Zitto Kabwe: Wahariri waulizeni CHADEMA wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe jela

Zitto Kabwe amesema:

"Sakata la Freeman ni moja kati ya vitu vinavyoniumiza sana, Freeman amenilea, ninavyomuona yupo jela simuoni kama Mwenyekiti wa CHADEMA, namuona kama Kaka yangu, nimefanya jitihada kuhakikisha anatoka Jela na kila nilichofanya kina ruhusa ya Mbowe, nimeenda Jela na nimeongea nae kumuambia nataka kufanya hivi akaniambia fanya"

"Wao wanamuona Mwenyekiti wao yupo Jela Mimi namuona Kaka yangu yupo Jela huo ndio utofauti, Wahariri waulizeni wenzetu wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe nje ya Jela, Mimi naamini tulichofanya Dodoma (kumuomba Rais Samia amsamehe Mbowe) isingeleta kelele zilizopigwa, leo tungekuwa na Mbowe nje, naamini hivyo"
hakika mbowe angekuwa nje tatizo hao wanao amini wanaweza kutunishiana misuli na serikali ndiyo shida
 
Zitto Leo unaamini Connection yako na Rais Samia itaweza kumtoa Mbowe Gerezani..??? Na hio ndio unaita juhudi.
 
Zitto Kabwe kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo amewambia wahariri wa vyombo vya habari kuwa amefanya sana jitihada kumtoa Mbowe jela na Mbowe mwenyewe alibariki jitihada za Zitto kupambana kumtoa jela.

Zitto anasema kuwa CHADEMA wanamuona Mbowe kama mwenyekiti yeye ana muona kama kaka yake ambaye yuko gerezani!

Zitto ametaka wahariri wawatafute viongozi wa CHADEMA wawaulize wamefanya jitihada gani kumtoa Mbowe jela?

My opinion!

Zitto anaona wazi kuwa njia ya Chadema kutumia mahakama kumpambania Mbowe haiwezi zaa matunda kamwe na ana hakika haitozaa na ndio maana anaona njia ya kumuombea msamha kwa Rais ndio njia bora na anawaona Chadema hawafanyi lolote liwezekanalo kumtoa Mbowe!

Zitto anaona Mbowe amefanya kosa tofauti na sisi tunavyo ona? Zitto anajua zaidi kuzidi sisi?

Zitto anawezaje kujitenga na hoja ya kutaka kutumika na CCM kama daraja la kumtafutia Rais umaarufu....kwa kutengeneza tatizo na kulitatua na kujipigia makofi?

Zitto ni kweli anaamini Mbowe ni gaidi?

=========

Zitto Kabwe amesema:

"Sakata la Freeman ni moja kati ya vitu vinavyoniumiza sana, Freeman amenilea, ninavyomuona yupo jela simuoni kama Mwenyekiti wa CHADEMA, namuona kama Kaka yangu, nimefanya jitihada kuhakikisha anatoka Jela na kila nilichofanya kina ruhusa ya Mbowe, nimeenda Jela na nimeongea nae kumuambia nataka kufanya hivi akaniambia fanya"

"Wao wanamuona Mwenyekiti wao yupo Jela Mimi namuona Kaka yangu yupo Jela huo ndio utofauti, Wahariri waulizeni wenzetu wana mikakati gani ya kumtoa Mbowe nje ya Jela, Mimi naamini tulichofanya Dodoma (kumuomba Rais Samia amsamehe Mbowe) isingeleta kelele zilizopigwa, leo tungekuwa na Mbowe nje, naamini hivyo"

Anaota ndoto na mwendelezo wa ndoto ni huu hapa:

IMG_20220304_161122_491.jpg

Kama si ndoto basi ni ugonjwa usiokuwa na tiba.

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom