Zitto Kabwe: Uhuru Wangu wa Maoni Ulilenga Kulinda Uhuru, Haki, Hadhi na Madaraka ya Bunge

[B]Kifyatu[/B], niliamua nichukue muda nipitie japo michango yako mbalimbali ya awali kabla sijauendeleza huu mjadala na wewe na amini usiamini nimepitia asilimia kubwa tu ya michango yako yote.

Lengo langu la kupitia hiyo michango ni hamu ya kutaka kujua misimamo yako katika hoja mbalimbali zinazotolewa humu JF na baada ya kufanya hivyo nimechukua uamuzi kama ifuatavyo.

Toka sasa utakuwa kwenye orodha yangu ya ignore kwa sababu naamini watu aina yako ni hatari kwa ustawi wa jamii na mmechangia kwa kiasi kikubwa uzoroteshaji wa utawala wa sheria.

Kuliko kujadiliana na wewe ni heri kujadiliana na meza ya kulia chakula (kama kweli umeishi Marekani utanielewa) Uzuri wa hiyo meza ni kwamba haina habari na utamu/uchungu wa kilichowekwa juu yake.

Samahani sana kama hatua yangu itakukwaza, ila ninayo tabia hii ya kuchagua ni nani wa kujadiliana naye...kwaheri.

Terrible mistake kum-ignore huyu, mkabe hoja kwa hoja akimbie yeye mwenyewe. Kama huwezi nikuunfishe kukabiliana naye. Moja ya post zangu nimemjibu hivi:

List ya mafisadi ilipopelekwa bungeni nini kilitokea? Ilipita? Ilipopelekwa kwenye mkutano wa hadhara pale Mwembeyanga nini kilitokea? Au hukuwa umezaliwa?

Moja ya post zake anasema hivi:
Hii sikua nimeiona.

Ndio mkuu, umenikumbusha mbali sana. Ujana wetu tulipitia mengi.

1. Tulicheza twist na kuvaa suruwali za kubana kama zenu siku hizi mpaka mzee Kawawa (waziri mkuu) akaamua kuzitia mkasi. TUKAPONA

Najua kuna mahali ni mwongo sasa sijui ni uongo kwamba kasoma UDSM Engineering au kaongopa kwamba alivaa suruali za kubana zilizokatazwa na Kawawa.

Tuanze kuchambua ongo zote mbili. Kama kasoma Engineering basi kaongopa kwamba alivaa suruali zile akiwa kijana, pale UDSM ile Faculty of Engineering (FFOE) imeanzishwa 1974 ndipo vijana wa pale wakaingia na ku-graduate kwa mara ya kwanza 1977.

Huyu anasema ujana wake suruali zake zilibana wakatiujana ule ulikuwa wa mwaka 1962 Kawawa akiwa PM na Nyerere akiwa mbunge tu. Sasa kama hiyo 1962 tusema alikuwa na miaka 18, basi maana yake alizaliwa walau mwaka 1944.

Vijana wa mwaka huo (1944) wengi waliochelewa wali-graduate mwaka 1974 wakiwa na miaka 30 na waliowahi wali-graduate hata FOE haijaanzishwa.

Hana chochote. Huyu ni mtu ambaye yuko exposed na mambo mengi na hivyo anawez ku-argeu na ukadhani CV yake ni sahihi na ukizingatia kuwa ameficha jina lake.

Halafu hajui kudanganya. Pale FOE first class Honors zinajulikana kila mwaka kuanzia hiyo 1977 zikiwemo za akina Prof. Materu, Prof. Nzali (RIP), Mr. Ishengoma, Dr. Zaipuna Yonah na hakuna hata mmoja unayeweza kumweka katika arguments za huyu bwana.

Msubiri aje uone nitakavyomshusha.
 
Tukubaliane kwamba, mihimili yote ya serikali hutegemeana. Lakini pia, ni vyema tukakubaliana kimsingi kwamba:
1. Bunge lina mfumo wa utawala ambao huendesha shughuli za siku hadi siku;
2. Bunge lina Kamati mbalimbali ambazo, kila kamati ina wabunge kutoka kambi zote mbili;
3. Kwamba, maazimio ya bunge huamliwa kwa wingi wa kura (ama za wazi au za siri);
4. Ziara za raisi au matukio ya kimaendeleo yanayomhusu raisi yanayooneshwa mubashara na runinga mbalimbali hayawezi kufanana na kuoneshwa kwa bunge ambalo limejaa vioja vinavyodhalilisha bunge! Au muda wa matukio ya raisi yanachukua muda mfupi sana ukilinganisha na shughuli za bunge ambazo huchukua takribani siku nzima! Na kwamba haiyumkiniki akilini kutumia muda wote wa uwepo wa bunge kuangalia runinga (labda tukubaliane kwamba kwetu muda si mali).
5. Wabunge huruhusiwa kupeleka miswaada / hoja binafsi na kujadiliwa na wote.
Sasa swali langu kwa Zitto, ni je, kama hayo yote yanafanyika, inakuwaje unashindwa kuyashughulikia kibunge unayashughulikia mitaani? Huruma yetu kwako itakusaidiaje?
 
Kwahiyo kama kama mabunge ya awamu zingine/ya nyuma yalifuata maelezo ndio imegeuka sheria? Mbona Watanzania wengine mnataka kufanya tuonekane wapuuzi-puuzi tu?
Mkuu achana na huyo Kirikou Wa Kwanza hajitambui
Umezisoma hizo hoja hapo juu Mkuu ?.Hebu rudia tena kusoma na uhakikishe umeelewa vema.

Ndungai ni shiiiiida amekuwa Spika wa ndiyo toka kwa Mtukufu malaika wa Chato cha ajabu anapokea Amri za Maliyamungu Bashite ni Aibu kuwa na Spika wa hivyo
 
Vijana wazamani kama Kifyatu na wa aina kama yeye ndio wametuleta hapa tulipo sasa.Mhandisi haeleweki na anachozungumza kabisa.Nadhani wahandisi ni vizuri wahusike katika kazi za kubuni miundo mbinu na kuboresha iliyopo kwa kufuata dira kwa mahitaji ya baadae. Dar es salaam na Dodoma inawatosha kuwa busy kiasi cha kutohusika na mambo mengine la sivyo wataleta uhandisi kwenye siasa matokeo ndo haya.............unless kwa wahandisi wenye vipawa vya siasa na uongozi haiwezekani kwa kila mhandisi kujua siasa.
Na sidhani kama kukaa Marekani miaka 32 na anakuja na hoja kama hizo za ajabu ajabu.Hao ndio tuliokuwa tunawategemea kutuendeleza angalia tu comments zake.Hana na hajai kwa sisi tuliokaa Tz kwa miaka 32.Mzee rudi tu America,hukuwezi huku kabisa.Na kwanza sijui ulikuwa unahusika na nini huko America?? Kama ni ubunifu basi ilikuwa kazi ngumu sana kueleweka huko ulikokaa miaka hiyo yote. Na maadili yakuanika elimu yako sjui umeyatoa wapi anika IQ hizi elimu za publication ni taabu sana.
Mimi ni mhandisi na nadhani wewe ni mwanasiasa. Hebu niulize swali lolote lile la kisiasa unalodhani ni gumu na halikujibiwa na Magufuli.

Msiwadharau wahandisi, ndio wanaoendesha nchi sasa.
 
Kwa lugha ya kawaida, Watanzania wote milioni 50 wangetakiwa kushiriki katika mikutano ya Bunge kutunga sheria, kupitisha bajeti na kuisimamia Serikali lakini kutokana na ugumu wa jambo hilo, ukawekwa utaratibu wa uwakilishi unaotumika sasa.

Kwa utaratibu huu uliowekwa na Katiba, wananchi wakapewa mamlaka ya kuchagua wabunge katika kila jimbo, na wabunge wengine wanaopatikana kwa utaratibu mwingine, ili waweze kuchukua maoni yao, kero zao na kuziwakilisha bungeni.

Uhuru wa wananchi kuchagua wawakilishi hao kupitia vyama tofauti vya siasa ulianza katika uchaguzi wa mwaka 1995. Kabla ya hapo wabunge hao walitokana na chama kimoja kilichokuwapo – Chama cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo, licha ya wawakilishi hao kuchaguliwa chini ya mfumo unaotambulika kikatiba, katika siku za karibuni malalamiko ya upinzani kukandamizwa ndani ya chombo, na washindani wao kupendelewa yaliyokuwapo muda mrefu yamezidi kukomaa.

Wakati hali ikiwa hivyo, pia yameibuka madai ambayo pia yanazidi kukita mizizi kuwa Bunge hilo limekosa meno ya kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi.

Ingawa mara kadhaa uongozi wa Bunge umekanusha madai hayo na kutunisha misuli kuulinda muhimili huo, madai hayo yamezidi kuongezeka.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameibua hoja 10 anazodai zinaonyesha udhaifu wa chombo hicho huku akisema hali hiyo haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Wiki iliyopita, Zitto alitoa hoja hizo mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akisisitiza kuwa Bunge hilo limeingiliwa na mhimili wa Serikali, linapangiwa cha kufanya na namna ya kuisimamia Serikali.

