Zitto Kabwe: Uhuru Wangu wa Maoni Ulilenga Kulinda Uhuru, Haki, Hadhi na Madaraka ya Bunge

Well done Mheshimiwa Mbunge. Umejitetea vizuri, na umetetea uhuru wa kutoa maoni. Wako mambumbu wengine siku hizi wamejiaminisha kabisa kwamba sisi Watanzania hatuna uhuru wa kutoa maoni.

Kama maoni yako ni Spika Ndungai ni mpumbavu basi hayo ni MAONI, na una ruhusa ya kuwa nayo, na kuyasema. Hata mimi naona Spika Ndungai amekuwa mtupu sana. Sana kabisa.

Nashukuru Mungu kuona taifa langu lina viongozi vijana shupavu, wakiwa ni pamoja na Tundu Lisu, Zito Kabwe, Halima Mdee, Godbless Lema na wengineo. Mungu awabariki, na awalinde dhidi ya watu wasiojulikana.

Like Mag3, I am neither Chadema nor CCM. I have never been a member of a political party. Mtanzania, basi. Inatosha.
 
Asante sana kwa response yako. Nitajihidi nijibu hoja zako kama ulivyozitoa...muda tu ndio kikwazo. Hata hivyo utumiaji wako wa nyie Chadema umenishangaza na kuniacha hoi kidogo.

Ni kweli mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM kwani kwa hali tuliyo nayo kama taifa sina wa kumlaumu bali CCM na naamini mtu yeyote mwenye akili timamu akijaribu kuvihusisha vyama pinzani na hali tuliyo nayo kama taifa sitamuelewa.

Hatujawahi kuwa chini ya serikali yoyote zaidi ya CCM na kwa Katiba tuliyo nayo hakuna kinachoweza kutendeka hapa nchini bila baraka za CCM na hata kama kuna uhalifu umefanywa na kikundi chochote, dola ni ya CCM.

Nasikitika kukufahamisha kwamba mimi si Chadema ingawa nimewaunga mkono kwa nyakati tofauti kwa jitihada zao za kuikosoa serikali ya CCM inapokosa dira na kuanza kulipeleka taifa kusiko.

Nasoma tu habari za Chadema kama unavyozisoma na ili tuweze kuwa na majadiliano mapana na chanya, nakuomba ufute kabisa hiyo dhana ya kunihusisha na Chadema kama mwanachama.

Nitarudi nikipata nafasi...

Samahani. "Nyie CDM" haikumaanisha wewe personally bali wanachama na wafuasi wote wa CDM.

Hapa tukizungumza tuhuma za Lissu kwa serikali tunazungumzia mashinikizo yanayotolewa na CDM, wanachama wake, pamoja na wale wasiokuwa wanachama lakini wana-sympathize na CDM dhidi ya serikali.

Wanachama wengi wa CCM walikwishachoshwa na uongozi wa chama chao hapo nyuma. Lakini sarakasi walizofanya CDM kwenye uchaguzi wa 2015 kuliwachosha wengi. Ushindi ulikuwa wa CDM mpaka yale madili yalipofanywa.

Kwa hiyo sisi wote tusio na vyama tunaangalia sifa za kiongozi anaenadiwa na sio chama chake. Ilani zote za vyama vya siasa TZ ni nzuri sana ukizisoma lakini utekelezaji wake ndio uliokuwa na mushkher.

Kuchagua kati ya Lowassa na Magufuli was a no-brainer. Wengi walichagua kiongozi bora na sio chama. Kwa hiyo tukiona watu wanamkubali Magufuli, sio dalili kuwa wanaikubali CCM, hapana ni kuwa wanamkubali Magufuli na uongozi wake. Tutegemee CCM nayo itarudisha mvuto wake wa awali.

Nasubiri utakapopata nafasi tuendelee na mjadala.
 
Una uhakika ni wapinzani tu wenye hisia hizo? Je, wanasheria wa US unakoishi na wa Britain nao ni wapinzani? Je, unadhani katika CCM hakuna wanaowanza hivyo?
Vyama vya sheria vya nje vimesikitishwa kwa shambulio hili. Wameitaka serikali iwatafute wahalifu wahusika. Hawajaishutumu serikali ya Magufuli kuhusika na shambulio lile.

Sasa nikuulize wewe. Hivi unadhani hakuna wanaohisi kuwa CDM wenyewe wanahusika na shambulio lile?
 
Sera hizo za wapinzani wakazitolee katika uwanja gani wakati shughuli za siasa zimepigwa marufuku?
Kwa nini hawaleti hoja hizo bungeni? Au kama bunge hawaliamini kwa nini badala ya kutukana (na kupinga kila kitu anachofanya Magufuli) majukwaani, mitandaoni na kwenye mikutano majimboni hawazileti hizi sera mbadala watu wakazikia?

Kelele zote tunazozisikia toka kwa viongozi wa upinzani yani hawawezi kuchomekea hata vito vichache vya sera zao?
 
Kifyatu,

don't distort the debate to create anarchy. The discussion here is about ten points submitted by Zitto Kabwe in the parliamentary committee, something which you never talk about.
People keep dragging me into Lissu's case and I have to respond to those inquiries. This is why I digressed from Zitto's points.

With regard to the 10 points raised by Hon. Zitto, there are very simple responces to each one of them. Already I have with me written responses.

You may notice I already have given terse answers to Mr. Zitto's point 6 and 7 in response to direct questions asked by members in this thread.

My full responces to the 10 points are rather long and verbose. At the moment I choose to hold on to them. I will find a suitable time and venue to release them.

This is Zitto thread for now, full of supporters and admirers. I don't want to rain on his parade.
 
Mkuu, hakuna watu wanaotishiwa hapa ila kuna watawala walaghai wanaotishika. Na sababu ya kutishika kwao? Ni wanafiki, wanakiuka katiba, na ni waovu wa kupindukia.
Mkuu katiba ya TZ ina mapungufu mengi na yanahitaji marekebisho.

Lakini kwa sasa Rais hajakiuka katiba. Na kama ni kweli Rais amekiuka katiba kwa nini wanasheria wabobezi wa upinzani hawaiburuti serikali mahakamani kwa kosa hili?

Tumesikia sana unguli wa Lissu katika sheria. Kwanini asilivalie njuga hili kosa na Rais kuvunja katiba mahakamani?
 
Nilichojifunza katika umri wangu na uzoefu wangu Wahandis ni watu makini wenye fikira pevu starajii wahandisi wakiwa na Ubabaishaji hata kwa mambo yaliyo bayana, mambo yasiyo hitaji mzani kuyapima,.
Nikutakie siku njema

Sijui kama wewe ni mhandisi lakini wahandisi, kutokana na rigorous training yetu katika math na engineering basi tunakuwa logical katika fikira zetu. Critical thinking ndio hallmark ya taaluma zetu.

Kwa hiyo tunapojadili kitu, hata kama hakiko kwenye fani yetu huhakikisha tunachochangia ni logical. Hakuna ubabaishaji hapa. Hii haina maana tupo sahihi wakati wote, la, lakini itakuhitaji ujipinde kujibu hoja zetu logically.

Hiki ndicho ninachofanya hapa. Kuna migongano ya mitizamo, mimi ninatoa hoja zangu na mwengine atoe hoja zake halafu tuone hoja zipi zina uzito.
 
Samahani. "Nyie CDM" haikumaanisha wewe personally bali wanachama na wafuasi wote wa CDM...

Nasubiri utakapopata nafasi tuendelee na mjadala.
[B]Kifyatu[/B], niliamua nichukue muda nipitie japo michango yako mbalimbali ya awali kabla sijauendeleza huu mjadala na wewe na amini usiamini nimepitia asilimia kubwa tu ya michango yako yote.

Lengo langu la kupitia hiyo michango ni hamu ya kutaka kujua misimamo yako katika hoja mbalimbali zinazotolewa humu JF na baada ya kufanya hivyo nimechukua uamuzi kama ifuatavyo.

Toka sasa utakuwa kwenye orodha yangu ya ignore kwa sababu naamini watu aina yako ni hatari kwa ustawi wa jamii na mmechangia kwa kiasi kikubwa uzoroteshaji wa utawala wa sheria.

Kuliko kujadiliana na wewe ni heri kujadiliana na meza ya kulia chakula (kama kweli umeishi Marekani utanielewa) Uzuri wa hiyo meza ni kwamba haina habari na utamu/uchungu wa kilichowekwa juu yake.

Samahani sana kama hatua yangu itakukwaza, ila ninayo tabia hii ya kuchagua ni nani wa kujadiliana naye...kwaheri.
 
Huyu Mhandisi kifyatu anadhani anaongea na watoto. Kwa aina ya sifa alizojimwagia kuhusu elimu yake na miaka aliyotaja kupata hiyo elimu anaonekana ni mzee. Cha ajabu nchi hii ilifikia pabaya huku yeye na Magufuli wakiwa kimya kabisa huku nchi inaliwa, leo ndio wameamka wakiwa wamechelewa sana wako harusini wanalazimisha kukaa viti vya mbele. Haya ndio mazee yaliyojaa unafiki pindi yakipata mlo yanakaa kimya hata kama mambo yanaharibika. Kwa taarifa yake huyo mzee kifyatu ni mnafiki wa kiwango cha kutupwa akae pembeni vijana wanaojitambua wafanye wajibu wao. Yeye ujana wake alikula na vimada huku nchi ikiliwa na viongozi waliokuwa madarakani, inshort huyo mzee ni bendera fuata upepo.

Cc: kifyatu.

Hii sikua nimeiona.

Ndio mkuu, umenikumbusha mbali sana. Ujana wetu tulipitia mengi.

1. Tulicheza twist na kuvaa suruwali za kubana kama zenu siku hizi mpaka mzee Kawawa (waziri mkuu) akaamua kuzitia mkasi. TUKAPONA

2. Tukaingia kwenye enzi za mabugaluu na raizoni huku akili zikivurugika na disco mania, mabolingo na macountry kama ya Skita Njau, halafu utitiri wa wakina Abba, UB40, Jackson 5s, n.k. TUKAPONA.

3. Tukaingia enzi za suruali za marinda na turn-ups na mchanganyiko wa miziki. Hapo tuliona hip-hop, rap, techno kuwa ni za vijana lakini tukawa tunasikiliza kwa chaati sana. Siasa za ushindani zilianza hapa. Lakini pia TUKAPONA.

4. Sasa tumerudi full circle. Suruali za kubana zilizotiwa mikasi na mzee Kawawa zimerudi in full force. Mimi mpenzi sana wa muziki wa bongo fleva. Lakini collection yangu ya mabolingo siitupi. Nikitaka kujisikia kijana tena huzisikiliza. Hapa vyama vya kipinzani vikaanza kuwa kama maadui. Nchi inachukua sheria za mwituni "kill or be killed". HAPA SIJUI KAMA TUTAPONA.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Kwa nini hawaleti hoja hizo bungeni? Au kama bunge hawaliamini kwa nini badala ya kutukana (na kupinga kila kitu anachofanya Magufuli) majukwaani, mitandaoni na kwenye mikutano majimboni hawazileti hizi sera mbadala watu wakazikia?

Kelele zote tunazozisikia toka kwa viongozi wa upinzani yani hawawezi kuchomekea hata vito vichache vya sera zao?

Mzee kifyatu nikikuambia ww pamoja na elimu yako unaishi kwa hasara sidhani kama nitakuwa nakukosea heshima. Umeambiwa wapinzani wananyimwa nafasi ya kufanya siasa nchi nzima ww unasema walete sera zao mtaani tuzielewe.

Huko bungeni unasema wapeleke sera zao, sitaki kuamini hili unaweza kulizungumza hadharani, mbele ya spika wa ccm akupe nafasi ya kuonyesha sera zako mpinzani mpaka wananchi wakuelewe? Kwenye bunge ambalo waziri au mbunge akiongea anaambiwa aongee kwa kifupi kwa sababu ya muda? Kweli sio bure nchi yetu ni masikini na ww unathubutu kuweka elimu yako hapa hadharani bila aibu.
 
