SDP_TZ_Mpya
Senior Member
- Jun 21, 2013
- 166
- 77
Mwanzo alisema anashutumiwa kuuza majimbo, kuishtaki CDM kwa CAG na kutoshiriki operesheni. Baadae kasema amehusishwa na waraka ambao yeye haufahamu. Sasa anakuja na masuala ya mabilioni ya Uswisi na kumhujumu Bungeni.
Ndio maana wenye upeo wamemwonya Zitto na wenzake waache kuongea ongea na vyombo vya habari. Msingi wake ni kuwa kama kweli Zitto anaomba msamaha wa dhati kauli zake zinaweza "kuisaidia" ku-influence maamuzi yatakayotokana na utetezi wao wa siku 14 baada ya barua.
Mbele ya wanahabari pale Serena Hotel, Zitto hakuwahi kutamka kuwa CDM na mafisadi wa CCM na serikali kwa ujumla eti wameshirikiana kumfukuza ili kukwamisha ufuatiliaji wa mabilioni ya Uswisi na kupooza Bunge km alivyoeleza kwenye kipindi cha Makutano Show cha Magic FM.
Kwa waelewa wanajua Zitto hana pa kushikilia ila kutaka huruma ya watanzania ila anajionesha wazi 'alitumwa'. Anaonekana sasa kuwahadaa wananchi kuwa CDM inafanya kazi na CCM na viongozi wake kumdidimiza yeye. Hii ni kiini macho na haiingii akilini. Kautumia sana udini na ukabila kujijenga na kuimarisha CHAUMMA cha wanakigoma kinachojumuisha mzee Rungwe, Kafulila, Mawazo na kiongozi wao Zitto km Ben Saanane alivyowahi kutudokeza.
Zitto bado,unahitaji kujifunza namna sahihi ya kupata mafanikio.