Zitto, Kafulila, Kitila Mkumbo, Hussein Bashe na akina Ben Saanane waweza Kuanzisha chama kingine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Kafulila, Kitila Mkumbo, Hussein Bashe na akina Ben Saanane waweza Kuanzisha chama kingine?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Dec 23, 2011.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nimenukuu hii Wanabidii na Nuclear,


  "[FONT=&amp]Haya ni maneno ya Zitto kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook, mchezo usomeni mapema. Kuna thread ililetwa hapa lakini ukiunganisha dots utapata ukweli wenyewe[/FONT]

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/154032-kabwe-kafulila-kitila-ben-ni-mtandao-wa-sasa-kama-wa-el-jk-ac-ra-1995-2005-a.html

  [FONT=&amp]Ni dhahiri kwamba kuvuliwa uanachama kwa David ni jaribio kubwa kwa mfumo wetu wa demokrasia kama ilivyokuwa huko nyuma wakati kina Erasto Tumbo walipovuliwa uanachama wa chama chao cha UDP. Ninaamini NCCR-M watamaliza matatizo yao kwa mujibu wa katiba ya chama chao na ndugu David Kafulila atazikabili changamoto hizi kama kiongozi kijana wa kisiasa na kuona hii kama fursa badala ya kukata tamaa. Ifahamike wazi kabisa kwamba David ni mtu huru mwenye mawazo yake na maamuzi yake. Kwamba sisi ni marafiki wa karibu na kwamba tunatoka mkoa mmoja haina maana kwamba lolote afanyalo ama nimemtuma au ninahusika. Ninaheshimu misimamo yake na siku zote huwa nipo upande wa anayeonewa, kudhulumiwa na mnyonge. Msimamo huu wa msingi usiwape watu nafasi ya kunihusisha na mambo ya chama dhaifu kisicho na dira kama NCCR-M.
  Kafulila akumbuke kwamba hakufukuzwa CHADEMA, alijiondoa mwenyewe. Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama chetu[/FONT]

  [FONT=&amp]Kitila ambaye anajulikana kuwa kambi ya Zitto na akina kafulila alichangia hivi jana.Wamejidhihirisha wazi[/FONT]

  [FONT=&amp]i)Nidhamu bila UHURU ni UTUMWA. Kama tunaweza kuwaambia Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, Spika wa Bunge, n.k. kwamba uongozi wao ni dhaifu, hadharani na mbele ya kadmnasi, viongozi wa vyama vya siasa wanapata wapi utukufu wa kujifanya kwamba hawawezi kusemwa nje ya vikao? Viongozi wa vyama vya siasa ni viongozi wa umma na hawawezi kuficha udhaifu wao katika mwamvuli wa nidhamu.

  ii)Maamuzi ya chama cha siasa chochote makini lazima yazingatie maslahi mapana ya kisiasa na kijamii kwa sababu chama cha siasa sio kitengo cha mahakama. Mahakama ina haki na wajibu wa kuchukua maamuzi yeyote madamu yamezingatia sheria zilizopo kwa wakati huo hata kama maamuzi hayo ni ya ovyo.Jambo hili haliwezi kufanywa na chama cha siasa makini cha watu.
  iii)Vyama vya siasa vipo kwa lengo la kukuza demokrasia. Msingi wa demokrasia ni UHURU WA KUTOA maoni. Kama vyama vya siasa vitatumika kuziba watu midomo kwa kisingizio cha kulinda nidhamu ya chama vitakuwa vinaua demokrasia.

  iv) Siamini,na haitatokea niamni, kwamba kumkosoa kiongozi yeyote hadharani ni utomvu wa nidhamu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Haya hapa ni maneno ya Ben Saanane kwenye ukurasa wake wa Facebook jana[/FONT]

  [FONT=&amp]“Nimeshawahi kusema hapa mara nyingi kwamba harakati za vijana katika siasa zinafungwa speed governor na wazee wasiopenda mabadiliko ndani ya vyama vya siasa.Fikra huru zinashambuliwa ndani ya vyama vya siasa.....nimefurahishwa pia na maneno ya Nape Nnauye bila kujali itikadi za kisiasa.Pia nitoe wito kwa vijana wa vyama vyote vya siasa kuungana katika harakati hizi na kulaani kwa nguvu zote juhudi za baadhi ya watu ndani ya vyama vya siasa kujaribu kufifisha harakati za kimageuzi au kiunamapinduzi.I dare them to make a constructive desicion and desist from personal attacks.They should Learn to tackle issues, not personalities. Attempting to intimidate is for empty headed thugs[/FONT]”

  [FONT=&amp]Pia hapa JF Alidhihirisha upinzani wa wazi wazi na hoja iliyotolewa na Lema anayeaminika kuwa karibu na mwenyekiti wa chama kwa kuandika hivi kuchangia hoja ya Lema[/FONT]

  My take: [FONT=&amp]
  Naona kuna dalili ya vijana wa aina hi"
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Chama kingine? hawawezi. Ninachokiona ni jitiohada za kutaka kupanua demokrasia ndani ya vyama vya siasa.

  Wanatoa ujumbe mahsusi wa kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kujenga tabia ya kuvumiliana na watu wanaopishana nao mitazamo ya masuala mbalimbali hata kama wako ndani ya chama kimoja. Kwamba watu wote lazima wawe na mtazamo mmoja juu ya kila jambo ni kitu hakiwezekani na kwahiyo, haki ya mtu kuwa na mawazo tofauti na kiongozi wake ni lazima ilindwe na iheshimiwe.

