Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa kati ya April na June 2017 tofauti na Taarifa ya Serikali. Fuatilia Press Conference Mbunge Zitto Kabwe kuanzia saa sita kamili mchana.
======
UPDATES..
Waandishi wa habari kutoka Vyombo mbalimbali vya utangazaji wameshafika Makao Makuu ya ACT Wazalendo. Sayansi - Kijitonyama. Tutakuwa live muda mfupi ujao baada ya wahusika kufika.
---------
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Zitto Kabwe tayari ameshafika..
View attachment 619056
Zitto ameanza kuongea..
Oktoba 20, 2017, Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo ilifanya kikao Dar kujadili hali ya kisiasa na kiuchumi ya Taifa letu.
Kamati ya Uongozi ilitaarifiwa juu ya shaka ya kitakwimu za Ukuaji wa Pato la Taifa zilizotolewa BoT kati ya Aprili – Juni 2017.
Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa (contraction) kati ya Aprili na June 2017 tofauti na taarifa ya Serikali.
Tumetumia taarifa za takwimu za Serikali kuchambua hali halisi, hatuvunji Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015.
"Shaka iliyokuwapo juu ya kupikwa kwa takwimu za ukuaji wa GDP ni halali, ni ya kweli na sasa tuna ushahidi".
Taarifa ya mwisho ya Mapato ya Serikali iliyotolewa na TRA ni ya kupikwa haina uhalisia. Nafahamu uchumi una lugha isiyo rafiki kwa walio wengi lakini nitajitahidi kutumia maneno rahisi ili wote tuelewane.
Pato la Taifa (GDP) ni jumla ya mapato ya watu wote waliopo katika nchi au taifa husika katika kipindi maalumu,hususani mwaka 1. GDP ni kipimo cha uhai wa Uchumi wa Taifa kwani ukuaji au uporomokaji wake hutumika kupima shughuli za kiuchumi za Taifa husika. Ukisikia GDP ni (+) maana yake kuna shughuli za uchumi zimeongezeka, Na (-) maana yake ni kuwa shughuli za uchumi zimepungua.
Kwa Tanzania, tuna utaratibu wa kutoa takwimu za GDP kila baada ya miezi mitatu ambapo huita robo. Mwaka mmoja una robo nne.
Tafiti zinaonyesha kuwa ili kuondoa umasikini wa Tanzania, uchumi wetu unatakiwa ukue zaidi ya 10% kwa miaka kama 5 mfululizo. Uchumi wa Tanzania haujawahi kukua kufikia 10% wakati wa utawala wote wa CCM. Kwa muda sasa, wastani wa ukuaji umekua ni 7%.
Thamani ya bidhaa zilizouzwa kwenye nchi nzima hupatikana Kwa kuzidisha wastani wa bei na mzunguko wa bidhaa (transactions). Nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita, mzunguko wa fedha umekuwa ni kati ya asilimia 0.5 na 1.5.
Je, Pato la Taifa kwa mwaka 2015 na 2016 lilikuaje? Wananchi wanalalamika "Vyuma vimekaza. Ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuwaje tuna GDP inayokua wakati wananchi wanalia?
Takwimu za makusanyo ya kodi za serikali kutoka TRA zinaacha mashaka makubwa mno kwani ni takwimu za kutengenezwa.
Kusinyaa kwa ukuaji wa uchumi kutokana na sera mbaya za Serikali, kumesababisha makusanyo ya Mapato ya Serikali kushuka mno.
Baada ya maelezo haya, mtakubaliana nami kuwa takwimu za Pato la Taifa Kwa robo inayoishia Juni 2017 si takwimu sahihi. ZIMEPIKWA!
-----------
*Nyaraka za ushahidi zimeambatanishwa katika mfumo wa PDF