Zitto, Kafulila, Kitila Mkumbo, Hussein Bashe na akina Ben Saanane waweza Kuanzisha chama kingine?

Mimi mawazoyangu, pamoja na Democrasia kuna utaratibu wa kufuata. Hakuna anaye zuiwa kutoa maoni yake kwenye kikao. Lakini tukifikia kutumia vyombo vya habari kufikishan ujumbe kwa kiongozi wako au unao waongoza sidhani kama tutafika.

Nilazima kila chama kicheze mpila kama timu moja tunasemana na kurekebishana tuukiwa peke yetu lakini tukiwa nje lazima tuonyeshe mshikamano la sivyo tutampa adui tena adui mbaya anaye tutafuta ili atushinde. Hata katika familia kuna utaratibu wa kutoa maoni haiwezekani baba au mama akikosea tumuaibishe mbele ya uma siyo maadili yetu.

Hata mimi nikijana lakini nadhani sisi vijana tunayo matatizo ya jinsi ya kuwasilisha mambo, damu huchemka sana na matokeo yake hukuta tumeharibu vitu kabla ya wakati wake.

Sasa huyu Davidi kama alitaka uwenyekiti angeangalia katiba inasemaje na muda ungefika angepeleka hojayake na kuchaguliwa.Katiba lazima ifuatwe la sivyo hata nchi haiwezi kutawalika kama kila mtu akifanya anavyotaka kwa kisingizio eti anao uhuru wa kutoa maoni
 
Kwani kila mmoja aliwahi kutamka hadharani kuwa yeye ni makini? Nyerere? Mkapa?
Wewe akili yako inavyokutuma, ni lazima kila mtu afuatilize ya hao uliowataja? Huo si umasikini wa kifikra?

Yani haki ya kusema uko makini inatokana na hao watu?

Si unaona uwezo wako wa kufikiri unapofikia?

Usipende kujivua nguo all the time.

Ni ushauri tu...
 
Mtu anazaliwa akiwa makini ama umakini unajengeka taratibu hatua kwa hatua kadri mtu anavyokutana na masuala mbalimbali?

Ukiangalia kwenye kamusi kwa mfano, makini ina maana ya "dignified manners". Kikanuni huwezi kuwa na dignified manners kisha ukajinadi kuwa wewe una dignified manners, kwa sababu hapo hapo itakwisha kuondoa kwenye hizo dignified manners. Kujinadi kuwa wewe ni makini ni ishara ya majivuno.
 
Na Kitila naye? Yeye ana usafi gani? Kama hicho chama kipya kitaanzishwa na hawa vijana halafu na Kitila akawemo, basi yatakuwa yale yale ya CCM, maana hata Kitila Mkumbo naye utendaji wake katika nafasi yake ya uongozi pale chuo ni kama wa CCM tu, tena pengine mbovu kuliko huo.

Sioni kama ana kipya cha kuleta iwapo atasimama upande wa siasa. Nakumbuka alivyosimamia zoezi la uchaguzi wa viti maalumu, na ninajaribu kuufikiria usafi wake hata aweze kusimama upande wa wale wanaoponda uongozi wa vyama vyao.
 
Ligi huiwezi, labda kule Chit Chat na MMU, kwenye blah blah...

Kwenye issue nadda!

Kwa hiyo, hiyo statement hapo juu ina consitute haki ya kutoa ushauri wa kugombea urais?

Nakukumbuka sana kwenye mijadala, na uwezo wako wa kufikiri naufahamu kwa kiasi kikubwa, hivyo hunitishi kwa hoja kaabisah!

Hiyo statement hakuna sehemu iliyomzuwia mtu haki yake ya kushauri.
 