[B]Kifyatu[/B], niliamua nichukue muda nipitie japo michango yako mbalimbali ya awali kabla sijauendeleza huu mjadala na wewe na amini usiamini nimepitia asilimia kubwa tu ya michango yako yote.

Lengo langu la kupitia hiyo michango ni hamu ya kutaka kujua misimamo yako katika hoja mbalimbali zinazotolewa humu JF na baada ya kufanya hivyo nimechukua uamuzi kama ifuatavyo.

Toka sasa utakuwa kwenye orodha yangu ya ignore kwa sababu naamini watu aina yako ni hatari kwa ustawi wa jamii na mmechangia kwa kiasi kikubwa uzoroteshaji wa utawala wa sheria.

Kuliko kujadiliana na wewe ni heri kujadiliana na meza ya kulia chakula (kama kweli umeishi Marekani utanielewa) Uzuri wa hiyo meza ni kwamba haina habari na utamu/uchungu wa kilichowekwa juu yake.

Samahani sana kama hatua yangu itakukwaza, ila ninayo tabia hii ya kuchagua ni nani wa kujadiliana naye...kwaheri.
Yes Sir.

Nilifikiri umepitia hoja zangu halafu ukakutana na matusi na kejeli tu. I am glad hukuona utusi wowote. I write clean.

Kama utanipuuzia na kutojadili hoja zangu kwa sababu unaona ninakupotezea muda wako, hii ni haki yako. Power to you.

I hope our paths cross again under more favourable circumstances.

So long for now.
 
Mzee kifyatu nikikuambia ww pamoja na elimu yako unaishi kwa hasara sidhani kama nitakuwa nakukosea heshima. Umeambiwa wapinzani wananyimwa nafasi ya kufanya siasa nchi nzima ww unasema walete sera zao mtaani tuzielewe.

Huko bungeni unasema wapeleke sera zao, sitaki kuamini hili unaweza kulizungumza hadharani, mbele ya spika wa ccm akupe nafasi ya kuonyesha sera zako mpinzani mpaka wananchi wakuelewe? Kwenye bunge ambalo waziri au mbunge akiongea anaambiwa aongee kwa kifupi kwa sababu ya muda? Kweli sio bure nchi yetu ni masikini na ww unathubutu kuweka elimu yako hapa hadharani bila aibu.
Hivi hawa wakina Lissu, Mdee, Kubenea, Zitto, Lema, Mbowe, Msigwa, Lowassa, Mnyika, na wengineo waliofanya mihadhara nje ya bunge mpaka wengineo wakaingia matatani kwa utusi au kejeli waliwezaje kufanya hivyo na washindwe kunadi sera zao mpya?

Kila leo wanasiasa wa upinzani wanazungumza na wananchi kupitia mikutano, vyombo vya habari na mitandaoni. Hawawezi kutumia hizi fursa kuelezea siasa zao mpaka wafanye maandamano nchi nzima?

Wapinzani hawako serious kujijenga kisiasa ili wakubalike na Watanzania kama ilivyokuwa kabla ya 2015. Wao wanataka kuibomoa serikali ya Magufuli ili wapate political points wakidhani hicho kitawainua kisiasa.

Hata ingekuwa CDM ndio imeshika dola halafu CCM (kama upinzani) wafanye wanachokifanya CDM sasa wasingekubali.

Nilikwisha sema hapo nyuma kuwa kujaribu kuubomoa utawala kwa hila zitakazofanya nchi isitawalike ni anarchy na hakuna administration yoyote ile duniani itakayoruhusu hicho.
 
Elimu
Elimu
Elimu
Ndicho nilichokiona kwenye hoja kuntu za Zitto.
 
Acha kupotosha mzee, hakuna anayetaka kufanya maandamano nchi nzima, na hata kama ni maandamano yapo kisheria. Halafu hao wapinzani uliowataja wanapofanya hizo press wanakuwa wanafanya kuhusu na wanaishia wapi baada ya hizo press?

Sawa labda nikubaliane na upotoshaji wako. Inakuwaje ccm wao wanaweza kufanya mikutano bila bughudha? Kibaya zaidi hata wakati wa ufunguzi wa miradi ya maendeleo unaona inatumika kama ni mikutano ya ccm na kampeni za wazi? Kinachofanyika hapa nchini japo unajaribu kuficha kichwa kwenye mchanga kama mbuni, tuna rais asiyeweza siasa za ushindani full stop. Hayo mengine unayoleta hapa ni mbwembwe tu.
 
Kuna kitu kinaitwa "the bully pulpit".

Raisi kama mtawala anayo hiyo privilege ya kutembea nchi nzima na kutoa hotuba na aghalab huingiza siasa. Haya ndio marupurupu walionayo washindi wa uchaguzi.

Kama CDM, CUF au chama kingine kikishinda uchaguzi watakuwa na hizi privileges pia.

Wanasema "elections have consequences"

Lakini usemi wa nyie vijana wa leo mnasema:

Don't hate the player, hate the game.
 
Kwa nini hawaleti hoja hizo bungeni? Au kama bunge hawaliamini kwa nini badala ya kutukana (na kupinga kila kitu anachofanya Magufuli) majukwaani, mitandaoni na kwenye mikutano majimboni hawazileti hizi sera mbadala watu wakazikia?

Kelele zote tunazozisikia toka kwa viongozi wa upinzani yani hawawezi kuchomekea hata vito vichache vya sera zao?

List ya mafisadi ilipopelekwa bungeni nini kilitokea? Ilipita? Ilipopelekwa kwenye mkutano wa hadhara pale Mwembeyanga nini kilitokea? Au hukuwa umezaliwa?
 
Mzee kifyatu nikikuambia ww pamoja na elimu yako unaishi kwa hasara sidhani kama nitakuwa nakukosea heshima. Umeambiwa wapinzani wananyimwa nafasi ya kufanya siasa nchi nzima ww unasema walete sera zao mtaani tuzielewe.

Huko bungeni unasema wapeleke sera zao, sitaki kuamini hili unaweza kulizungumza hadharani, mbele ya spika wa ccm akupe nafasi ya kuonyesha sera zako mpinzani mpaka wananchi wakuelewe? Kwenye bunge ambalo waziri au mbunge akiongea anaambiwa aongee kwa kifupi kwa sababu ya muda? Kweli sio bure nchi yetu ni masikini na ww unathubutu kuweka elimu yako hapa hadharani bila aibu.
Vijana wazamani kama Kifyatu na wa aina kama yeye ndio wametuleta hapa tulipo sasa.Mhandisi haeleweki na anachozungumza kabisa.Nadhani wahandisi ni vizuri wahusike katika kazi za kubuni miundo mbinu na kuboresha iliyopo kwa kufuata dira kwa mahitaji ya baadae. Dar es salaam na Dodoma inawatosha kuwa busy kiasi cha kutohusika na mambo mengine la sivyo wataleta uhandisi kwenye siasa matokeo ndo haya.............unless kwa wahandisi wenye vipawa vya siasa na uongozi haiwezekani kwa kila mhandisi kujua siasa.
Na sidhani kama kukaa Marekani miaka 32 na anakuja na hoja kama hizo za ajabu ajabu.Hao ndio tuliokuwa tunawategemea kutuendeleza angalia tu comments zake.Hana na hajai kwa sisi tuliokaa Tz kwa miaka 32.Mzee rudi tu America,hukuwezi huku kabisa.Na kwanza sijui ulikuwa unahusika na nini huko America?? Kama ni ubunifu basi ilikuwa kazi ngumu sana kueleweka huko ulikokaa miaka hiyo yote. Na maadili yakuanika elimu yako sjui umeyatoa wapi anika IQ hizi elimu za publication ni taabu sana.
 
Spika Ndugai anazidi kujidhalililisha, eti badala ya kujiongeza anafuata akili za Msukuma.
 
Back
Top Bottom