Zitto kawaambia hawana uwezo na wanaendekeza utii wa Chama chao si kuwapiga vita

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,890
Mbunge Zitto Kabwe awapiga vita wabunge wa Dar
Muhibu Said said:


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe,amesema Dar es Salaam, ni mkoa pekee uliosheheni wabunge wasiokuwa na uwezo wa kutetea masuala ya kitaifa bungeni na kuwataka wananchi wajipange, ili kuwang�oa katika majimbo wanayoyashikilia.

Kabwe, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (Chadema) alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Kongamano la Demokrasia na Maendeleo katika Jimbo la Ubungo, lililofanyika Ukumbi wa Kilato, Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam. ''Hakuna mkoa wenye wabunge wabovu kama Dar es Salaam. Huwezi kumsikia Charles Keenja (Jimbo la Ubungo), Rita Mlaki (Kawe), Idd Azzan (Kinondoni), wakitetea masuala ya kitaifa bungeni. Labda kwa sababu hawasumbuliwi na wananchi,'' alisema Kabwe.

Wabunge wengine wanaoongoza majimbo yaliyoko Dar es Salaam ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni Mussa Azzan �Zungu� (Ilala), Abbas Zubeir Mtemvu (Temeke) na Mwinchoum Abdulrahman Msomi (Kigamboni). Kutokana na hali hiyo, Zitto aliwataka wananchi, kila mmoja kwa nafasi yake kujipanga kuhakikisha wabunge hao wanang�olewa katika majimbo wanayoyashikilia katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2010 ili kuleta mabadiliko mkoani humo.

Alisema anaamini taifa kamwe haliwezi kuendelea kama wananchi wataridhia ukiritimba wa chama kimoja uendelee bungeni. Akizungumzia bajeti ya mwaka wa fedha wa 2008/2009 Kabwe alisema bajeti hiyo si ya wananchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali ni ya matajiri kuendelea kutolipa kodi.

''Tungeiita ni bajeti ya wananchi kama tungepunguza bei ya mafuta, ili kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha, kwani maskini ndio wanaolipa zaidi kodi kuliko matajiri ambao hawalipi kodi. Jambo hilo tuliwaambia katika bajeti ya mwaka jana, lakini hawakuelewa,'' alisema Zitto. Alisema hivi sasa dunia nzima inalia kwa tatizo la njaa kutokana na kutokuwepo kwa chakula cha kutosha kama vile mahindi na mchele, lakini cha kushangaza namna bajeti ilivyopangwa, kana kwamba mambo ni sawa tu nchini.

Alishauri badala ya kuondoa kodi katika majembe ya mkono na matrekta, serikali ingeingiza matrekta yenyewe na kuyagawa katika Halmashauri angalau trekta 10 kila halmashauri kwa operesheni maalum ya kuzalisha chakula nchini na kwamba, operesheni hiyo ikiisha yauzwe kwa wananchi wa vijijini. Naye Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema Taifa, John Mnyika alisema wameamua kujipanga ili kuanzisha harakati za kuleta mabadiliko katika Jimbo la Ubungo baada ya jimbo hilo kutelekezwa kimaendeleo na viongozi mbalimbali
 
Last edited by a moderator:
This is the move i was expected from political-non-rulling parties....

Let the wind blow the yard....
 
naona yo yo alikuwa akimjibu shy ambaye inaonekana ujumbe wake umefutwa.

wiki endi hiii!
 
Asanteni kwa kunijulisha na sasa tuangalie mada .Ndiyo nagundua kwamba kuna message imefutwa si ajabu alitukana bila ya hoja .
 
Hivi kuna wabunge wanajua hiyo kitu inaitwa maslahi ya taifa? Wengi naona wanashughulikia matumbo yao tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom