ZITTO KABWE vs JULIUS MTATIRO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZITTO KABWE vs JULIUS MTATIRO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 3, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wadau Zitto Kabwe na Julius Mtatiro wana nafasi zinazofanana ndani ya vyama vyao wote ni manaibu katibu wakuu Tanzania bara.Lakini kwa siku za karibuni Julius Mtatiro anaonekana kuwa msaada mkubwa kwa chama chake na kukijengea mtazamo chanya kwa wananchi.Chadema inaonekana kama haina naibu katibu mkuu kwani kila mara ni lazima tamko lolote rasmi la kichama atoe Katibu mkuu au mkurugenzi wa mambo ya nje John Mnyika.Je ina maana hakuna umuhimu wowote wa chadema kuwa na Naibu katibu mkuu bara?? Au kikatiba hii nafasi haimpi madaraka makubwa ya kitaifa kama kwa chama cha CUF??. Inasemekana Naibu katibu mkuu wa Chadema bara anaonekana ofisi za makao makuu ya chama wakati wa vikao vya kamati kuu tu...Je tupendekeze hii nafasi Chadema ifutwe?? Chadema isipokuwa na mtu mahiri wa kutoa matamko ya kichama kila siku hakika itafunikwa na CUF siku si nyingi.Haiwezekani kumtegema Katibu Mkuu kila siku azungumze...yeye anapaswa kutoa matamko maalum tu kwani hakika kwa sasa hivi DR Slaa ndiye kiongozi mkuu wa upinzani Tanzania angalau kwa sasa,hawezi kuwa msemaji wa chama kila siku wananchi watamchoka haraka...Nawasilisha...
   
 2. P

  PATAKUCHA TU New Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zittto = Katibu Mkuu wa Daruso (Waziri Mkuu sasa)
  Mtatiro = Waziri Mkuu wa Daruso.

  Zitto = Mbunge.
  Mtatitiro = Si Mbunge.

  Zitto = Uthubutu.
  Mtatiro = Uthubutu.

  Zitto = Naibu Katibu Mkuu CHADEMA.
  Mtatiro = Naibu Katibu Mkuu CUF.

  Zitto = Mshauri wa Rais wa Ujerumani masuala ya kiuchumi kusini mwa jangwa la sahara.
  Mtatiro = Hakuna.

  Zitto = Hakurupuki.
  Mtatiro = Ana kurupuka.

  Zitto = Misimamo ya hoja za ni za political-academic
  Mtatiro = Hawezi kujenga hoja za kisiasa tu.

  Zitto = Ana mtoto nje ya ndoa na Jack.
  Mtatiro = Ana mtoto nje ya ndoa na Emmy.

  Zitto = Muislam.
  Mtatiro = CUF.

  Zitto = Shahada ya uzamili - uchumi.
  Mtatiro = Shahada ya kwanza - Ualimu.

  Zitto = Kijana pekee aliyepitia misukosuko ya kisiasa kuliko vijana wote Tanzania - 2005 - 2010.
  Mtatiro = Hakuna.

  Zitto = Too ambitious hata kama anawauza wenzake. hana tamaa ya utajiri, bali anataka kuona mission and vision zake zinatakelezwa kwa njia na gharama zozote.
  Mtatiro = not too much ambitious.

  Zitto = Hufikiri ndipo hutenda.
  Mtatiro = Hutenda ndipo hufikiri. too mechanical.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280

  Crap,...... naomba jina la naibu katibu mkuu wa CCM hapa.
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimpigie simu jamaa yangu yuko pale Exim bank!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Duu..... mkuu ... safari yako hapa JF itakuwa kali ..... post ya kwanza kabisa....... ina makali hivyo..... basi mimi nimebahatika kuwa mtu wa kwanza kabisa kukupa ka thanks........
   
 6. S

  Shkh Yahya Senior Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimecheka mno na hii compare and contrast..yaani you made my day!!!very funny and interesting.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Zitto = Ana mtoto nje ya ndoa na Jack.
  Mtatiro = Ana mtoto nje ya ndoa na Emmy.

  Huu ni ushamba, sasa sisi inatuhusu nini mambo yao ya familia?
   
 8. C

  Calipso JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hapa naweka ushabiki upande, mtatiro nyota yake ndo sasa inaanza kupaa tena kwa kasi,lkn zitto yupo juu kwa sasa tena sana, lkn chadema wakifanya mchezo kijana wetu JULIUS MTATIRO atawafunika, na mimi binafsi namkubali mtatiro.. lkn wote ni kutoka vyama vya upinzani,so muhimu ni kuhakikisha CCM INANG'OKA TU...
   
 9. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Karibu,
  Hongera kwa uwiano uliouanika hapa jamvini.
   
 10. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  yahaaa hiyo imekaaa vizuri sana:whoo::whoo::whoo::whoo:
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwel patakucha
   
 12. T

  The Informer Senior Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umejaribu kumpamba rafiki yako Zitto, lakini ukweli unabaki palepale kuwa Zitto amejiharibia yeye mwenyewe kwa tamaa zake za utajiri, madaraka na umaarufu.

  Mtatiro is a rising star in Tanzanian politics. Si mbunge lakini ni maarufu kutokana na kazi zake na anakisaidia chama chake. Kosa alilofanya ni la kiufundi tu, aligombea jimbo la Ubungo ambalo Mnyika amejiweka sawa kwa miaka mingi. Laiti angeenda jimbo la Temeke, Kigamboni au Kinondoni, sasa hivi angekuwa ni mbunge.

  Ushahidi kuwa Zitto ana tamaa ya utajiri: Msimamo wake wa kifisadi kwenye Dowans/Richmond, TICTS na TANROADS. Pia alipewa pesa nyingi na mafisadi kujaribu kumng'oa Freeman Mbowe kama mwenyekiti wa Chadema. Anaeleweka vizuri kuwa hana maadili ya uongozi, ndiyo maana viongozi wenzake wa Chadema wamemshtukia. Ataishia kwenda CCM akajimalize huko kisiasa. Zitto Kabwe yuko kwenye payroll ya Rostam Aziz, hilo linafahamika wazi.

  Hayo mambo mengine ya kuzaa nje ya ndoa, etc ni kukosa hoja tu za msingi.

  Mtatiro ni jembe la uhakika, inabidi ahamie CHADEMA achukue nafasi ya Zitto.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280

  Yaani kabisa unajidanganya mwenyewe kwamba huyo ni mgeni? basi umeliwa huyo ni mwenyeji kuliko wewe, na usikute yupo na zitto karibu sana, mimi nimemchukia kwa unafki wake tu wa kumdiscolyfie mtatiro kwa kila jambo this is not fair, mimi sio supporter wa Cuf lakini post za kizembe na kujipendekeza za huyu bwana haziwezi support kutoka kwangu hata siku moja. Labda naomba anijibu swali dogo tu katika vijana ambao ni wahanga wa siasa mbovu, Zitto amewahi kufungwa jela ipi? pili kuna ulemavu wowote wa kudumu au majelaha aliyopata toka 2005 mpaka 2010? kama hana majibu ya maswali haya tafadhali afunge domo lake, sisi wengine tumeshaweka maisha yetu rehani kwa ajili ya kupinga dhuluma na sio kutafuta umaarufu.
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.... kweli leo mtanichanganya..... sasa nimwamini nani jamani.......? nikikubaliana na wewe mwingine nae atkuja sema wewe umetumwa na mtatiro....
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  wewe ndo zito?
   
 16. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Siku hizo Zitto Kapotea kama mrema hivi
  Muda si mrefu ataanza kuvaa suti na kandambili kama mrema
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu. ngoja kidogo..... nimeanza kukuamini sasa....... kwa sababu gani....... nimegundua aliyeanzisha topic hii ndio yule yule aliyechangia wa kwanza kwenye thread...... je ni kweli...?
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi,
  Heri ya mwaka mpya.

  Mtatiro na Zitto kabwe ni vijana bado wachanga katika anga za siasa wanahitaji mambo mengi ya kujifunza kabla hawajakabidhiwa madaraka makubwa waliyonayo sasa [Naibu katibu mkuu].

  Mheshimiwa Zitto Z kabwe kaanza siasa zamani kidogo [miaka mitano] ukimlinganisha na Mtatiro ambae kajaribu kugombea ubunge kwa mara ya kwanza.Mheshimiwa Zitto amepoteza mwelekeo wake wa kisiasa hajulikana anachokifanya CHADEMA pengine angekimbilia CCM angeeleweka vizuru zaidi kuliko kubaki CDM ambako wamemstukia si mwenzao.Zitto alianza kupoteza mwelekeo alipokubali uteuzi kamati ya madini alibadilika kabisa alifika wakati alikuwa akiunga mkono Dowans wazi wazi.

  Mtatiro kapewa unaibu katibu mkuu kubalance mambo CUF.Muda aliotumikia wadhifa wa Naibu katibu mkuu ni mfupi sana kumuhukumu kwa wema au ubaya.Maandamano ya CUF ya kudai katiba mpya ni moja ya mambo yaliyompatia sifa kubwa ndani ya nchi na kimataifa.Vyombo vya habari vya kamataifa Al Jazeera na Euro news vimesaidia sana kijana Mtatiro kujulikana sehemu mbali mabali duniani.Mtatiro anaweza kuisaidia sana CUF kujipenyeza zaidi Tanzania bara ambako bado watu wengi wanakitilia shaka CUF.Mtatiro kaziba pengo la Lwakatare aliyetimkia CHADEMA.
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280

  Mkuu kwa kukujibu swali lako, mimi ni mtu mwenye fikra huru ambazo haziendani na ushabiki wa kisiasa, mtoa mada ametoa mada utazani yupo kwenye platform ya chadema, kumbe hii ni platform huru yenye watu wenye mawazo huru, haiitaji degree kujuwa kwamba mchango wa yule bwana ni kumdhihaki mtatiro,
  Ushauri wa bure kwa wapenzi wa vyama vya kiushindani nyote ningependa muuwelewe ukweli huu, wanachama na mashabiki karibu wote wa CCM wapo kwenye chama chao kwa sababu ya itikadi. period.
  mtu yeyote ambaye yupo kwenye chama au anasupport chama kwakumpenda mtu, basi amepungukiwa akili na hajitambuwi, na mazuzu wengi wa namna hii wanapatikana kwa wingi kwenye vyama vya upinzani.
  Humu wapiga porojo wengi ukiwauliza chadema ni chama cha mlengo gani utacheka mwenyewe, ukiwauliza ni nini falsafa ya chadema hapo ndio balaa, madudu huwezi kupewa jibu, katiba ya chadema hiyo ndio usiwaulize kabisa, lakini wao waulize Zitto ndio hapo utamjuwa mpaka aliyezaa nae, na sasa hivi hawara yake mpya anaitwa nani n.k hao ndio magreat thinker.
   
 20. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Naenda kupata lunch nitachangia nikirudi
   
Loading...