Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa.

Zitto ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika Kipindi cha Makutano kinachorushwa na Redio Magic FM ya jijini, Dar es Salaam ambapo alitakiwa kuelezea kipindi cha uongozi wa rais huyo ambaye amebakiza miaka miwili madarakani.

Akijibu swali hilo, Zitto alisema kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu uhuru wa maoni tofauti na ilivyo kwa viongozi wengi duniani.

Mbunge huyo alisema, huchukia watu wanaposema, Rais Kikwete ni dhaifu na kuwataka kutotumia vibaya uhuru wa kutoa maoni.

“Naomba nisieleweke vibaya, lakini ukweli ni kwamba, Rais Kikwete ameacha kiasi kikubwa uhuru wa watu kutoa maoni. Sasa rais anaweza kutukanwa lakini yeye hachukii. Ni vema wananchi wakaacha kutumia vibaya uhuru huo.

“Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika machafuko makubwa,” alibainisha Zitto.

Pia alimwagia sifa, Rais Kikwete kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kuwezesha katika kipindi kifupi viongozi wawili wa mataifa makubwa kuja nchini.

“Rais ame balance (ameweka uwiano sawa) wa uhusiano wa kimataifa. Tunashuhudia ndani ya miezi mitatu marais wawili wanakuja nchini yani Rais wa China, Xi Jinping ambaye alikuja mapema mwaka huu na Rais wa Marekani, Barack Obama anayetarajia kuja nchini, Julai Mosi mwaka huu,” alisema mbunge huyo.

Mbali na sifa hizo, alimtahadharisha rais kuwa anapaswa kuwa makini na watu aliowaita wafaidhina ambao wanateka watu maarufu wakiwamo waandishi wa habari.

Alisema watu hao wanaweza kufuta sifa za uongozi wa Rais Kikwete kutokana na tabia iliyoanza kujengeka nchini hususan ya utekaji, kung’oa kucha na kutoa macho kama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolom Kibanda.

“Matukio yanayoendelea nchini yanaweza kumwondolea sifa rais. Sasa tunashuhudia waandishi wanaanza kuuawa na wengine kuzuriwa ni vema akakemea vitendo hivyo visiendelee kuwepo ndani ya jamii yetu,” alisema.

Zitto alimtaka rais kuhakikisha vurugu za kidini ambazo zimeanza kuchipukia nchini zinakomeshwa kwa nguvu zote ili Watanzania waendelee kuishi kwa kupendana kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Kuhusu suala la udini na vitendo vya rushwa, namuomba Rais Kikwete awe mkali kwa kuvidhibiti. Iwapo vitadhibitiwa mapema ni wazi atamaliza uongozi wake na heshima kubwa,” alisisitiza Zitto.

Habari: JAMBO LEO.
 
""nachukia watu wanaosema raisi kikwete ni dhaifu .....Mnyikaaaaaa bundi kaanza tena CHADEMA.
 
Zitto anamuonea huruma jamaa kwa kumaliza urais na reputation mbaya..Ila bado jamaa ni mdhaifu tu, lets be honest.
 
“Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi
kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama
rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi
kwamba nchi ingekuwa katika machafuko
makubwa,” alibainisha Zitto.


Hivi ndugu Zitto wakati anatoa matamshi hayo sijui kama alifikiria tukio la kuogofya kama la mwanahabari David Mwangosi...
Sijui kama alifikiria vitisho wavipatavyo wale wote wanaothubutu kuweka bayana kadhia za Serikali hadharani...
Serikali ya sasa ni kama panya tu, inang'ata na kupuliza ili ionekane ni njema mbele ya wananchi wake...
 
Kuukubali ukweli kwa mwanasiasa siyo udhaifu bali ni dalili za kukomaa kisiasa.

Ukweli hauna Itikadi.

Endelea kusimama kwenye ukweli ambao ni ufunguo wa kwenye mema katika jamii.

Bravo
 
Kuukubali ukweli kwa mwanasiasa siyo udhaifu bali ni dalili za kukomaa kisiasa.

Ukweli hauna Itikadi.

Endelea kusimama kwenye ukweli ambao ni ufunguo wa kwenye mema katika jamii.

Bravo

Kunya anye kuku akinya bata kaharisha
 
Hivi aliyesema kwanzia leo ni marufuku CHADEMA kuisifia selekali si ndo huyu huyu au?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Zitto kafilisika kihoja!
Rais mzuri duniani anapimwa kwa mambo makubwa 3
1.Kuimarisha uchumi-JK kashindwa
2.Commander-in-Chief-Majeshi yetu yanapigana vita isiyo na faida yyt huko Congo na yalienda Comorro
3.Usalama wa nchi-vurugu za Mtwara

MB wa Jamhuri ya TZ anaposifia kaa sababu tu JK kawa mstahimilivu au kwasababu tu kamleta Obama sio tu anajichanganya bali pia apuuzwe
 
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru

Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.

Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!

Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.

Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album

Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.
 
leo hii mpo mtandaoni na kutoa maoni sababu ya kikwete .. kikwete ni mvumilivu sana atakuja kukumbukwa atakapoondoka .. kuna nchi nyingine mitandao kama jamii forums wangeshaifunga kitambo...
kama ilivyo facebook kwa baadhi ya nchi

bravo zito! hakika weye ni mwanasiasa uliyekomaa
 
Back
Top Bottom