Kama waliokuzunguka ndio wanaopima umakini wako, bila shaka wanakuambia kwamba wewe ni makini. Na hiyo inatokana na jinsi unavyofanya mambo yako hadi hao waliokuzunguka wakauona umakini wako. Sasa katika hali kama hiyo kwanini mtu makini asijiite kwamba yeye ni makini kwakuwa tayari ushahidi upo kwamba yeye ni makini?
Umakini ninao usema hapa hautokani na ushabiki, uwezi kubadilisha ushabiki kwenda umakini. Kama nilivyosema awali umakini unatokana na matendo yako na mawazo yako. Na hapa kinachopimwa ni kwa namna gani unaweza kusoma na kuelewa misingi mbalimbali ya kukufanya uwe makini, tofauti na ushabiki unaopata. Ni rahisi sana kupata ushabiki kuliko kupata umakini!
 
Ukiangalia kwenye kamusi kwa mfano, makini ina maana ya "dignified manners". Kikanuni huwezi kuwa na dignified manners kisha ukajinadi kuwa wewe una dignified manners, kwa sababu hapo hapo itakwisha kuondoa kwenye hizo dignified manners. Kujinadi kuwa wewe ni makini ni ishara ya majivuno.

Mwalimu nimekusoma lakini naomba usinichoke,

Majivuno yanamuondolea mtu umakini?
 
Mwalimu nimekusoma lakini naomba usinichoke,

Majivuno yanamuondolea mtu umakini?

Ikiwa umakini ni dignified manners, kuanza kujitapa kuwa wewe una dignified manners tayari inakutoa kwenye kundi la wenye degnified manners.

Mtu makini hawezi kuwa na majivuno. Mwenye majivuno si makini.
 
Umakini ninao usema hapa hautokani na ushabiki, uwezi kubadilisha ushabiki kwenda umakini. Kama nilivyosema awali umakini unatokana na matendo yako na mawazo yako. Na hapa kinachopimwa ni kwa namna gani unaweza kusoma na kuelewa misingi mbalimbali ya kukufanya uwe makini, tofauti na ushabiki unaopata. Ni rahisi sana kupata ushabiki kuliko kupata umakini!

Kibs achana na washabiki,

Hapa mimi niko serious nataka kufahamu juu ya hii dhana ya kwamba mtu makini hawezi kujiita makini. Nazungumzia watu wanaoelewa mambo, si washabiki.
Kama unafanya mambo na wale wanaoshuhudia ama kunufaika na mambo yako bila kuweka ushabiki wakakuambia, ama ukasikia wakisema Kibs ni mtu makini, na wewe ukajiridhisha kwamba uko makini kutokana na jinsi unavyotenda na kuenenda, kwanini usijiamini na kujiita mtu makini? Nimeuliza hapo kabla, ukijiita makini huo umakini unatoweka? hata kama ni majivuno wewe mwenyewe kujiita makini.
 
Ok basi, ameipuuza haki yao ya kumshauri agombee urais, happy now?

Kwani poiti yanu huioni?

wewe unahitaji scientific research aisee
wapi ulipoona nimepuuza haki?
kwani kushangaa watu kumuona Lema agombee urais ni 'kupuuza haki'??????
 
Ok basi, ameipuuza haki yao ya kumshauri agombee urais, happy now?

Kwani poiti yanu huioni?

Sijaiona pointi yako, kwa sababu apparently wewe mwenyewe huoni, ndio maana una flip-flop ndani ya dakika 5 tulokuwa hapa
 
Nathubutu kusema, vijana wa kweli ambao wanaweza kuikomboa nchi hii hawapo katika hao tunaowaita vijana wanasiasa wa sasa, hao wote mfumo umeshawaharibu na hawana jipya zaidi ya kutafuta cheap popularity, vijana wa kweli ni wapo na wanafuatilia mapungufu na nguvu ya makundi mawili ya wanasiasa:WAZEE NA VIJANA waliopo sasa na hao ndio watakuja na mapya katika nchi yetu lakini si hao mambao tunawaona ni vijana wapenda maendeleo, hakuna lolotea hapo, tamaa tu za uongozi.
 