Mengi aliyoyaeleza Zitto si mapya, yamekuwapo ya wabunge wamekuwa wakiyasema, lakini alichofanya ni kuyakusanya kujenga uzito wa hoja yake kuwa chombo hicho kimejisalimisha kwa Serikali kinyume na inavyotakiwa kuwa.

Kabla ya tukio hilo, Mbunge huyo alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Kigoma baada ya kuitwa na Kamati hiyo kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na maoni yake kwenye mitandao ya kijamii akimkosoa kiongozi huyo.

Hii si mara ya kwanza tangu kuanza kwa Bunge la 11 kwa wabunge wa upinzani kuibua tuhuma kama hizo huku wakijenga hoja zinazoakisi udhaifu wa Bunge hilo. Vilevile, hata jicho la watu walio nje ya Bunge wanaeleza hisia zao zinazoonyesha hali hilo.

Aliyekuwa Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza anasema si wapinzani tu, hata mwanaCCM wanaona na kutambua udhaifu huo lakini wamekuwa waoga wa kukiri mbele ya wananchi.

Ruhuza anasema sababu ya kutokiri udhaifu inachagizwa na woga wa wabunge wengi wa chama hicho.

“Kinachosikitisha zaidi, baadhi ya wanaCCM wanaopinga udhaifu wa Serikali au Bunge wanatengwa, si wenzao. Mfano, Nape Nnauye aliponzwa na msimamo wake wa kukosoa udhaifu wa Serikali, wabunge wengine wameamua kuangalia masilahi yao tu na huo ndiyo usaliti kwa Watanzania waliowatuma bungeni,” anasema Ruhuza.

Ruhuza anasema wananchi wanatakiwa kutambua kuwa Bunge si chombo chao bali ni chombo kinachotumiwa na CCM na Serikali yake, na kutolea mfano wa muswada binafsi wa Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia wa kutaka kuongeza muda wa ukomo wa urais na ubunge hadi miaka saba.

Anasema hata mapendekezo yaliyokuwa kwenye rasimu ya Jaji Warioba, kuhusu wananchi kumwajibisha mbunge wao na vipengele vya maadili waliviondoa.

“Kwa hatua hiyo, Bunge ni la wananchi au la CCM?” anahoji.

Ruhuza anasema matokeo ya haki wananchi kukosa taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa Serikali ili kuiwajibisha kupitia uchaguzi.

Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar, Profesa Abdul Sherrif anasema kwa mamlaka aliyopewa rais kikatiba ni hatari na vigumu kwa Bunge kuisimamia Serikali.

Profesa Sherrif anasema tatizo hilo lilibainika miaka mingi ndani ya Bunge hilo na ndiyo sababu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba ilikuwa imepunguza baadhi ya madaraka ya rais ili kuimarisha uhuru wa chombo hicho.

“Bunge linapokuwa katika hali hii ni vigumu kubadilika bila Katiba, na hali hii imekuwa ni tatizo la nchi nyingi Afrika,” anasema Profesa Sherrif.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas anakanusha madai ya Serikali kuliingilia Bunge akimtaka Zitto kuchukua hatua kama sheria zimevunjwa.

“Serikali ina majukumu yake, inatoa bajeti kwa Bunge, huko ndiyo kuingilia Bunge? Bunge linatunga sheria ndiyo tuseme linaingilia mahakama? Mahakama inapotafsiri sheria inaingilia Bunge? Hii mihimili haiwezi kufanya kazi in isolation (kwa kutengana).

Kuhusu madai Serikali kuhusika na shambulio la Lissu (Tundu), Dk Abbas anamtaka Zitto kusubiri uchunguzi wa Serikali badala ya kujadili hisia.

Kilio cha wapinzani

Siku chache zilizopita, Spika Zitto kwamba, anao uwezo wa kumzuia asizungumze ndani ya vikao vyote vya Bunge hilo hadi muda wake kumalizika.

Mbali na hilo, tayari wabunge wawili, Halima Mdee na Ester Bulaya wanatumikia hukumu itakayoweka nje ya mikutano minne ya Bunge hilo la 11 kutokana na adhabu ya Spika Ndugai kwa madai ya kukosa nidhamu.

Wabunge wengine waliowahi kusimamishwa kwa vipindi tofauti ni Zitto, Godbless Lema (Arusha Majini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Kibamba) na Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini).

Si hayo tu, Bunge la kumi na moja limeweka rekodi ya kushuhudia askari wa polisi wakiingia kuwaondoa kwa nguvu wabunge ama baada ya kutofautiana na hoja na Spika au kupinga mambo fulani ndani ya ukumbi huo.

Mei 30, mwaka jana wabunge saba wa upinzani walisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa vipindi tofauti baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni na kusababisha vurugu bungeni.

