Zitto Kabwe: Tatizo la umeme leo ni siasa za mwaka 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe: Tatizo la umeme leo ni siasa za mwaka 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Edson Zephania, Jul 20, 2011.

 1. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leo katika wall yake ya facebook ameandika "Idris Rashid alitoa tamko kuhusu umeme mwezi Machi 2009, Raia Mwema wamerudia tamko lile leo Uk 13. Jisomee! Tatizo la sasa la umeme ni siasa za mwaka 2009".

  Wadau kama kuna mtu aliyesoma hilo gazeti atuwekee hilo tamko tulione.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Zitto hakukosea Idriss Rashid alikuwa mzalendo na aliona mbali ila mafisadi na wanasiasa waliona anaingilia biashara zao za umeme uchwara. Kwa ufupi, tungelimsikiliza Dr Idriss Rashid tusingelikuwa hapa but watu wakaamini maneno ya mafisadi ndio tuvumilie tena. Wengine wameanzisha biashara za kuuza solar panells majumbani zinauzwa milioni 1.6- milioni 3 kutoka india na china. Symbion nao wanalipwa billioni zao kwa mwezi. IPTL nao wanapata bilion zao ndio hivyo tena Tanzania Shamba la Bibi.
   
 3. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  hakuna lolote suala la umeme bado ni kutaka kupeana ulaji tu ni ilianza muda mrefu kama suala ni mvua haikuacha kunyesha juzi ni miaka na miaka lakn umeme tulipata kama kawaida iweje leo ndio iwe mgao, je unajua kwamba zitto ni zao la akina lowassa na hata wakati anataka kugombea uenyekiti chadema ni hao akina lowassa walimdhamini hata kufikia kumpa hammer na nyumba masaki nani asiejua??? tusifanyane malimbukeni jaman
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo lenu baadhi yenu hamuangalii contents bali mnaangalia nani kasema (Miafrika ndio ilivyo). Ulimbukeni tulio nao ni kufikiria kila mtu mbaya na kuogopa kufanya maamuzi magumu. Nikikuuliza una kithibitisho cha unachokisema huna na tatizo la umeme wa tanzania sio mvua bali mipango mibovu ya serikali ya CCM tangu enzi za mwinyi. Sasa CEO wa Tanesco alipoliona akawa anataka kuwasaidia wadanganyika mafisadi wakaona bora wamuondoe kwani atawaharibia mirija yao ya miradi ya umeme.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  idis rashid the best ceo of tanesco ever
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hata kutembeza bahasha alikuwa the best ever.
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Idriss Rashid alikuwa MDINI tu
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hebu fafanua udini wake mkuu au una chuki na CEO muislamu???
   
 9. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  umeme na siasa vinaendana vipi? someone has to draw a line please, mmezidi sasa
   
 10. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nimesoma kwa kina article katika gazeti la Raia Mwema na kwa kweli ilikuwa ni taarifa ya Idriss Rashid kwa vyombo vya habari kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans. Kwenye paragraph ya pili kutoka mwisho ameandika nanukuu " Ni imani yetu kwamba tumeshajieleza na kujenga hoja za kutosha, na wananchi wa Tanzania watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, mahspitali hayatoi huduma, viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu tulishindwa kufanya maamuzi".

  Siasa za CCM za uraisi wa 2015 ndizo zinalitesa taifa kwa sasa. Serikali inaogopa kufanya maamuzi na kusikiliza porojo za wale jamaa wa CCJ (Sitta na Mwakyembe), sasa tupo hapa tulipo ambapo Dr Idriss alitabiri. Sasa nani wa kuchukuliwa hatua. Wananchi ni lazima tuamue sasa or never.

  Serikali ya CCM imechoka na imechoshwa na malumbano ya kisiasa ndani yao wenyewe, ndiyo maana huoni ajabu Mh Sitta kwenda Mbeya kwenye mkutano wa hadhara na kumsema vibaya waziri mwenzake (Ngeleja ) kana kwamba yeye si sehemu ya serikali. Ufalme wa CCM umefitinika na sharti uondolewe madarakani. Na hii si ya kusubiri 2015, tutakuwa tumechelewa mno, wanatakiwa waondolewe sasa tena kwa nguvu.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 11. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  Kwa Faida ya wana Jamvi.
  Mwezi Disemba 2008 tanesco iliwasilisha Wizara ya Nishati na Madini tathimini ya hali ya uzalishaji ya umeme nchini kwa wakati huo.
  Na kwamba mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa megawati 745 kila mwaka na kwa wakati ule nakisi ni 150 megawati.
  Hatua iliyopendekezwa na Tanesco .Mosi Tanesco ilipendekeza ununuzi wa mitambo ya Dowans na ikaenda mbele na mapendekezo ya fuatayo

  1.Kuhakikisha megawati 45 za tegeta na megawati 200 za kiwira zinaingia kwenye mtandao,na ikibidi serikali iongeze nguvu kwenye uwekezaji.
  2.Uzalishaji wa chanzo cha maji cha Ruhuji ufanyiwe kazi haraka kwa kuwa uwekezaji wa mitambo ya maji unachukua miaka mingi na ili Ruhuji iongeze megawati 350 kwenye mfumo wa umeme ifikapo 2015 taratibu nyingi inabidi ziwe zimekamilika mwezi Machi 2009.
  3.Mradi mwengine mkubwa na umeme utokanao na Gesi asili ya mnazi Bay megawati 300 ulitarajiwa kuingia kwenye mtandao 2012 umekwama kutokana na matatizo ya kiuchumi duaniani na taasisi za fedha ambazo zimewafanya wawekezaji wakubwa wa mradi huo kuendelea

  Giza alilolitabiri Dr.Idriss Rashidi miaka miwili iliyopita.Raia Mwema Julai20-Julai 26 2011
   
 12. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako mdondoaji una mapenzi binafsi na mtu hata kama akikosea kwako sawa tu huyo Zitto na Dr idrissa lao lilikua moja tu kuingiza nchi katika mtego wa kuilipa ile kampuni kwa kisingizio cha kununua mitambo mbn nchi kama ya senegal imeweza kuleta umeme kwa siku moja tu tena baada ya maandamano au nao unataka kusema wamnunua mitambo chakavu kama unavyotaka tumia ubongo badala ya spinal cord kufikiri bana zitto alikua ana interest katika hilo
   
 13. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ubinafsi tu ndiyo unatupeleka kubaya! God have mercy!
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hebu nieleze wapi nimesema nina mapenzi binafsi na mtu. Nilichosema mie ni kuwa tatizo la umeme la Tanzania ni systemic failure iliyoanza tangu utawala wa Mwinyi na kumalizia utawala huu. Dr Idriss aliliona hilo ndio maana wakapeleka mapendekezo serikalini na kuweza kulitatua both short term and long term. Kasome raia mwema mkuu utapata picha halisi kabla hujanilaumu.

  Maandamano ni fikra za mgando kwani hata mkiandamana hamtaweza kutatua shida ya umeme. Unamsingizia Zitto alikuwa na interest ukiulizwa wapi huna hata pa kuanzia acheni vitu vya kuzusha. Ndio maana nasema sisi watanzania baadhi yetu tuna fikra za mgando hata mtu akiwa na mawazo mazuri ya kutusaidia kujinasua basi ataangaliwa ni nani kama ni muislamu ataambiwa mdini au kama kabila fulani ataambiwa mkabila mwishoe tunabakia pale pale hatuendelei na wajanja wanazidi kututafuna kwa kutuingiza kwenye mikataba mibovu na vimradi uchwara vya umeme.
   
 15. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nachojua hata mitambo ya Dowans ingenunuliwa bado tungekuwa gizani tu............ Hii si issue kwa sasa kinachotakiwa ni CCM itoke imeshindwa kuongoza.
   
Loading...