Tatizo liko hapa...wanaotoa maoni na kusema kwa uhuru wanalalamika kwamba demokrasia na uhuru wa mawazo unaminywa kwa maslahi binafsi ya wachache

Wanaoshindwa kuvumilia uhuru wa mawazo na kuona maslahi yao yako hatarini basi husingizia siri za chama,vikao au uhuru bila nidhamu.So uhuru wa mawazo,demokrasia na wigo wa mamlaka ndani ya vyama vya siasa uende sambamaba na dhana ya uwajibikaji na kuzingatia maslahi mapana ya chama.Hii ni kwa viongozi wa vyama vya siasa na wanachama wa chama husika

Wakati mwingine tunaipinga CCM kwamba inaminya uhuru wa mawazo na demokrasia.Pia tunapinga na kulaani matumizi ya maneno kama siri za jeshi au nyaraka za siri.hii imekuwa silaha kubwa kwa madikteta wote kwenye vyama vya siasa na viongozi wa serikali (hasa viongozi dhaifu).Ndiyo maana leo hii unaona south Africa bado Zuma amekaliwa kooni na Archbishop Desmund Tutu(Mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel) pamoja na wanaharakati wengine juu ya mswada kandamizi na utakaofifisha dhana ya uwazi na uwajibikaji (mswada wa kulinda nyaraka za siri)

Niseme tu kwamba kiongozi dhaifu au adui wa Demokrasia hana chama,kabila wala dini.Mathalani watetezi wa haki na uhuru wa maoni au demokrasia hawana kabila,dini,wala chama cha siasa.Madikteta ni madikteta tu
 
Kibs achana na washabiki,

Hapa mimi niko serious nataka kufahamu juu ya hii dhana ya kwamba mtu makini hawezi kujiita makini. Nazungumzia watu wanaoelewa mambo, si washabiki.
Kama unafanya mambo na wale wanaoshuhudia ama kunufaika na mambo yako bila kuweka ushabiki wakakuambia, ama ukasikia wakisema Kibs ni mtu makini, na wewe ukajiridhisha kwamba uko makini kutokana na jinsi unavyotenda na kuenenda, kwanini usijiamini na kujiita mtu makini? Nimeuliza hapo kabla, ukijiita makini huo umakini unatoweka? hata kama ni majivuno wewe mwenyewe kujiita makini.

Hao walokuita makini kama wao ni makini, basi wakisikia tu kuwa wewe mwenyewe unajiita makini, watajua kuwa walikosea, wewe si makini :D

Ni sawa na mtu anaesifika kuwa na tabia nzuri, kisha akapita mbele za watu na kujitapa " Kwa vile mie nna tabia nzuri, basi sitafanya kadha wa kadha". Hapo tayari ameshavunja kanuni ya tabia njema.
 
wewe unahitaji scientific research aisee
wapi ulipoona nimepuuza haki?
kwani kushangaa watu kumuona Lema agombee urais ni 'kupuuza haki'??????
Kila mtu ana haki ya kumshauri ama kutokumshauri mtu yeyote kugombea ama kutokugombea urais...

Ulichotakiwa kupinga ni sababu walizozitoa hao watoa ushauri, otherwise ni mahaters tu humu, niko stable...
 
Heshima kwako Kigarama.

Muzee unakuwa wapi ninapomzungumzia huyu mpiganaji asiyetumia akili umeniacha nashambuliwa natukanwa nadharauliwa kisa kusema kweli.Nashukuru Mungu wapo watu wenye kuangaisha akili zao wameanza kujiuliza anakotupeleka Lema.Jana usiku nilikuwa Njiro resourt natazama mpira wa Chelsea na Spurs mjadala wa Lema ukaibuka kama moto wa mabua.Kifupi uongozi wa CDM hasa makao makuu unahitajika kuiangalia siasa za Arusha kwa jicho la uangalifu mkubwa.

Lema ameshaingia kwenye dimbwi lile lile la kupenda sifa ambalo Mrema alikuwa anaogelea miaka kadhaa iliyopita. Lema hashauriki wala hatashaurika kwamba "anakosea" na kwa bahati mbaya kama ilivyokuwa kwa Mrema naye pia amezungukwa na "wapambe" wanaomwimbia nyimbo za "ndiyo Mzee!!"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom