Zitto Kabwe anahitaji ulinzi

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,502
6,403
Habari wakuu,

Kutokana na hali ya kiusalama hapa nchink kuwa ndogo hasa kwa wapinzani wa mwenye nchi, ikiwemo kupigwa risasi kwa wabunge, utekaji na uepo wa kundi la kiasi lisilojulikana

Ni wazi shahiri mheshimiwa mbunge Zitto kabwe anahitaji ulinzi wa kiwango cha juu, lakini ni nani atapaswa kuwa mlinzi wa Zitto katika nchi hii yenye mapandikizi kila kona?

kwa kazi nzuri, kubwa na nzito anayoifanys mheshiwa Zitto kwa watanzania dhidi ya serikali badhilifu na gandamizi kwa wapinzani, ni bora Zitto atafutiwe ulinzi mapema sana kabla yajamkuta mengine yanayoendelea hapa nchini.

Zitto unahitaji ulinzi, huenda umejipanga na unajilinda lakini hao walinzi wako wamepia mafunzo wapi? Vipi watu wasiojulikana hawawezi pitisha mikono yao kwa hao walinzi

Zitto alindwe hata kwa gharama yoyote!
 
Hivi yule CAG yuko free au ndio Lubuva style?

Nakumbuka Lowasa na Sumaye wakati wanataka kwenda Bahari beach hotel kujiunga na UKAWA wazee wa suti nyeusi waliwazongazonga kweli ila walikomaa mpaka wazee wa suti nyeusi wakaregea.

Kwa maoni yangu tumuombee zaidi CAG maana huu muziki ni yeye ndio ameweka Cd halafu ametuachia tuucheze.

Sidhani hapa duniani kama kuna mtu ana jeuri ya kumkatalia Rais hadharani swali kama aliloulizwa.

Nimemsikiliza Dr Chegeni jana kwenye kipima joto badala ya kuonesha yeye ni mtu wa kuisimamia serikali lakini ameonesha dhahiri yeye ni dekio la executive.

Watanzania tumeliwa hatuna bunge na huyo CAG repoti ya mwakani ni lazima ataandikiwa na aliye juu.

Hivi Tanzania tumemkosea nini Mungu wa kweli?
 
Siyo Zitto tu Mkuu hata CAG ajilinde sana. Tayari kuna chuki ya kutisha dhidi yake ndani ya Serikali mpaka Bungeni wakati hana hatia yoyote ile zaidi ya kufanya kazi yake ambayo ni kwa mujibu wa nafasi yake ambayo aliteuliwa na Kikwete. Tangu jiwe liingie madarakani kumekuwepo na msukumo mkubwa kukwamisha kazi ya CAG na hata kumuondoa pia ili kiwekwe kikaragosi cha jiwe.

Taifa linayumba sana na linapitia kipindi kigumu mno tangu tupate uhuru.

naunga mkono hoja. nikikumbuka yaliyomtokea LISSU dodoma sina imani kabisa na usalama wa zitto. tunaomba waliokaribu na zitto wamwambie awe makini sana kipindi hiki.
 
WaTz wangelikuwa wazalendo Zitto angelilindwa. Lakini waTz ni wanafki, hivo ajihadhari
Hata Zitto ni sehemu ya watu wanafki tu ingawa kwa hili la kuichambuwa CAG report amefanyakazi nzuri.

Labda tu kama humjui Zitto ni kwamba yeye ni muislamu, ametoka Kigoma na ameaga kwao, yeyote atakayejaribu kumdhuru basi kwenye ukoo wao hata panya hatosalia.

Kwahiyo nikutowe hofu kuhusu Zitto huyu ana ulinzi wa kisayansi za chini ya bahari.
 
Siyo Zitto tu Mkuu hata CAG ajilinde sana. Tayari kuna chuki ya kutisha dhidi yake ndani ya Serikali mpaka Bungeni wakati hana hatia yoyote ile zaidi ya kufanya kazi yake ambayo ni kwa mujibu wa nafasi yake ambayo aliteuliwa na Kikwete. Tangu jiwe liingie madarakani kumekuwepo na msukumo mkubwa kukwamisha kazi ya CAG na hata kumuondoa pia ili kiwekwe kikaragosi cha jiwe.

Taifa linayumba sana na linapitia kipindi kigumu mno tangu tupate uhuru.
Mwangalie vizuri Profesa Assad ana sigida kubwa kwenye paji la uso, hii ni moja ya ishara kwamba huyu mtu ni swala tano.

Kwa jinsi ninavyowafahamu mimi watu wenye hamu na nia ya kuiona firdaus hata umtishe vipi huyu hawezi kupindisha ukweli, ccm wajifunze katika hili wakitaka kuendelea na wizi wao hivi vyeo wawe wanawapa makafir wala kitimoto na wanywa pombe waliojaa urafi roho mbaya na hawana khofu na Mungu.

Mimi ni Mkristo ila nawajuwa vizuri waislamu wa kweli wengi kwenye hizi nafasi wana roho za kibinadamu.
 
Zito ajilinde Mwenyewe,kama kuna mtu aliyedhoofisha upinzani nchi hii basi ni Zito,na lazima alipe gharama ya usaliti wake,mpaka awamu hii ya jiwe iishe Zito atakua ashalipa gharama za usaliti aloifanya kipindi cha JK.
 
Mungu yupo nawe Zitto katika hili,akulinde dhidi ya hila, njama na vitisho vya mafashisti.
 
Niliposikia LISSU kashambuliwa akiwa kwenye gari nilishangaa sana - mtu unalipwa zaidi tshs 12M kwa mwezi halafu unatembea na gari linaloruhusu risasi kupenya

Zipo gari nyingi mpya au used tena za bei ndogo ambazo hata ziangukiwe chuma ww unadunda tu afu mnafanya masihala. Nitoe rai kwa waovu kutotumia mwanya huo kuichanganisha serikali kupitia kupanga njama za kipuuzi.
 
Hata Zitto ni sehemu ya watu wanafki tu ingawa kwa hili la kuichambuwa CAG report amefanyakazi nzuri.

Labda tu kama humjui Zitto ni kwamba yeye ni muislamu, ametoka Kigoma na ameaga kwao, yeyote atakayejaribu kumdhuru basi kwenye ukoo wao hata panya hatosalia.

Kwahiyo nikutowe hofu kuhusu Zitto huyu ana ulinzi wa kisayansi za chini ya bahari.
2nd paragraph, you have nailed it!
 
Mwangalie vizuri Profesa Assad ana sigida kubwa kwenye paji la uso, hii ni moja ya ishara kwamba huyu mtu ni swala tano.

Kwa jinsi ninavyowafahamu mimi watu wenye hamu na nia ya kuiona firdaus hata umtishe vipi huyu hawezi kupindisha ukweli, ccm wajifunze katika hili wakitaka kuendelea na wizi wao hivi vyeo wawe wanawapa makafir wala kitimoto na wanywa pombe waliojaa urafi roho mbaya na hawana khofu na Mungu.

Mimi ni Mkristo ila nawajuwa vizuri waislamu wa kweli wengi kwenye hizi nafasi wana roho za kibinadamu.
Tunaswali nae pale NGAZIJA, hana tabu na mtu!
 
uzuri wa waislam wakiikamata imani wanaikamata kweli,unaweza hata ukahisi ni vichaa wanavyoikamata dini.ndio maana amemuumbua malaika.
 
Back
Top Bottom