Zitto katika mtihani mzito; Kuingizwa kamati ya uchunguzi wa Mabilioni Uswisi?

Greenwhich

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,337
968
Mwanasheria mkuu wa Serikali Fredrick Werema amesema serikali imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kufuatilia sakata la mabilioni yaliyofichwa Uswiss.

Werema aliwataja wanaounda kikosi hicho kuwa ni maafisa wa usalama wa Taifa, TAKUKURU na polisi wa kimataifa (Interpol). Werema amesema pia watamteua Zitto Kabwe kuwa mjumbe wa kikosi hicho kwa sababu ndiye aliyeibua sakata hilo.

Source: Mwananchi Jumapili.

My Take
Zitto atakuwa katika mtihani mgumu kukubali ama kukataa kuwa mjumbe wa kikosi hiki hasa ikizingatiwa 'nia njema' ya Werema kuunda kikosi hiki.
 
Sina imani na usalama wetu wa taifa. Labda interpol wanaweza kutusaidia kufanikisha hili. Zitto lazima achange vizuri karata zake otherwise ataumbuka katika hili.
 
Zitto Kabwe hapa ndio au utajisafisha na kuonekana kuwa kweli wewe ni kijana machachari mzalendo unayetaka kuwa amiri jeshi mkuu au utajionyesha kuwa wewe ni sehemu ya mafisadi kazi kwako, play your part!
 
Greenwhich Itaandaliwa ripoti hapo mara usikie ziliandaliwa mbili, iliyowasilishwa siyo. Ahhhh upuuzi mtupu! Mtu mwenyewe Werema anayeunda tume. Huyu ni mtu ambaye sijawahi kusikia akitoa hata kauli moja ya busara! Nadhani kama inaundwa na Werema Zitto asihangaike kuifanyia kazi. Ripoti aliyotoa inawatosha waende wakafanye kazi wenyewe huo ni wajibu wao. Kama kweli wanataka waunde tume huru yenye wajumbe kutoka vyama vya upinzani peke yake.
 
Last edited by a moderator:
Itaandaliwa ripoti hapo mara usikie ziliandaliwa mbili, iliyowasilishwa siyo. Ahhhh upuuzi mtupu! Mtu mwenyewe Werema anayeunda tume. Huyu ni mtu ambaye sijawahi kusikia akitoa hata kauli moja ya busara! Nadhani kama inaundwa na Werema Zitto asihangaike kuifanyia kazi. Ripoti aliyotoa inawatosha waende wakafanye kazi wenyewe huo ni wajibu wao. Kama kweli wanataka waunde tume huru yenye wajumbe kutoka vyama vya upinzani peke yake.

Huyu Werema si ndiye alitukana siku moja eti watu wana vichwa vya kufugia nywele?
 
Nani ampe ushauri mpe wewe. Maji aliyavulia Nguo hivyo Hana budi kuyaoga
 
Zitto Kabwe hapa ndio au utajisafisha na kuonekana kuwa kweli wewe ni kijana machachari mzalendo unayetaka kuwa amiri jeshi mkuu au utajionyesha kuwa wewe ni sehemu ya mafisadi kazi kwako, play your part!

Hapo mie sioni umakini wa Werema, hii kitu ameshaivalisha gamba la kisiasa...CCM na serikali wamegomea wananchi, maana hawataki kubadilika kwenye utendaji wao
 
Zitto Kabwe hapa ndio au utajisafisha na kuonekana kuwa kweli wewe ni kijana machachari mzalendo unayetaka kuwa amiri jeshi mkuu au utajionyesha kuwa wewe ni sehemu ya mafisadi kazi kwako, play your part!

Hapo kuna kitu sielewi. Sioni ni kwa namna gani Mh Zitto anaingia kwenye 'pressure' kwa sababu hicho ni kikosi kazi cha SERIKALI. Sio Tume ya Rais au Bunge. Sioni ni kwa namna gani utendaji wao utamhusu Zitto kwani hata findings zao sio rahisi ziwekwe wazi zikikamilika.

Wao waendelee kivyao na Zitto na wengine kivyetu kisha tuje kulinganisha findings zetu. Tusishangae sana hii ikiwa funika kombe nyingine.
 
Mkuu nimenusa pointi yako hapa.
 
werema ni kilaza kabisa, kama kayasema hayaaaaa, zitto katoa hoja bungeni, huwezi mmjumusha katika tume ya serikali tena! .........wataalamu wa mambi tusaidieni
 
Ni fursa nzuri kwake zitto kuendeleza sakata hili,,mimi sion mtihan ulio mbele yake katika hilo

mafisadi wana tafuta kila sababu ya kupinindisha pindisha ukweli,lakini kamwe hatutafumba macho,lazima kitaelewaka tuh
 
Itaandaliwa ripoti hapo mara usikie ziliandaliwa mbili, iliyowasilishwa siyo. Ahhhh upuuzi mtupu! Mtu mwenyewe Werema anayeunda tume. Huyu ni mtu ambaye sijawahi kusikia akitoa hata kauli moja ya busara! Nadhani kama inaundwa na Werema Zitto asihangaike kuifanyia kazi. Ripoti aliyotoa inawatosha waende wakafanye kazi wenyewe huo ni wajibu wao. Kama kweli wanataka waunde tume huru yenye wajumbe kutoka vyama vya upinzani peke yake.

zito si naye yumo kwenye kamati,sasa wasiwasi wa nini.
Kama shutuma alizifabricate sasa ndo mda wa kujua mbivu na mbichi.
 
werema, usalama na takukuru hawana la maana. serikali ilishajikakanganya kwenye hili iweje leo waone vema kulishughulikia na hasa kwa kushirikisha hao watetezi wao?
 
Zito hawezi kuumbuka kwa hili kutokana na ukweli kwamba pamoja na ukweli kwamba yeye ndiye aliyeliibua suala hili bungeni yeye naye alilisoma kwenye ripoti ya mwaka ya benki kuu ya uswizi. Hivyo basi suala la baadhi ya watanzania kumiliki akaunti zafedha kwenye benki za uswizi sio siri
Hivyo basi nadhani serikali ifuate protocal zinazotakiwa ili ijulikane kama fedha hizo si halali yao hao wameliki wake huko uswizi zirejeshwe nchini. kama ni halali yao wachiwe fedha zao mfano unaweza kukuta baadhi ya wamilik wa hizo fedha huko uswizi mmoja wapo ni Said Bakharesa mtu kama huyu fedha hizo zitakuwa ni halali yake aachwe na fedha zake. Ila kama ni mtumishi wa umma ambaye mshahara na marupurupu yake yanajulikana itabidi abanywe aelezi vizuri amezipataje.
 
Zitto hakuna haja ya kuwa katika hiyo team, wewe endelea na mkakati wa uchunguzi huru, wakati wao watakapotoka na ripoti yao "feki" maana ndivyo itakavyokuwa wewe tayari unayo ripoti ya kuitikisa serikali mpaka ipate nyufa zisizo zibika, hiyo itasaidia sana kama agenda 2015, badala ya wao kunadi sera na wagombea wao, watakuwa na wakati mgumu wa kutetea tuhuma.
 
Zito anapenda sana sifa na kwa hili hana msaada kwani kwenye tume ya madini alisaidia nini muacheni akapate posho hana chochote mzee wa kulalamika kama kweli ana uchungu angetaja majina tume ya nini wakati majina anayo?
 
  • Thanks
Reactions: CRN
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom