Nimenukuu hii Wanabidii na Nuclear,
"Haya ni maneno ya Zitto kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook, mchezo usomeni mapema. Kuna thread ililetwa hapa lakini ukiunganisha dots utapata ukweli wenyewe
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-wa-sasa-kama-wa-el-jk-ac-ra-1995-2005-a.html
Ni dhahiri kwamba kuvuliwa uanachama kwa David ni jaribio kubwa kwa mfumo wetu wa demokrasia kama ilivyokuwa huko nyuma wakati kina Erasto Tumbo walipovuliwa uanachama wa chama chao cha UDP. Ninaamini NCCR-M watamaliza matatizo yao kwa mujibu wa katiba ya chama chao na ndugu David Kafulila atazikabili changamoto hizi kama kiongozi kijana wa kisiasa na kuona hii kama fursa badala ya kukata tamaa. Ifahamike wazi kabisa kwamba David ni mtu huru mwenye mawazo yake na maamuzi yake. Kwamba sisi ni marafiki wa karibu na kwamba tunatoka mkoa mmoja haina maana kwamba lolote afanyalo ama nimemtuma au ninahusika. Ninaheshimu misimamo yake na siku zote huwa nipo upande wa anayeonewa, kudhulumiwa na mnyonge. Msimamo huu wa msingi usiwape watu nafasi ya kunihusisha na mambo ya chama dhaifu kisicho na dira kama NCCR-M.
Kafulila akumbuke kwamba hakufukuzwa CHADEMA, alijiondoa mwenyewe. Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama chetu
Kitila ambaye anajulikana kuwa kambi ya Zitto na akina kafulila alichangia hivi jana.Wamejidhihirisha wazi
i)Nidhamu bila UHURU ni UTUMWA. Kama tunaweza kuwaambia Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, Spika wa Bunge, n.k. kwamba uongozi wao ni dhaifu, hadharani na mbele ya kadmnasi, viongozi wa vyama vya siasa wanapata wapi utukufu wa kujifanya kwamba hawawezi kusemwa nje ya vikao? Viongozi wa vyama vya siasa ni viongozi wa umma na hawawezi kuficha udhaifu wao katika mwamvuli wa nidhamu.
ii)Maamuzi ya chama cha siasa chochote makini lazima yazingatie maslahi mapana ya kisiasa na kijamii kwa sababu chama cha siasa sio kitengo cha mahakama. Mahakama ina haki na wajibu wa kuchukua maamuzi yeyote madamu yamezingatia sheria zilizopo kwa wakati huo hata kama maamuzi hayo ni ya ovyo.Jambo hili haliwezi kufanywa na chama cha siasa makini cha watu.
iii)Vyama vya siasa vipo kwa lengo la kukuza demokrasia. Msingi wa demokrasia ni UHURU WA KUTOA maoni. Kama vyama vya siasa vitatumika kuziba watu midomo kwa kisingizio cha kulinda nidhamu ya chama vitakuwa vinaua demokrasia.
iv) Siamini,na haitatokea niamni, kwamba kumkosoa kiongozi yeyote hadharani ni utomvu wa nidhamu.
Haya hapa ni maneno ya Ben Saanane kwenye ukurasa wake wa Facebook jana
Nimeshawahi kusema hapa mara nyingi kwamba harakati za vijana katika siasa zinafungwa speed governor na wazee wasiopenda mabadiliko ndani ya vyama vya siasa.Fikra huru zinashambuliwa ndani ya vyama vya siasa.....nimefurahishwa pia na maneno ya Nape Nnauye bila kujali itikadi za kisiasa.Pia nitoe wito kwa vijana wa vyama vyote vya siasa kuungana katika harakati hizi na kulaani kwa nguvu zote juhudi za baadhi ya watu ndani ya vyama vya siasa kujaribu kufifisha harakati za kimageuzi au kiunamapinduzi.I dare them to make a constructive desicion and desist from personal attacks.They should Learn to tackle issues, not personalities. Attempting to intimidate is for empty headed thugs
Pia hapa JF Alidhihirisha upinzani wa wazi wazi na hoja iliyotolewa na Lema anayeaminika kuwa karibu na mwenyekiti wa chama kwa kuandika hivi kuchangia hoja ya Lema
My take:
Naona kuna dalili ya vijana wa aina hi"