  Katika hili,niko pamoja na Zitto, Dr. Kitila, Ben Saanane, Kafulila na wengine wote wanaopigania demokrasia halisi ndani ya vyama vya siasa. Lazima tutoke kwenye maigizo ya demokrasia ndani ya vyama na tuwe na demokrasia ya kweli. Hakuna kushabikia nidhamu ya uoga kwa sasa.
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu huwa nasema tatizo la Tanzania ni watanzania wenyewe, hasa Wazee. Mwalimu Kitila alinishambulia sana akasema mie mbaguzi wa umri.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Lema anasimama wapi katika kundi hili?
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mIMI NAELEKEA UZEE, LAKINI VIJANA KUAMUA KWNDA SOLO... WILL BE ONE OF THE BIGGEST MISTAKE IN tANZANIA politics

  it hasnt succeeded anywhere in the world, and i think Malema ana Nguvu za TB JOshua kwa namna fulani ya kuvutia watu hata kama things dont make sense

  IT IS TOO EARLY FOR THAT, YOU DONT DERAILS JUST AFTER GAINING MOMENTUM
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ubaguzi wa umri ni sawa tu na wa dini, kabila, au jinsia!!! Ni dhambi aliyolaani nyerere enzi zake
   
 7. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wengine tutaendelea kusimamia kwenye kupinga ukuu wa chama (part supremacy) dhidi ya haki ya kikatiba ya wanachama wa kawaida. Mimi nasema iwe mtu yeyote yule chama hakiwezi kunyang'anya haki yake ya kufikiri ambayo alizaliwa nayo. Viongozi wa hivi vyama wana tabia sana ya kutishia wanachama wenzao kwa sababu wameshajenga mazingira ya kuabudiwa.

  Ndhamu gani hiyo wanayotaka ambayo inavunja haki ya mtu kusema anachofikiri huku akitakiwa awe kasuku wa kusema au kuyaunga mkono mambo yanayofanywa na viongozi wake hata kama mambo hayo hayaungi mkono.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Wakifanya hivyo watakuwa wanaisaidia CCM 2015!!! Na pia inawezekana kabisa wakawa wanafanya mbio za sakafuni.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mimi bado nahisi suala la Kafulila lina
  'hadithi nyingine' tusioijua......
  nafikiri kuna kitu zaidi ya tunayoyaona.......hasa pale walipompa onyo Mkosamali

  kufukuzwa kwa Kafulila kuna mikono mingi zaidi ya NCCR tu....

  uswahilini wana msemo unasema 'mkomesheni akome'.....
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lema ameshaingia kwenye dimbwi lile lile la kupenda sifa ambalo Mrema alikuwa anaogelea miaka kadhaa iliyopita. Lema hashauriki wala hatashaurika kwamba "anakosea" na kwa bahati mbaya kama ilivyokuwa kwa Mrema naye pia amezungukwa na "wapambe" wanaomwimbia nyimbo za "ndiyo Mzee!!"
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Lema ni "mtu makini"
   
 12. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hilo ndilo lengo lao!
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wasianzishe chama kwa misingi hiyo, watakuwa wanafanya kosa kubwa. kama wanabaguliwa katika vyama sasa hivi kwa ajili ya ujana wao, na wao wakaamua kuungana kama vijana na kuanzisha chama, watakuwa wanathibitisha ule ubaguzi kwa sababu na wao watakuwa wanwabagua wazee... watakuwa na tiofauti gani nao kwa dhambi hiyo ya ubaguzi.

  Lakini, chama cha siasa ni kitu kikubwa zaidi ya ujana. nadhani kinapaswa kuwa chombo kinachowakilisha maslahi ya wengi. Ni kweli chama kinashauriwa kuwa na mrengo wake, lakini kuanzisha chama cha vijana kutokana na dhambi ya kuwabagua vijana, sidhani kama ni mwanzo mzuri wa kujenga chama chenye kuwakilisha maslahi ya wengi
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Waanzishe tu,watanzania tutawahukumu kwa unafiki wao.Tena napendekeza Bashe ndio awe mgombea wa urais,ili Rost tamu
  asikasirike!
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Gaijin upo serious? Hebu msome Kigarama. Kwa mtazamo wangu, na ni baada ya kusoma tamko lake, Lema ni mfuata upepo!
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hivyo ndivyo alivyojiita mwenyewe kwenye tamko lake juu ya sakata hili la Kafulila

  "....Kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako,...."

  Akipongeza uamuzi wa NCCR-Mageuzi
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa hapo wafuasi wake si watu wa kuonewa huruma kwa kweli???
  yaani kuna watu wanafikia mpaka kushauri Lema agombee urais mwaka 2015..
  hii nchi ina vituko vipya kila siku
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hii thread ina maneno mazito sana.kama huna la maana ku comment,ni vyema usome comment za wenzako upite..si lazima uandike plz.
   
 19. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Vyama vyetu vyote vina mapungufu makubwa..lakini hapa naona watu wana uchu wa madaraka tu akuna kingine,wanaona kwenye vyama walivyo sasa wanachelewa...tuone wakishaanzisha icho chama kama kila mwanachama akizinguliwa ndani ya chama atakuwa anaitisha press conference kukosoa viongozi wake..tunakisubiri.
   
 20. fige

  fige JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama tuko kwenye ndoa ,mmojawapo anatoa ya ndani nje ya ndoa,je tuseme huo ni uhuru wa kufikiri ?
  Mara nyingi ukiona hivyo kuna mawili;-
  1.Huyo anayebwabwaja nje ana lake jambo analolitafuta na kwa kufanya hivyo anataka kulihalalisha,inawezekana ikawa kwa uzuri au ubaya au ubinafsi.

  2.Huko ndani ya ndoa hakuna nafasi(uhuru)wa kuongea .Ni kama mpira unaojazwa hewa ,ikizidi,itapasua mpira na maana yake hewa itatoka.
   
Loading...