Zitto Kabwe ukishinda shangilia ushindi lakini pia ukishindwa tulia jipange upya

omegas

Senior Member
Jun 3, 2018
111
137
MWANASIASA Mkongwe Zanzibar, Baraka Mohamed Shamte, amemtaka kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, kabla ya kudai kumefanyika maonevu na unyanyasaji, kwanza aileze dunia kiongozi gani wa chama chake aliyewaamrisha wafuasi wake kubeba silaha za jadi na kujiweka tayari kwa mapambano.

Pia amemtaja Zitto ni kati ya viongozi wanaotakiwa kubebeshwa lawama, kuzomewa na kupuuzwa kutokana na hotuba zake zilizotaka kuvuruga amani wakati wa kampeni.

Baraka Shamte, alitoa matamshi hayo jana kisiwani Unguja, kufuatia madai ya Zitto aliyesema kuna watu huko Pemba wameuawa, kuteswa, kupigwa na kuumizwa wakati hakuna ushahidi wa matukio hayo na hadi sasa vyombo vya dola havijathibitisha.

Pia alimtaka Zitto asidhani hakuna ushahidi wa matamshi yake alioyatoa kwenye majukwaa ya kisiasa yaliowataka wafuasi wake kuingia mitaani kinyume na sheria, kuandamana na kupinga matokeo ya Uchaguzi ikiwa chama chake hakitashinda.

“Zitto asicheze ngoma ya wachawi na wanga. Ikiwa anataka kuimba nyimbo za wanga aende ging’ingi akacheze kuliko kuimba mitaani. Asikubali kulishwa uongo na uzushi mdomoni mwake. Maneno yake yenye viashiria vya jinai yapo na iko siku yatawasuta” Alisema Shamte.

Mwanasiasa huyo, alisema Zitto asifikiri wanaoshitakiwa kwenye mahakama za kimataifa ni watawala peke yao badala yake ajue hata viongozi wa upinzani hukabiliwa na mashitaka ikiwa kuna ushahidi au matamshi yaliolenga kuvuruga amani na umoja.

“Mwenyeliti wake Maalim Seif ndiye aliyewataka vijana ACT Wazalendo kubeba mundu, mikuki, mawe, mashoka na mapanga. Akawahimiza wakusanyike kwenye barabara kuu za Michenzani, kuandamana na kupambana na polisi hadi wapewe ushindi ” Alisema.

Aidha kabla ya kutamka maneno hayo, akiwa ziarani kisiwani Pemba mwanzoni mwa mwaka huu, alisikika akisema wazi wazi mwaka huu liwalo naliwe, kama noma naiwe noma na ikitokea mtu kupigwa au kujeruhiwa asiende polisi badala yake wajibu mapigo.

Shamte alisema Maalim Seif ndiye aliyewaimbisha vijana wa ACT Wazalendo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti huku wakimuitikia hawaogopi lakini pia ndiye aliyepania kutaka kuvuruga uchaguzi kwa kuwataka wanachama wake wajitokeze kupiga kura Oktoba 27 kinyume na sheria.

Alisema Zitto anapowaomba marais wastaafu kina Joachim Chisamo, Thabo Mbeki na Ulusegun Obasanjo waje zanzibar au Tanzania huku ni kuwazubaisha na kuwapa matumaini yasiokuwepo wafuasi wao baada ya kushindwa vibaya ikiwemo na yeye kupoteza kiti cha ubunge cha Kigoma mjini.

“Kwanza Zitto ayakumbuke alioyasema kwenye majukwa. Yeye na wenzake ndio waliotaka mapema zitokee vurugu. Asidhani wanaoshitakiwa ni watawala tu bali hata upinzani unapovunja sheria hubeba msalaba wa tuhuma zote zitakazothibitika “Alisisitiza Shamte.

Vile vile alisema hata wakati akitaja idadi ya watu anaodai kujeruhiwa huko Pemba kwa kusema kwake uongo alikataa kuwataja watu waliopigwa mapanga msikitini jambo ambalo linathibitisha taarifa ya Zitto ilijaa usanii wa kisiasa anaofundishwa na Maalim Seif.
 
Back
Top Bottom