Chanzo chake

Wakati Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho anasema hali hiyo inachagizwa na uvumilivu mdogo wa kisiasa, ujana na masilahi binafsi ya vyama, mwenzake wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda anasema huo ni mpasuko unaotokana na kukomaa kwa itikadi za uchama zaidi kuliko hoja zinazojadiliwa.

Mbunda anasema hali iliyofikia ni kiti kutumia mamlaka yake kuwakomoa wapinzani wanapojaribu kuibua hoja dhidi ya chama kilichopo madarakani.

“Maamuzi yanayotolewa na lugha chafu zinazotolewa zinatafsiri wazi hali ya kutokuheshimiana. Uchama umefikia hatua ya kuharibu ladha ya Bunge. Nilitegemea kuona busara zaidi ya kiti cha Spika, kinachoendelea na vita ya kukomoana,” anasema.

Pamoja na mazingira hayo, Mbunda anaunga mkono nadharia ya kuendelea kwa misuguano hiyo akisema ni njia ya kutafuta suluhu kwa miaka ijayo.

“Kuna nadharia ya Mao Zedong, ‘contradiction’ akimaanisha kwamba, migogoro siyo mibaya, ni lazima itokee ili kujifunza kwa hapo baadaye,” anasema.

Pia, tatizo hilo linaweza kutokana na mfumo wa Bunge lenyewe na uongozi wa Bunge kuwa sehemu ya uongozi wa chama kinachotawala.

Ibara ya 62 ya Katiba ya mwaka 1977 inaeleza kuwa Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi na Bunge hilo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na wabunge.

Kwa mujibu wa ibara hiyo, Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza yote aliyokabidhiwa na Katiba huku sehemu ya pili ya Bunge ikiwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba”

Pili, kwa mujibu wa Ibara ya 66 ya Katiba ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa chini ya mabadiliko ya 5 na 14 kwamba, kuhusu aina sita za wabunge, kuna kundi la wabunge wasiozidi (10) wa kuteuliwa na Rais.

Aidha, kuna wabunge ambao ni mawaziri wanaoteuliwa na Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye huingia bungeni kwa nafasi yake baada ya kuteuliwa a Rais.

Pia, katika Bunge la sasa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alipata sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mbunge.

Kwa upande mwingine, Spika wa Bunge anayetokana na CCM anakuwa mjumbe wa vikao vyote vya juu vya chama na anaingia kwenye kamati ya wabunge wa CCM.

Suluhisho pekee

Suluhisho la matatizo hayo ni upinzani kujijenga na kuongezeka kwenye chombo hicho ili kuweka uwiano ulio sawa na pengine kuwa na uwezekano wa kumwondoa spika kama anatenda kinyume na Katiba, jambo ambalo kwa sasa haliwezekani.

Kutokana na mazingira hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufuatilia mwenendo wa Bunge, Albanie Marcosy, alikaririwa na gazeti hili hivi karibuni akisema kwa sasa hakuna uwezekano wa kumwondoa Spika au Bunge hilo kuongozwa na upinzani hadi pale Katiba mpya itakapopatikana au upinzani utakapokuwa na wabunge wengi.

Kwa mujibu wa Katiba, utaratibu wa kumwondoa Spika au Naibu Spika madarakani unatajwa katika Ibara ya 85(4) pamoja na Kanuni ya 138 (1) ya kanuni za kudumu za Bunge.

Hata hivyo, kanuni ya 138 (3), inamtaka Spika kukalia kiti wakati wa mjadala wa hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika.

Katika Bunge la Kumi, wabunge wa upinzani akiwamo Tundu Lissu waliwasilisha hoja tisa za kumwondoa madarakani Job Ndugai (wakati huo akiwa naibu spika), lakini hadi Bunge hilo linavunjwa hakuna hata hoja moja iliyojadiliwa.

Juni mwaka jana, Spika Ndugai aliwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ombi la Ukawa la kumng’oa naibu wake Dk Tulia baada ya wapinzani hao kuainisha hoja sita za kumng’oa madarakani kutokana na kuvunja kanuni za Bunge hilo, kuonyesha upendeleo, kutumia lugha za maudhi na kuonyesha upendeleo kwa wabunge wa CCM, ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.

Chanzo: Mwananchi
 
Zitto kajenga utetezi mzuri hapa ndipo tutaona mamlaka za kamati za kibunge dhidi ya upendeleo kwa spika kama hawata angalia hoja makini hizi.
 
Mimi ni mhandisi na nadhani wewe ni mwanasiasa. Hebu niulize swali lolote lile la kisiasa unalodhani ni gumu na halikujibiwa na Magufuli.

Msiwadharau wahandisi, ndio wanaoendesha nchi sasa.

Kuendesha nchi sio hoja, hoja ni wahandisi kuendesha nchi kwa tija.
 
Back
Top Bottom