Zitto Kabwe: Watu wameumizwa sana na ‘Wazalendo’, Nataraji CAG atafanya Ukaguzi Maalumu kwenye Mradi wa Bandari ya Tanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
961
1,000
Salaam Wakuu,

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT WAZALENDO, Zitto Kabwe ameshangazwa na Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga.

Akiandika kwenye Mtandao wa Twitter amesema:

"Mwaka 2019 Mamlaka ya Bandari Tanzania iliingia Mkataba wa USD 172M na Kampuni ya China Harbour Eng Ltd wa upanuzi wa Bandari ya Tanga. Baada ya Mwezi Kampuni hiyo ikaipa kazi hiyo hiyo kampuni nyengine ya CCCC-Tianjin Dredging kwa Gharama ya USD 16M! CAG hukuona hili?"

" Gharama za Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Tanga zimefikia zaidi ya TZS 500 Bilioni. Mzabuni alipewa kazi ‘ikiaminika’ kuwa Eneo ya kuchimba lina mwamba."

" Mkandarasi akakuta lina tope tupu. Meneja wa Bandari Tanga alipohoji makao makuu, akahamishiwa Kigoma kisha akafukuzwa Kazi!"

" Watu wameumizwa sana na ‘Wazalendo’ waliokuwa wanajificha kwenye kichaka hicho kufanya ubadhirifu. Nataraji CAG atafanya Ukaguzi Maalumu kwa Mradi huu wa Tanga na kuchukua hatua stahiki Pamoja na Miradi mingine yote ambayo ilikuwa inatumika kufanya ubadhirifu wa Fedha za Umma". Mwisho wa Kunukuu.

Je, nini maoni yako kutokana na hiki alichokisema Zitto Kabwe?

Screenshot_20210430-060755.png
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
55,461
2,000
Tumechoka kusikia habari za ufisadi,ubadhirifu,wangekuwa wanazipotezea
Tu

Ova
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,263
2,000
Hii inatokana na tabia ya kudharau maandalizi ya awali kama feasibility studies, environmental and social impact assessments, geotechnical surveys, preliminary designs n.k. kwa kisingizio kuwa inapoteza muda na ni njia ya washauri kula. Watu makini wanatoa muda wa kutosha kuchunguza na kupanga kabla ya kutekeleza lakini sisi tunakimbilia kutekeleza bila kujipanga vizuri.

Amandla...
 

King klax

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
3,333
2,000
Kazi tunayo jamani mm na chama changu tumekula tayari keki ya taifa,, tuwaachie wengine walepo keki
 

DURACEF

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
976
1,000
Tanzania ina vitu vingi sana vya kipuuzi....hivi kweli watu wanahamasishana kulipa kodi huku wengine wanachezea tu......
Huu ni ushenzi sana.
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928
1,000
Zito Kabwe ni kama mbowe tu haaminiki na taarifa zake, hata ndege alituambia ni mitumba haitaweza kupaa.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,920
2,000
"Mradi wa kimkakati" neno hili lilizaliwa awamu iliyopita kwa lengo la kutupiga huku tukipumbazwa

Mwamba JPM aliangushwa na wasaidizi wake
 

Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
723
1,000
Zito Kabwe ni kama mbowe tu haaminiki na taarifa zake, hata ndege alituambia ni mitumba haitaweza kupaa.
Thibitisha unakinzana na hoja yake kwa kutoa hoja juu ya anachosema zzk, otherwise rudi kwa waliokutuma waambie nimefukuzwa Jamiiforum wanasema kichwani kwangu kumejaa mbung'o.
 

hatanasio

Member
Apr 12, 2021
20
45
Zito haaminiki kabisa anatoa taarifa za uzushi hata aliweza kuisaliti CHADEMA wakamtimua kwa usakatonge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom