Zitto Kabwe: Tamko la jana la Serikali ya Tanzania na Barrick Gold lililenga kupoza bei ya Dola, lakini soko limegoma...

Huyu Zitto naye ni walewale wachumi wa makaratasi ya kisiasa.

Yaani tamko la Rais wa nchi masikini kama Tanzania libadilishe exchange rate ya dola.

Tamko hilo linahusu share za Barrick na sio exchange rate. Ndio maana baada ya tamko hilo share za Barrick zimepanda thamani yake.

Ukiangalia utagundua trend za kimataifa zinaonyesha dola inapanda thamani yake kulinganisha na thamani ya pesa nyingine. Hili sio suala la Tanzania pekee. Hata thamani ya Pound ya Uingereza inashuka ukilinganisha na Dola. Vivyo hivyo Euro.

Angalia hata shilling ya Kenya, Uganda kwa dola jinsi ambavyo imeshuka. Kwa hiyo na nchi hizo zina uza korosho?

Hii nchi ina vituko vya wanasiasa!

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sorry mkuu lakini umeandika utumbo mtupu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema uwa dakitari asiyejuwa kazi na akawa hajui kuwa hajui ni hatari kuliko yule asie jua na akatambua kuwa hajui. Kma mkuu hutambui kuwa hujui mifumo ya uchumi inavyojiendesha, na unajiona unajua, basi wewe ni mtu hatari sana.
 
Huyu Zitto naye ni walewale wachumi wa makaratasi ya kisiasa.

Yaani tamko la Rais wa nchi masikini kama Tanzania libadilishe exchange rate ya dola.

Tamko hilo linahusu share za Barrick na sio exchange rate. Ndio maana baada ya tamko hilo share za Barrick zimepanda thamani yake.

Ukiangalia utagundua trend za kimataifa zinaonyesha dola inapanda thamani yake kulinganisha na thamani ya pesa nyingine. Hili sio suala la Tanzania pekee. Hata thamani ya Pound ya Uingereza inashuka ukilinganisha na Dola. Vivyo hivyo .

Hii nchi ina vituko vya wanasiasa!

Sent from my iPhone using JamiiForums

Na wewe hujamuelewa Zitto. Hakuwa na maana influence iwe kwenye dola huko nje ila hapa ndani maana anauza dola akijua supply inaongezeka anaweza kushusha bei na hivyo kuonekana shilling ime-gain. Plain simple
 
Huyu Zitto naye ni walewale wachumi wa makaratasi ya kisiasa.

Yaani tamko la Rais wa nchi masikini kama Tanzania libadilishe exchange rate ya dola.

Tamko hilo linahusu share za Barrick na sio exchange rate. Ndio maana baada ya tamko hilo share za Barrick zimepanda thamani yake.

Ukiangalia utagundua trend za kimataifa zinaonyesha dola inapanda thamani yake kulinganisha na thamani ya pesa nyingine. Hili sio suala la Tanzania pekee. Hata thamani ya Pound ya Uingereza inashuka ukilinganisha na Dola. Vivyo hivyo .

Hii nchi ina vituko vya wanasiasa!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Thamani ya Euro kwa $ imeendelea kuwepo pale pale 1.13
 
Somo kidogo:

Kwenye uchumi matamko na hata vifo wakati mwengine huweza kuchangamsha bei, haswa bei za fedha za kigeni au bei za hisa. Tamko la jana la Serikali ya Tanzania na @BarrickGold lililenga kupoza bei ya Dola. Lakini soko limegoma na leo dola imefungua na shs 2415 .

Watanzania mjue Haya ni matokeo ya Mambo 2 makubwa.

- Moja, maamuzi ya hovyo Kuhusu Zao la Korosho ambalo ni zao kiongozi katika kuleta fedha za kigeni
- Mbili ni ubinywaji wa Demokrasia kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, kuwabambikia kesi wanasiasa wa upinzani ikiwemo kupigwa risasi Tundu Lissu na Kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa hivyo kupelekea wafadhili kutoleta fedha za kigeni nchini.

Nini matokeo ya Hali hii? Serikali itashindwa kulipa wakandarasi wa miradi yake mikubwa au kama ikiwalipa basi ita default malipo ya madeni yaliyowiva au kuchelewesha mishahara ya watumishi wa umma.

Serikali itafanya nini? Nionavyo, Kwa kuwa Serikali hii ni kiburi itaamua kukopa kutoka benki za nje kwa fedha za kigeni ili kuficha aibu kwa Wananchi na hivyo kuingiza nchi kwenye madhara makubwa zaidi. Ushauri wangu?

Serikali ikubali uchunguzi huru wa shambulio la Lissu na kuachia vyama vya Siasa Kuwa huru kufanya siasa ikiwemo kufuta kesi zote za kisiasa dhidi ya wapinzani.

Muhimu zaidi Rais kama Mkuu wa Nchi aombe kikao na Maalim Seif kupata suluhisho la haki ya Wazanzibari kupata Serikali waliyoichagua Oktoba 25, 2015. Ikishafanya Hivi Serikali iwaombe baadhi ya wanasiasa kwenda kwa Donors kuomba waachie misaada.

Pili Serikali iache kubana Sekta binafsi ili uwekezaji uje nchini na kuongeza inflows za fedha za kigeni. Mabadiliko makubwa yafanyike Wizara ya Fedha na Benki Kuu ili kuweza kutekeleza sera bora za Uchumi na Rais amwombe Prof. Ndulu kuwa Mshauri Mkuu wa Uchumi kwa angalau mwaka mmoja.

Najua Rais magufuli hatafanya Haya licha ya yeye mwenyewe kujua hali ni mbaya sana kiuchumi. Akiendelea na sera zake, mtaniambia dola imefika ngapi tarehe kama hii mwezi machi.

Hizo hela za Barrick hawezi zipata na Acacia wameshasema hawajui hayo makubaliano ya Serikali na Barrick.

Kwa hiyo hakuna FOREX INFLOWS!
Dola imepanda kipindi cha JPM tu? Ndulu alivyokuwa Gavana, wapinzani wakiandamana n.k dola haikupanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Zitto naye ni walewale wachumi wa makaratasi ya kisiasa.

Yaani tamko la Rais wa nchi masikini kama Tanzania libadilishe exchange rate ya dola.

Tamko hilo linahusu share za Barrick na sio exchange rate. Ndio maana baada ya tamko hilo share za Barrick zimepanda thamani yake.

Ukiangalia utagundua trend za kimataifa zinaonyesha dola inapanda thamani yake kulinganisha na thamani ya pesa nyingine. Hili sio suala la Tanzania pekee. Hata thamani ya Pound ya Uingereza inashuka ukilinganisha na Dola.

Kiuchumi kupanda au kushuka kwa dola ukilinganisha na pesa ya nchi kuba faida na hasara zake.

Hii ni faida kwa wanaouza bidhaa nchi za nje lakini ni hasara kwa wanaonunua bidhaa kutoka nje.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Uwe unakubali kwamba kuna mambo huyajui, kwenye masoko ya kimataifa news zina effects kubwa. Mfano ukiona Trump katweet kwamba wanaiwekea China vikwazo utaona Dola inapanda thamani ghafla.

Kwa waliosoma forex nadhani watakuwa wameelewa sana anachomaanisha Zitto.
 
Dola imepanda kipindi cha JPM tu? Ndulu alivyokuwa Gavana, wapinzani wakiandamana n.k dola haikupanda?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata Enzi za Nyerere ilikuwa ikipanda lakini kwa Viwango gani baada ya Muda gani hiyo ndio Hoja ,kwa huyu Malaika wako ndio inapanda kwa kasi ya Dream linner..Dola inapopanda ina haribu mambo mengi sana wengine inatukatia Mitaji yetu so usiongee tu kwa sababu umeweza ku'long in Jamiiforums.
 
Hivi mnataarifa kuwa wajuvi wa masuala ya kifedha na uchumi kwa nchi zinazojitambua na kukwepa mitego ya kinyonyaji ya 'kimtaji/capitalism' wameanza kuachana na dola na sasa wanakusanya vito vya thamani kama dhahabu na Almasi na kadhalika!? Dollar, imeishapata mpinzania na mpinzani huyo atajiimarisha muda si mrefu.
 
Hata Enzi za Nyerere ilikuwa ikipanda lakini kwa Viwango gani baada ya Muda gani hiyo ndio Hoja ,kwa huyu Malaika wako ndio inapanda kwa kasi ya Dream linner..Dola inapopanda ina haribu mambo mengi sana wengine inatukatia Mitaji yetu so usiongee tu kwa sababu umeweza ku'long in Jamiiforums.
Huo ni mtizamo mmoja mtizamo mwingine ni kuwa watu Wana pesa sana wananunua vitu sana nje ya nchi ndio maana bei ya dollar inapanda.Kushuka dollar kwaweza kuwa sababu ya ulofa watu hawaagizi vitu nje sababu ya umaskini uliokubuhu demand ya dollar inakuwa hamna watu hela hawana.Kipi vizuri dollar ipande sababu watu Wana pesa au ishuke sababu watu malofa wa kutupwa hawawezi nunua vitu nje?
 
Pia kuna sehem niliwah kuhudhuria ktk shereh hali ilikuwa ngum nilikuwa na rafiki yng moja ambae hakuchangia kamati ikakaa wakapangwa watu wa5 ,akanza mmoja akaja akamuuliza unakunywa kinywaji gani akatamka akaondoka baada ya kupita mda akaja mwingine akamuuliza tena unatumia kinywaji gani akamjibu akaondoka hd mtu wa 5 anakuja kumuuliza sherehe ndo inamalizika na hakupewa kinywaji chochote ila alishiriki kuangalia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Zitto naye ni walewale wachumi wa makaratasi ya kisiasa.

Kwa hiyo kwa akili za Zitto huyo CEO wa Barrick aliitwa kuja kupoza bei ya shilingi kwenye dola? Hii ni zaidi ya fikra za ki-comedy.

Yaani tamko la Rais wa nchi masikini kama Tanzania na kampuni ya Barrick libadilishe exchange rate ya dola!

Tamko hilo linahusu share za Barrick na sio exchange rate. Ndio maana baada ya tamko hilo share za Barrick zimepanda thamani yake.

Ukiangalia utagundua trend za kimataifa zinaonyesha dola inapanda thamani yake kulinganisha na thamani ya pesa nyingine. Hili sio suala la Tanzania pekee. Hata thamani ya Pound ya Uingereza na pia Euro inashuka ukilinganisha na Dola.

Kiuchumi kupanda au kushuka kwa dola ukilinganisha na pesa ya nchi kuba faida na hasara zake.

Hii ni faida kwa wanaouza bidhaa nchi za nje lakini ni hasara kwa wanaonunua bidhaa kutoka nje.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Siku Zitto akifufua zao la michikichi huko kwao Kigoma hadi akazalisha kuliko Malaysia nitaamini kweli ni mchumi jasiri wakupewa nishani ya Nobel,lakini nikiendelea kusikia kwanini hazalishi akitegemea kukinga bakuli toka serikali kuu nitampa pole,kwani kazi ya mbuge ni zaidi ya tweet
 
Back
Top Bottom