MJIMPYA
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 506
- 272
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema ili Tanzania ijiweke katika mazingira mazuri ya ushirikiano na nchi nyingine za Afrika Mashariki, lazima itende haki kwa raia wa nchi hizo wanaofanya kazi mbalimbali nchini.
Akichangia hotuba ya makadirio na mapato na matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika mwaka wa fedha wa 2011/12 bungeni jana mjini Dodoma, Zitto alimtolea mfano Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Sam Shollei ambaye alidai amenyimwa kibali. MCL ni kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Zitto alisema nchi inapoamua kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, haipaaswi kuwa na uwoga.
"Kampuni ya Mwananchi Communications imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini, tena uwekezaji wake mkubwa ni kutoka Kenya, wamewekeza hapa na ndiyo vinara katika soko la hisa Dar es Salaam," alisema Zitto.
"Leo hii CEO wa Mwananchi (Shollei) kamaliza muda wake ameomba kuongezewa kibali serikali yetu inamnyima, tunatuma meseji gani kwa wenzetu," alisisitiza.
Alihoji kuwa kama serikali inataka Watanzania wakafanye kazi, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na wakinyimwa vibali, itamlaumu nani."Wakinyimwa tutasema nini, lazima tuwe makini katika maamuzi tunayoyachukua," alisema Zitto.
Alisema licha ya kuelewa kwamba kuna haja ya kujenga uwezo wa ndani, lakini kabla serikali haijaruhusu uwekezaji wa ndani, lazima iwaruhusu wenye mtaji ili waweze kuendesha shughuli zao.
Je ni kweli Zitto ana maanisha au kuna siri ktk hili? Kuna mtu aliwahi kuandika kuwa Mwananchi ni gazeti ambalo huwa linamwandika vizuri Zitto, je hii ni kurudisha fadhira?
Na je kwanini hakutaja/kufuatilia sababa za huyu kunyimwa kibali? Kuna wa-Kenya wengi sana wanafanya kazi TZ kwa miaka mingi tu, kwa nini huyu mmoja tu Zitto ndo ajudge kuwa TZ haiwatendei haki?
Nikuulize Zitto make najua utasoma hapa, una uhakika Kenya mTZ anaweza kuishi na kufanya kazi kwa uhuru na amani kama wao wanavyoishi TZ? Kwa taarifa yako hata wewe ukienda Kenya likakupata lolote hakuna mbunge anaweza kukusema bungeni kwao, hata magazeti ya udaku yanaweza yasiandike habari yako.
Kuna waTZ wengi sana wametendwa mabaya huko Kenya, hakuna mtetezi na hata habari haziandikwi.
Acheni mambo hayo.