI TENDA OVU LOLOTE......huu ni UPUUZI MKUBWA SANA....
Afu nashangaa sana kwanini WAO KILA JAMBO NI KUJIFANYA KUTETEA kila akiguswa mpinzani????

Kingne tunachotakiwa kutambua MAKONDA si mpuuzi kutoka ADHARANI na kuwataja hawa VIONGOZI na majina MAKUBWA kwenye hii ishu ya MADAWA......he has information zinazompa KIBULI KUFANYA HIVYO....na mtambue hata yeye ana WANASHERIA anaoshauriana nao kwanza na kumpa go ahead katika kutaja haya MAJINA....

kuna wachangiaji WENGNE HUMU JF ni wanafki sana LEO WANAANZA KUJATA MAJINA MAKUBWA ambayo mmekuwa mkitaka sana kuyasikia,,WMATAJA MBOWE TU.....imekuwa MAKONDA MMBAYA.........acheni unafki.....KILA MTU ABEBE MSALABA WAKE
 
Wakati chadema wanataja list of shame uwanja wa mwembe yanga walizingatia brand za watu au zile zilikuwa ni siasa za kusafishana au walifata sheri gani waliitaja mpaka Rais wa nchi JK eti naye FISADI hakuna sheria yeyoye inayokataza serikali kutaja wahalifu eti tutaenda kumshtaki kwa sheria gani aliyesema si makonda kama makonda bali ni mkuu wa mkoa wa DSM mwakilishi wa Rais mkoa wa DSM

Tena ametaja majina ndani ya ofisi ya serikali si studio ya clouds au kwenye bar ni kama mbuge kusema kitu ndani ya mbunge ni tofauti na kukisema nje ya Bunge

Na Chadema ndio mabingwa wa kutaja watu tena hadharani leo katajwa Chief wa Ufipa mnapiga kelele wacheni vyombo vya dola vifanye kazi yake akijulikana hausiki bhasi watu wangapi wamepata tuhuma na kwenda kushinda mahakamani na maisha yanaendelea? leo Mbowe anapata watetezi tena kwa makosa ambayo hata mkewe hawezi kuthibitisha kwa 100% hausiki kwa vile ni biashara haramu ambayo hata mkeo anaweza asijue kuwa unaifanya itakuwa nyinyi ?
 
Back
Top Bottom